Peramiho yetu
JF-Expert Member
- May 25, 2018
- 5,303
- 14,983
Na habari zake n za waislamu tuuMzee hajielewi huyu ana udini sana...sasa hapo kuna watu wengi kuzidi misiba ya Mzee Nyerere, Kanumba na Rais John Pombe Magufuli??Muda mwingine tuweni wa kweli na wawazi hii mitandao isitudanganye kwa faida yako au dini yako
Peramiho...Na habari zake n za waislamu tuu
Mzee kifupi n mdini japo anamambo mengi ya manufaa kwa umma ila sipendi anapoingiza Sana udini
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Paris...No hard feelings kabisa nimependa unachofanya watu wengi tulikuwa hatujui kuhusu ukweli wa uhuru wa Tanganyika…kuhusu historia ya jiji la Dsm…na mambo mengi kuhusu watu wake wazawa….hongera sana na Mungu akubariki.
Impipi,Mzee ni kweli Tanzania all Muslim party ilikwamisha kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika mapema?
Kimo...nashindwa kuelewa watu wenye makasiriko..huyu mwandishi ana andika juu ya kile anachokifahamu kwa hadhira fulani anayoifahamu, anatoka mtu huko kavimbiwa viazi anamuamulia juu ya andiko lake.., ukiangalia mtiririko wa hao waliotangulia ni jamii fulani hivyo hiyo rekodi inahusu jamii fulani, sio nchi nzima jamani..mwacheni mzee wa watu atiririke, ndio humo humo kuna vitu na wengine tunajifunza.
We ndio mdini Sasa nyang'au we! IdiotMzee hajielewi huyu ana udini sana...sasa hapo kuna watu wengi kuzidi misiba ya Mzee Nyerere, Kanumba na Rais John Pombe Magufuli??Muda mwingine tuweni wa kweli na wawazi hii mitandao isitudanganye kwa faida yako au dini yako
Hata ukimdharau unampa kula? Au anatembea na mama yako?Mzee anajidanganya tu anatuona sote mazuzu,siki hizi namdharau sana,anazeeka vibaya ,anaandika ujinga ,udini unampofua,
Mzee mohamed said achana na hao vitoto vipuuzi ambao hawajielewi haoKizeze,
Kila mwandishi anakuwa na watu wake anaowaandikia.
Mimi nimetokana na jamii ya mjini Dar es Salaam na ninaponyanyua kalamu hawa ndiyo ninaowaandikia.
Hii sikuanza leo.
Wengi hapa JF wamenifahamu kwa kuandika historia ya watu wa pwani na mfano wa hao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Historia hii iligueza historia iliyokuwapo na kufunzwa shule za msingi hadi vyuo vikuu.
Niliamua kuandika historia hii kwa kuwa hakuna mtafiti aliyeiandika labda kwa kuwa si historia yao hivyo hawaijui au waliona haina umuhimu.
Wala mimi sikusema hawakuiandika kwa sababu ya udini.
Sikuona haja ya kukejeli wala kuandika maneno makali kwa sababu historia ya wazee wangu na jamii yangu haikuandikwa.
Wala sikughadhibika kuwa historia inayosomeshwa imetutupa nje.
Nilichofanya niliamua kufanya utafiti na kuandika.
Kilichonishangaza ni kuwa wako waliokujakunilaumu kuwa nimesukumwa kuandika kwa sababu za udini.
Hawa wote ni watu wa hapa nyumbani.
Nje ya mipaka ya Tanzania historia hii ilipokelewa vyema sana na nikaalikwa vyuo vingi kuzungumza.
Sasa ninapoandika historia ya maziko makubwa ninakusudia kueleza historia ya jamii yangu ifahamike ilikuwaje.
Hakuna anaekataa kuwa maziko ya Mwalimu Nyerere yalikuwa makubwa.
Lakini nitakuambia kitu.
Nyerere alipofika kwenye maziko ya Abdul Sykes hakuamini macho yake.
Alikuwa hajapata kushuhudia mazishi kama yale.
Sasa kama nisingeandika historia hii wewe ungeyajuaje haya?
Kuna mengi tungeweza kujadili kwa taratibu bahati mbaya historia hii inawapandisha hasira.
Ningeweza kuhadithia jinsi Mwalimu Nyerere na Mama Maria walivyopokelewa Dar es Salaam katika mitaa ya Kariakoo na wazee wetu na mapenzi yaliyokuwa baina yao.
Ningeweza kueleza maisha yalivyokuwa na mapenzi yaliyojengeka baina yao na kisa kilichomshtua Abdul Sykes siku ilipodhaniwa Nyerere kalishwa sumu katika chakula nyumbani kwake.
Mengi ninayo kwa kuwa ingawa mimi nilikuwa mtoto lakini ni sehemu ya historia hii na waliofanya haya ni wazazi wangu.
Halafu unatumia Tecno Fi! Wangoni bwanaNa habari zake n za waislamu tuu
Mzee kifupi n mdini japo anamambo mengi ya manufaa kwa umma ila sipendi anapoingiza Sana udini
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Huo ni urongo,kanumba,ruge na nyerere ndio maziko yaliyovunja rekodi acha kudanganya mzee mzima
Msoso...Mzee mohamed said achana na hao vitoto vipuuzi ambao hawajielewi hao
Anatembea na mama yako mzaziHata ukimdharau unampa kula? Au anatembea na mama yako?
Dau kwao kilwa sijui hao wengine wamanyema,wenye dar es salaam yao hapo hakuna kwenye listUwe unaelewa yanaongelewa maziko ya watu wa Dar Es Salaam hasa wa Magomeni na kariakoo
Key...Ukubwa wa Mazishi una vigezo vipi ? Labda tukianzia hapo ndio tutakwenda sambamba ya yapi ni makubwa na madogo ni yapi...., Ingawa sidhani kama kulinganisha ukubwa huu una tija sana.... Anyway asante kwa Taarifa
Sasa mkuu wewe Tozo hazijakukumba huko ulipo ? Nimekuomba tu vigezo vya ukubwa na udogo kama hautojali kwa sentensi chache wewe unaniambia nikatumie MB zangu chache za kudunduliza nikaangalie video..., Kweli tunatakiana Heri sisi kama Watanzania ?Key...
Sikiliza hii video naeleza maziko makubwa mwaka 1968 na yale yaliyokuwapo:
Thread 'Zumari: Maziko ya Abdul Sykes 13 oktoba 1968' Zumari: Maziko ya Abdul Sykes 13 oktoba 1968