Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MAZIKO YA ABDULWAHID SYKES 1968
Mazishi ya Abdulwahid Sykes yalifanyika siku ya Jumapili tarehe 13 Okrtoba, 1968.
Mazishi yake yalikuwa makubwa yasiyo kifani.
Ukitoa mazishi ya mwaka wa 1950 ya Sheikh Idrissa bin Saad, muasisi na Khalifa wa Tariqa Askariya na mazishi ya Sheikh Kaluta Amri Abeid mwaka 1963, Dar es Salaam ilikuwa haijapata kushuhudia mazishi kama hayo.
Gerezani yote ambako Abdulwahid aliishi katika utoto wake na mahali ambapo alianza harakati zake dhidi ya Waingereza, kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa kama vile imesimama hakuna kinachoendelea ila maziko ya Abdulwahid.
Hii ilikuwa pamoja na sehemu nyingine zilizozunguka Kariakoo kama Misheni Kota na Kisutu.
Gerezani kwa hakika ilikuwa na mwito wa pekee. Ilikuwa ni kutoka Gerezani ndipo walipotoka wanaharakati wa mwanzo waliounda TANU ukimtoa John Rupia.
Siku hiyo Gerezani ilikuwa imekuja kumzika shujaa wao.
Watu walianza kukusanyika nyumbani kwa mama yake, Abdulwahid Bibi Mruguru bint Mussa mapema asubuhi ambako maiti ilipokuwa imepelekwa.
Ilipofika adhuhuri ikawa kama vile Dar es Salaam nzima imekusanywa pale.
Chifu wa Unyanyembe Abdallah Said Fundikira, ambae Abdulwahid alisomanae darasa moja katika shule ya Kitchele mjini Dar es Salam katika miaka ya 1930 na mtu ambae walikwenda wote kuhiji Makka alikuja Dar es Salaam kwa ndege kutokea Nairobi kuja kuhudhuria mazishi.
Wakati ule Chief Fundikira alikuwa Mwenyekiti wa Shirila la Ndege la Afrika ya Mashariki.
Rais Nyerere alikuwa mmoja wa watu waliokwenda kuomboleza kifo cha Abdulwahid.
Watu wa itifaki walimuweka Nyerere jamvi moja na Ahmed Rashad Ali na walikula chakula sinia moja.
Akitembea kwa miguu Nyerere alilifuata jeneza la Abdulahid nyuma kutoka Mtaa wa Lindi, Gerezani hadi Msikiti wa Kitumbini maiti ilipokwenda kuswaliwa swala ya jeneza kama ilivyo ada ya Kiislam.
Pale Kitumbini, Nyerere alisimama nje ya msikiti pamoja na wananchi wengine kungojea maiti ilitolewe nje.
Mfanyabiashara mmoja wa Kiasia kuona Rais amesimama wima, kwa ajili ya heshima alileta kiti na kumuwekea Nyerere akae. Nyerere alikataa kukaa na akawa amesimama pamoja na watu wengine.
Kutoka Kitumbini msafara wa maziko ulielekea makaburi ya Kisutu kwa ajili ya mazishi.
Wakati huu wote wakielekea makaburini, Nyerere alikuwa nyuma ya jeneza kichwa chake amekiinamisha na kila wakati alionekana akifuta macho yake na kitambaa.
Nyerere alikuwa analia.
Ilikuwa mwaka 1952 Abdulwahid alipofahamiana na Nyerere na yeye Abdulwahid akamjulisha kwa watu mashuhuri wa Dar es Salaam - Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mwinjuma Mwinyikambi, Mohamed Jumbe Tambaza, Omar Londo, Rajab Diwani, Mshume Kiyate, Bibi Tatu bint Mzee, Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bibi Asha Ngoma, Bibi Titi Mohamed, Bibi Hawa bint Maftah, Bibi Khadija bint Kamba, Said Chamwenyewe na wengi wengine.
Ilikuwa na kutokana na msaada wa Abdulwahid na wazalendo hawa ndiyo uliomuwezesha Nyerere kuwa katika siasa za Dar es Salaam, kuchukua uongozi wa TAA 1953 na mwaka wa 1954 TANU ikaundwa na Nyerere kuchukua uongozi wa nchi miaka tisa baadae.
Hakuna aliyeweza kukisia ni mawazo gani yalikuwa yanapita katika fikra za Nyerere.
Lakini ni wazi kuwa alikuwa akimfikiria Abdulwahid na jinsi pamoja walivyoweza kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Ilikuwa miaka15 iliyopita katika Ukumbi wa Arnatouglo, si mbali na pale alipokuwa, Nyerere aligombea urais wa TAA dhidi ya Abdulwahid.
Wote wawili wakiwa vijana wadogo.
Abdulwahid akiwa na umri wa miaka 30 na Nyerere akiwa na miaka 32.