mwekwa ntandu
JF-Expert Member
- Aug 24, 2019
- 1,040
- 2,428
Wakati niko shule ya msingi Nyakabungo mwanza alikuja mwana mazingaombwe mmoja,kwa macho yangu nilishuhudia mfuko mtupu ambao ulikung'utwa na nilijiridhisha haukuwa na kitu chochote ndani jamaa yule aliuwekea makaratasi tupu ambayo niliyachana kutoka kwenye daftari langu ambalo nilikuwa sijaliandikia chochote na mara baada ya kumwaga chini makarasi yale zilitoka blue blue tupu yaani noti za elfu kumi elfu kumi maana kipindi kile zilikuwa za blue.Mpaka leo huwa najiuliza maswali kama kaweza kufanya uchawi wa kugeuza karatasi kuwa pesa ameshindwa nini kutoa nyingi za kutosha ili azitumie mwenyewe na badala yake alituchangisha wanafunzi shiling hamsini hamsini za kutazama onesho lake!!???
Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app