nashindwa kuelewa watu wenye makasiriko..huyu mwandishi ana andika juu ya kile anachokifahamu kwa hadhira fulani anayoifahamu, anatoka mtu huko kavimbiwa viazi anamuamulia juu ya andiko lake.., ukiangalia mtiririko wa hao waliotangulia ni jamii fulani hivyo hiyo rekodi inahusu jamii fulani, sio nchi nzima jamani..mwacheni mzee wa watu atiririke, ndio humo humo kuna vitu na wengine tunajifunza.
Kimo...
Uchaguzi wa Kura Tatu mwaka wa 1958 ulisababisha farka ndani ya TANU na wa kwanza kujitoa katika chama alikuwa Zuberi Mtemvu akaunda African National Congress (ANC) chama hiki kikajulikana kama Congress katika umaarufu wake.
Wanachama wake wakaweka kibwagizo cha maneno haya katika kukisifu chama chao, ''Congress Jiwe Lisilovunjika.''
Baada ya Mtemvu kutoka TANU, Mashado Ramadhani Plantan na yeye akajitoa TANU akaunda All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT).
Hiki chama kilisababisha hofu kubwa sana na si tabu kuelewa kwa nini.
Zuberi Mtemvu chama chake kilikuwa kimesimama kwenye sera ya Afrika kwa Waafrika lakini chama cha Mashado Plantan kiliangalia maslahi ya Waislam baada ya uhuru hofu ikiwa Waislam kutotendewa haki na wale watakaoshika madaraka.
Kitu gani killisababisha hii shaka?
Ukoloni uliwanyima Waislam elimu, elimu ikawa katika mikono ya serikali na Wamishionari.
Ikawa wazi kuwa uhuru utakapopatikana watakaoshika madaraka ya kuendesha nchi watakuwa Wakristo.
Swali likawa, je hawa Wakristo wakiongozwa na Julius Nyerere watafanya uadilifu kuona kuwa Waislam wanatendewa haki na watapata fursa za elimu kama wengine?
AMNUT ikadai kuwa uhuru ucheleweshwe hadi pale Waislam watakapo kuwa na elimu ya kushiriki katika uendeshaji wa serikali.
Dai hili lilipingwa na TANU kwa mantiki kuwa hali ya baadae ya Waislam si suala la kujadiliwa na Waingereza waliokuwa wanaitawala Tanganyika.
Suala la Waislam hili litatatuliwa na serikali huru ya Tanganyika.
Huu ndiyo ulikuwa msimamo wa TANU na ahadi ya TANU kwa Waislam.
Katika hotuba yake maarufu ya kuaga alipostaafu aliyoitoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985 Mwalimu Nyerere aliwaeleza Wazee wa Dar es Salaam aliokuwa anawahutubia kuwa ametimiza ahadi yake ya kuleta usawa baina Waislam na Wakristo kiasi kuwa hawezi kujua waziri anayemteua ni Muislam au Mkristo.