Nyie ioneni nzuri hivo hivo ila mziki wake wake sio wa kitoto, nilishawah kupost khs hii gari, ngoja nii re-post hapo chini tena.
Asee nilinunua Mazda rx 8 ya 2005, ilikua inatumia rotary engine, manual, ni cc 1300 only lkn inatoa zaid ya horse power 200 na zaid. Tatizo kubwa la rotary engine ni "FLOODING" hapo ndo kwenye shida Sana. So kwenye rotary engine haitakiwi gari asubuh kuiwasha na kuondoka hapohapo unaiacha kwanza inachemka then ndo unaondoka na ukija kuipaki usiizime pia hapohapo. Na ili idumu atleast kila siku lazima uhakikashe gari inakimbizwa mpk mshale ufike kwenye redline, kwangu ilikua ni rpm 9000 ukifanya hivyo inadumu. Lkn since pia Rotary engine haitumii piston inakula engine oil saana saaana lkn ni engine yake ina nguvu Sana. Kwa wale wanaodhani eti ukubwa wa engine unachangia ulaji wa mafuta mnajidanganya hii Mazda rx 8 ilikua ni cc 1300 lkn lita 1 km8 highway na lita 1 km 6 kwenye foleni sababu ni sports car. Imagine cc 1300 lkn subaru forester, alteza sijui vi sport car zilikua hazikatizi mbele ya gari yangu. Ooh I will miss my Mazda