Mayunga yuo wapi? Nini kimemsibu kisanii?

Mayunga yuo wapi? Nini kimemsibu kisanii?

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
Wakuu nadhani kwa wenye kumbukumbu za huyu dogo anaitwa Mayunga aliwahi kushinda shindano la Africa nadhani ilikuwa Project fulan hivi siikumbuki vizuri, ila alivyoshinda alibahatika kufanya Ngoma na msanii Akon chin ya Marvin music, cha kushangaza na kilichouma zaidi siku ya fainali dogo anachukua kijiti alipokea taarifa ya Msiba wa Mama yake Mzazi,

Kusema kweli huyu Bwana mdogo ingefaa awe miongoni mwa wasanii wakubwa Tz, maana alibahatika kufanya ngoma msanii mkubwa Akon ngoma inaitwa Don't go Away, na alishoot video na video vixen ambae alishawahi kufanya kazi na star mkubwa Duniani Chriss Brown (Breeze).

Chakushangaza huyu bwana mdogo licha ya kula shavu nono na kutegemea tutaendelea kumuona anafanya vizuri ila cha ajabu huyu Bwana mdogo amebaki tu akionekana anakula Bata sana na hana Hit song yoyote ila anaonekana ni mtu yuko vzuri sana kimaisha,

Ila mwanzoni kipind anashiriki hili shindano alikuwa anaonekaa mganga njaa hata picha za marehem mama yake mzazi aliefariki siku ya fainali ukimuangalia unagundua kabisa hakuwa mama mwenye maisha ambayo sasa kijana wake anaishi.

Hapa ninachojiuliza ni kwamba dogo alivuta mkwanja wa maana kwenye shindano ndio maana anaonekana akila bata au anaishi katika mziki na anapiga show huku mjini zinazomuingizia pesa

IMG_20220324_164022_449.JPG
IMG_20220324_163817_473.JPG
IMG_20220324_163740_969.JPG
 
Mwache dogo aenjoy life..ulitaka asile bata?

Nakushauri jikite kusaka pesa ili uache kuonea wivu wanaume wenzako wakila bata.

#MaendeleoHayanaChama
Ila watu wa Jf mmesha changanyikiwa saa kila kitu tafta pesa, ujinga gani huo, mwenye pesa hafi, kwamba mwenye pesa hazeheki, mwenye pesa haendi chooni kukata gogo kama wengine, acheni ushamba
 
Naona aliunganishwa kweli kile chama kilichotaka kumchukua mama Kanumba
 
Cha msingi dogo ale kuku wake mtu yoyote asimbugudhi.

Kila mtu ale kuku wake.
 
Mwache dogo aenjoy life..ulitaka asile bata?

Nakushauri jikite kusaka pesa ili uache kuonea wivu wanaume wenzako wakila bata.

#MaendeleoHayanaChama
mkuu kwa taarifa yako sina njaa na simuonei wivu nataka kujua anachokifanya maana hata Mimi biashara zangu wanaonijua wanajua ninafanya nini na wakiulizwa watasema ninachofanya ovar maswala ya wivu hakuna aliyeyasemea hapa
 
mkuu kwa taarifa yako sina njaa na simuonei wivu nataka kujua anachokifanya maana hata Mimi biashara zangu wanaonijua wanajua ninafanya nini na wakiulizwa watasema ninachofanya ovar maswala ya wivu hakuna aliyeyasemea hapa
Ungemuuliza mhusika angekujibu btw ukijua anachokifanya itakusaidia nini.

Mtu ale bata kwa hela yake mwingine akereke?

Eeh jaman acheni hizo bana
 
Back
Top Bottom