Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #21
Idu...Ok fine mzee Mohamed utahojiwa na Clouds Tv na Abdul Sykes ni mmoja wa waasisi wa African Association alikuwa muislamu. Je hii ni justification kuwa waislamu pekee ndio walipigania uhuru wa Tanzania?
Utumwe mwandishi makini hapa Tanzania utamtaja Massoud Kipanya?
Historia iliyokosewa na akina nani? Nani hapa Tanzania hajui kuwa kulikuwa na African Association, ambayo akina Sykes walihusika kuiunda. Nani hajui kuwa baadae palikuja kuwa na TANU.Idu...
Mimi nimesahihisha historia iliyokosewa.
Tena nimeandika historia ya wazee wangu.
Sioni tatizo liko wapi.
Hayo mengine sidhani kama yanahitaji mimi kujadili na wewe.
Idu...Historia iliyokosewa na akina nani? Nani hapa Tanzania hajui kuwa kulikuwa na African Association, ambayo akina Sykes walihusika kuiunda. Nani hajui kuwa baadae palikuja kuwa na TANU.
Hoja hapa ni hili suala ambalo mnataka kulipotosha kuwa sababu Sykes alikuwa muislamu basi waislamu ndio walipigania uhuru wa Tanganyika. Mohamed Said mzee wetu hii sio sawa.
Mbali ya hayo mbona huweki mambo wazi kuwa kulikuwa na Tanganyika territory civil service association ambayo ilianzishwa na akina Martin Kayamba na kisha baadae kukawa na African Association?
Mbona unastick juu ya Dock workers association huku ukisahau hata mikoani kulikuwa na vyama vya waafrika kutetea maslahi yao?
Historia iliyokosewa na akina nani? Nani hapa Tanzania hajui kuwa kulikuwa na African Association, ambayo akina Sykes walihusika kuiunda. Nani hajui kuwa baadae palikuja kuwa na TANU.Idu...
Mimi nimesahihisha historia iliyokosewa.
Tena nimeandika historia ya wazee wangu.
Sioni tatizo liko wapi.
Hayo mengine sidhani kama yanahitaji mimi kujadili na wewe.
We mzee usipanic. Kabla ya AA 1929 kulikuwa hakuna taasisisi za kupigania maslahi ya waafrika? Kayamba unamuona kibaraka wa waingereza sababu alikuwa mkristu?Idu...
Martin Kayamba alikuwa kibaraka wa Waingereza.
Inaelekea huijui historia ya wazee wangu na taasisi walizoanzisha - AA 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933, Dockworkers Union 1948 na TANU 1954.
Wewe sasa andika historia za hivyo vyama vingine.
Sielewi vipi unahangaika na historia ambayo mimi nawaeleza wazee wangu.
Idu...Historia iliyokosewa na akina nani? Nani hapa Tanzania hajui kuwa kulikuwa na African Association, ambayo akina Sykes walihusika kuiunda. Nani hajui kuwa baadae palikuja kuwa na TANU.
Hoja hapa ni hili suala ambalo mnataka kulipotosha kuwa sababu Sykes alikuwa muislamu basi waislamu ndio walipigania uhuru wa Tanganyika. Mohamed Said mzee wetu hii sio sawa.
We mzee usipanic. Kabla ya AA 1929 kulikuwa hakuna taasisisi za kupigania maslahi ya waafrika? Kayamba unamuona kibaraka wa waingereza sababu alikuwa mkristu?
Sihangaiki na historia yako kisa tu wazee wako walishiriki.
Unatakiwa uweke wazi kuwa kulikuwa na taasisi nyingi zilizoundwa kutetea haki za waafrika. Sio Dockworkers union pekee kisa wazee wako walishiriki.
Pia unatakiwa uweke wazi kuwa TANU ilipatikana baada ya AA hivyo sio sababu ya kusema wazee wako walipuuzwa na kusahauliwa.
Mzee Mohamed samahani. Ila najua unafahamu kuwa sio wewe pekee ulieandika hitoria ya juu ya TANU na watu wanajua kuchekecha mambo.Idu...
Ukianza na hii ''We Mzee,'' ni kuwa umehamaki.
Sina sababu ya kuingia katika ugomvi.
Historia hii inanihusu mimi na nimeandika kitabu sasa kina miaka 23.
Kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni kimechapwa mwaka wa 1981 toleo moja.
Ktabu changu kipo toleo la nne.
Kiingereza toleo la pili Kiswahili la nne.
View attachment 1797509
View attachment 1797510
Idu...Mzee Mohamed samahani. Ila najua unafahamu kuwa sio wewe pekee ulieandika hitoria ya juu ya TANU na watu wanajua kuchekecha mambo.
Mzee Mohamed sijakupata. Yaani CCM haitambui kuwa akina Sykes walikuwa na mchango mkubwa kupatikana TANU? Hawafahamu kadi za TANU zilivyogawiwa kinamba?Idu...
