Maziko ya Kifalme na faragha - Kinafanyika nini?

Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Posts
4,710
Reaction score
2,587
Alipofariki Nelson Mandera dunia nzima ilenda live kwa kipindi chote cha msiba na maombolezo, ilipofikia mwili kuwekwa katika nyumba ya milele kamera zilizimwa na tukaambia ni ndugu wa karibu tu ndio watakaoshiriki zoezi zima la kuzika.

Jana tena wakati Malkia anazikwa pamoja dunia kushiriki kuanzia msiba unaanza mpaka mwishoni tunaambiwa ndugu wa karibu na wanaohusika tu ndio wanamaliza. Sasa sie wananzengo tumebaki na maswali mengi mno kuhusiana na maziko ya wafalme, malkia. machifu na watemi wa huku kwetu.

Hadithi zetu za kale zilitwambia mfalme anazikwa na watu wa kumsindikiza na kumshikilia kaburini tena wakiwa hai vijana mashababi na mabint chuchu konzi. wahistoria mnatuambiaje Malkia kazikwa peke yake au kuna waliomsindikiza vipi siku hizi mbona inafichwa wakati zamani walikuwa wanahadithia.

Aliyetizama sinema ya shaka Zulu atanielewa na maanisha nini, lakini marehemu mzee wangu wakati akinipigia story za kwao unyamwezini watemi wao huko walizikwa na watu. Ukiungalia msiba wa malkia pasi na shaka taratibu zoote za maziko ya kale ya kifalme zilifuatwa ila mwishoni ndio watu wa karibu tu wamemaliza.

Ebu tukumbushane na kujuzana zaidi, JF ndio kwenye elimu yote nafungua mjadala hili hawa vijana wa 2000 waone tulipotoka.
 
Bibi eliza amezikwa na mme wake alikuwa akimsubiri, jana ndo wamelazwa wote sehemu moja😉. Kama kuna vijukuu vya kuwasindikiza labda watafute ambavyo havitoki ufalmeni maana vijukuu/ vitukuu vyao vyote tunavijua kama kimojawa tusipokiona siku za usoni tujuwe kilisindikiza.
 
Matambiko hakuna tofauti na hicho.
 
hawachukui katika wao, watu wanachukuliwa kutoka katika jamii ni ufahari mkubwa mwanao au ndugu yako kumsindikiza mfalme. Hii ni katika hadithi za kale. Ebu tafuta cinema au series ya shaka Zulu utaona haya tunayosema
 
hawachukui katika wao, watu wanachukuliwa kutoka katika jamii ni ufahari mkubwa mwanao au ndugu yako kumsindikiza mfalme. Hii ni katika hadithi za kale. Ebu tafuta cinema au series ya shaka Zulu utaona haya tunayosema
Kwamba sinema ya shaka zulu ndio iwe fact? Lakini Africa tuna mila za ajabu sana
 
Niliskia tule tu mbwa tuwili tunamsindikiza,ngoja tuone km vitaonekana mbele huko.
 
Kwamba sinema ya shaka zulu ndio iwe fact? Lakini Africa tuna mila za ajabu sana
sinema ni reference, kwa taarifa yako facts inaandikwa, ina hadithiwa na wengine wanacheza sinema ili vizazi vinavyokuja vione na kujua yaliyopita kabla yao. Muda ni mchache humu elimu iko kwa watu wengi utapata kwa njia tofauti.
Lakini ndio mila zetu, wengine si wana keketa mpaka leo
 
Kuna vitu itakua wanavimalizia,ambavyo jamii nyingine haitakiwi kuona.
 
Ni kweli, mamchifu na wafalme hua wanazikwa na watu hai... sidhani kama hizo mila bado zipo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…