Mzee Mohamed, sitaki kuamini kuwa CCM hawatambui mchango wa Abdul Sykes mpaka TANU ikazaliwa na kisha tukapata uhuru.
Yawezekana tu uzembe wa watu wasiojitambua ndio walifanya makosa ya kutoingiza habari zake Abdul.
Lakini pia napingana na wewe kuwa mchango wa akina Sykes pekee ndio ulikuwa sababu kubwa ya kulete mafanikio ya kuzaliwa TANU.
Mfano unajikita kueleza jinsi Dockworkers union ilivyokuwa na ushawishi chini Abdul kiasi cha kuipa sapoti TANU huku ukisahau kulikuwa na colonial service union nyingi za kiafrika ambazo pia zilitoa sapoti kwa TANU. Mfano chama cha wafanyakazi wa reli na vingine vingi vilileta mchango mkubwa.
Pia hutaki kukubali ukweli kuwa sio akina Sykes tu pekee waliounganisha watanganyila ka kisaha AA ikapatikana mwaka 1929.
Hutaki kukubali kuwa Martin Kayamba ambae aliplay big role mpaka AA ikazaliwa alitoa mchango mkubwa kisa tu ni mkristo.
Lakini tambua kuwa ni vitabu vichache sana vilivyoandika juu ha Martin Kayamba.
Maandiko yako yako very biased kiasi cha kutia shaka.
View attachment 1797745
Idu...
Ndiyo nasema kuwa unapenda kujadili historia hii lakini bahati mbaya huna ujuzi wa mengi katika somo hili.
Chukua muda uisome hii historia ndipo uje tufanya mjadala.
Kuondolewa majina ya Abdul Sykes, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate kwa kuwataja wachache katika historia ya TANU haikuwa uzembe.
Hili lilikusudiwa.
Hassan Upeka aliyekuwa mmoja wa watafiti na waandishi wa historia hiyo chini ya Chuo Cha CCM Kivukoni anasema kuwa Dr. Mayanja Kiwanuka aliyekuwa kiongozi wa jopo alikataa kupokea taarifa za Abdul Sykes.
Haya nimeyaeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Hiyo book review ya Brian Eccles naifahamu sana.
Nyingine ni ya John Iliffe, James Brennan na Jonathan Glassman katika Cambridge Journal of African History.
Sishangai aliyoandika.
Ila nashangaa kwa nini hakueleza kuwa kweli hao, '' Abdul Muslim associates,'' hawamo katika historia lau kama mchango wao ni muhimu.
Yawezekanaje kuwa baba na watoto wake wote wameshika uongozi katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na wote hawamo katika historia ya TANU?
Baba muaisisi wa AA na wanae wote waasisi wa TANU.
Tuje kwa Martin Kayamba.
Martin Kayamba hakuhusika katika kuunda AA.
Hili si jambo la sisi kuvutana.
Kleist Sykes kawataja wote walioasisi AA katika mswada wa kitabu alioandika kabla hajafa.
Sasa mswada huu ni kitabu: Daisy Sykes Buruku, ''Kleist Sykes The Townsman,'' ''Modern Tanzanians,'' Ilife (Ed) 1973.
Kleist Sykes yuko pia katika Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press, New York, 2011 na mwandishi wa maisha yake ni Mohamed Said.
Nahitimisha kwa kukufahamisha kuwa gazeti la Africa Events lililokuwa na makala yangu, ''In Praise of Ancestors,'' lilikusanywa lote na kutolewa katika mzunguko lisisomwe.
Kama nilivyosema sikulazimishi kuniamini katika haya ninayokueleza muhimu kwangu ni kuwa nimekueleza ule ukweli ninaoufahamu na yale yaliyonifika katika kusahihisha historia ya TANU.
Kleist Sykes muasisi wa AA 1929, Abdul, Ally na Abbas waaisi wa TANU 1954 kadi no 2,3, na 7.
Nina mengi katika historia ya TANU.