Walikuwa wapi wakati Chuo Cha CCM Kivukoni wamechapa kitabu cha historia ya TANU 1981 na Ally Sykes kadi No. 2 Abdul kadi no. 3, Dossa kadi no. 4, Denis Phombeah kadi. 5, Dome Budohi kadi no 6 na Abbas Sykes kadi no. 7 wamefutwa?
Mbona hawajachekecha mambo?
Nitajie mwingine aliyeandika historia ta TANU.
Idu...Mzee Mohamed sijakupata. Yaani CCM haitambui kuwa akina Sykes walikuwa na mchango mkubwa kupatikana TANU? Hawafahamu kadi za TANU zilivyogawiwa kinamba?
Mzee Mohamed hii haingii akilini. Walikataa ili iweje? Mwl Julius alikuwepo na alifahamu ukweli wote.Idu...
Walipokuwa wanaandika kitabu cha historia ya TANU walipelekewa historia ya Abdul Sykes wakakataa kupokea.
Idu...Mzee Mohamed hii haingii akilini. Walikataa ili iweje? Mwl Julius alikuwepo na alifahamu ukweli wote.
Mimi nakataa naona mnatafuta justification ili mlete zile story zenu.
Mdukuzi,
Mdomo haumkatai bwana wake.
Mzee Mohamed narudia kusema. Mnatafuta justification juu ya lawama mnazoeneza.Idu...
Hapana shida mimi nakueleza nikijuacho kuamini au vinginevyo ni juu yako mwenyewe.
Mwaka wa 1985 Nyerere alotoa medali 3979 kwa Watanzania waliofanya makubwa nchini.
Jina la Abdul halikuwapo.
Kabla ya kutolewa hadharani majina hayo muulizaji alimuuliza Mwenyekiti wa kamati ya kutunuku medali.
Mbona majina ya fulani na fulani na fulani hayamo?
Yakawa hayamo.
Wamekataliwa.
Idu...Mzee Mohamed narudia kusema. Mnatafuta justification juu ya lawama mnazoeneza.
Mwl Nyerere akatae mchango wa akina Sykes?
Nnangale,Kaka kiswahili unakiweza
Mzee Mohamed sikubaliani na wewe kuwa Abdul alifutwa katika historia.Idu...
Kama nilivyokueleza.
Mimi naeleza ninayojua kufikia Abdul kufutwa katika historia.
Si lazima uamini.
Nina mengi.
Idu...Mzee Mohamed sikubaliani na wewe kuwa Abdul alifutwa katika historia.
Unataka kusema uislamu wake ndio sababu?
Mzee Mohamed, sitaki kuamini kuwa CCM hawatambui mchango wa Abdul Sykes mpaka TANU ikazaliwa na kisha tukapata uhuru.Idu...
Sikulazimishi kuamini niliyoandika lakini nimesoma kitabu cha Kivukoni historia ya TANU imeandikwa bila ya kuwemo Abdul Sykes.
Halikadhalika kitabu cha Abubakar Ulotu kitabu chake cha historia ya TANU Abdul hayumo.
Lakini sijui kama unajua.
Hiki kitabu cha Abubakar Ulotu ni kutoka mswada wa historia ya TANU kilichokuwa kinaandikwa pale TANU Office na Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu mwaka wa 1962 Nyerere akihusika.
Abdul akajitoa katika uandishi wa hiki kitabu.
Dr. Kleruu akaendelea na uandishi hadi ukakamilika lakini TANU hawakuweza kukichapa kitabu kile.
Abubakar Ulotu akachukua mswada ule kwa siri na bila idhini ya TANU akachapa kitabu kile na akaweka jina lake kama mwandishi.
Nina mengi.
Tusimame hapa.
Idu...Mzee Mohamed, sitaki kuamini kuwa CCM hawatambui mchango wa Abdul Sykes mpaka TANU ikazaliwa na kisha tukapata uhuru.
Yawezekana tu uzembe wa watu wasiojitambua ndio walifanya makosa ya kutoingiza habari zake Abdul.
Lakini pia napingana na wewe kuwa mchango wa akina Sykes pekee ndio ulikuwa sababu kubwa ya kulete mafanikio ya kuzaliwa TANU.
Mfano unajikita kueleza jinsi Dockworkers union ilivyokuwa na ushawishi chini Abdul kiasi cha kuipa sapoti TANU huku ukisahau kulikuwa na colonial service union nyingi za kiafrika ambazo pia zilitoa sapoti kwa TANU. Mfano chama cha wafanyakazi wa reli na vingine vingi vilileta mchango mkubwa.
Pia hutaki kukubali ukweli kuwa sio akina Sykes tu pekee waliounganisha watanganyila ka kisaha AA ikapatikana mwaka 1929.
Hutaki kukubali kuwa Martin Kayamba ambae aliplay big role mpaka AA ikazaliwa alitoa mchango mkubwa kisa tu ni mkristo.
Lakini tambua kuwa ni vitabu vichache sana vilivyoandika juu ha Martin Kayamba.
Maandiko yako yako very biased kiasi cha kutia shaka.View attachment 1797745