Mazingaombwe ni ujuzi gani?

Mazingaombwe ni ujuzi gani?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
649
Reaction score
975
Wiki mbili zilizopita kuna Kijana (Jina kapuni).
Alipigwa 100k.

Kwenye mchezo huo kulikuwa na kete tatu moja ilikuwa na picha na ziingine mbili hazikuwa na picha, Sasa Bwana si dogo alijichanganya alipigwa za uso. Cha kushangaza ukiwa mpenzi mtazamaji unaona kabisa ile pale yenye picha ila ukijitosa utaimba HALLELUJAH.

Tuacheni na hilo tukio katika maisha yangu mpaka sasa nimeshuhudia Mazingaombwe mbalimbali.

Mwana-mazingaombwe kutafuna wembe na kutoa sindano mdomoni, Mwana-mazingaombwe kugeuza karatasi kuwa biscuits, Kuna ile ya kuvuta pikipiki kwa shingo (Sina hakika kama zile ni nguvu za wahusika au ni Mazingaombwe), Kuna nyingine iliyonishangaza pia Mwana-mazingaombwe alisimama kama mita tatu kutoka kwa Kijana aliyebeba ndizi ila cha ajabu Mwana-mazingaombwe akiwa ameshikilia kisu aliweza kukata ndizi kwa distance hiyo.

Ningependa tujadili hii WanaJamiiForums.
Je, Hii ni elimu gani? Inafikirisha.

Kiranga , Infropreneur
 
Mazingaombwe yapo hata mimi niliwahi kuyashuhudia.

Binafsi sielewi ni namna gani wanayafanya.

Lakini mazingaombwe si uchawi.

Mazingaombwe ni maarifa ya kibinadamu ambayo wengi hatuelewi yanafanyikaje.

Wana mazingaombwe wenyewe wana maarifa haya na kama wapo humu ningependa watupe hiyo elimu na haya maarifa.
 
Mazingaumbwe live haina tofauti sana na online casino games, tofauti ni Moja imezubaa nyingine imechangamka.


Aina hii ya michezo kaa nayo mita 1000.
Acha kabisa sijui dogo alipumbazwa.
Maana alipigwa 100k ndani ya dkk 3.

Ukiwa mtazamaji unaona kabisa ileee pale haina picha, Jichanganye sasa za uso😩😂😂
 
Back
Top Bottom