SoC04 Mazingira katika nyanja ya mito na udhibiti wa nishati zisizofaa kwa kupikia kama mkaa na kuni

SoC04 Mazingira katika nyanja ya mito na udhibiti wa nishati zisizofaa kwa kupikia kama mkaa na kuni

Tanzania Tuitakayo competition threads

swaumu mohamedi

New Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
3
Reaction score
2
MAZINGIRA
Tanzania yetu, Fahari yetu, mazingira yetu daima tutayatunza, Tanzania ndo nchi pekee yenye mazingira ya kuvutia na yenye nuru na mwangaza, hivyo basi ni jukumu la kila mwananchi kuweza kuyalinda na kuyatunza mazingira hayo, mito ni moja ya rasilimali yenye umuhimu zaidi tunapotunza mazingira yetu, maana mito inachukua takribani 99% ya ustawi wa Maisha ya binadamu na ustawi wa nchi kiujumla

Screenshot_20240622-192750.png


Hii ni picha inayoonesha mto Mara uliyoko Musoma nchini Tanzania

MABADILIKO YATAKAYOPELEKEA UMUHIMU WA MITO NCHINI TANZANIA

Mito izungushiwe uzio au ukuta ili kuzuia kusambaa kwa maji, Maji yatokanayo na mito huwezesha huzalishaji wa mazao katika sekta ya kilimo,endapo itawekwa mkakati mzuri wa utuzwaji wake kama vile mahala mito inapopatikana pajengwa uzio au ukuta utakaozuia kusambaa kwa maji katika maeneo mbalimbali na maji kuweza kukusanyika sehemu moja hii itasaidia wadau wanaohusika katika sekta ya kilimo kuweza kubuni mbinu mbalimbali za kilimo pasipo shaka ya uhaba wa maji pia itawezesha kuwepo kwa kilimo cha umwagiliaji wa mazao mbalimbali katika nchi yetu ambapo itapelekea ukuaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Pia kujengwa kwa mifumo bora ya maji taka ili kudhibiti mmonyoko wa maji yanayotiririka kwenya mito , itapelekea kupungua kwa uhaba wa maji kwa matumizi ya binadamu, hasahasa maeneo ambayo kuna uhaba wa vyanzo vya maji, kupitia hivyo itasaidia upatikanaji wa maji kiurahisi pia kuwepo na utunzwaji wa maji kwa muda mrefu hata kama kutatokea kipind cha ukame watu watakuwa na uwezekano wa kupata maji kwa matumizi mbalimbali ya kila siku kwa kufanya hivyo itapunguza adha ya ukosefu wa maji pia kupitia kutunza maji itasaidia wananchi waweze kuchota maji yaliyo safi na salama kwa matumizi kuliko maji yaliyosambaa hiyo pia itasaidia watu waweze kuepuka magonjwa mbalimbali kama vile kichocho ,kuharisha n.k pia hiyo itasaidia hata kwa vijiji ambavyo havina maji kuweza kupata maji kwa urahisi.

Pia kutokana na mapendekezo yalizotolewa na shirika la chakula( FAO) ni kuwa mito ndo chanzo kikubwa kinachotegemewa na mamillion ya watu nchini na duniani kwa ujumla kwa upatikanaji wa Samaki na maji safi na kusisitiza kuwa inapaswa kulindwa vyema zaidi ili kulinda mchango inayotoa kwa lishe ya binadamu na Uchumi wan chi kiujumla
Screenshot_20240622-195531_1.jpg


Hapo chini ni picha ya nipashe mwanga wa jamii inayoonesha baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mbori, Willaya ya Mpwapwa,iliyoko mkoani Dodoma wakichota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani huku wengine wakiyakanyaga wakati wakivuka kitendo ambacho ni hatari kwa afya ya watumiaji

Pia serikali ikaweka sera nzuri ya kuweza kupanda mimea kandokando ya mito, itasaidia kuzalisha umeme, mfano mto Rufiji uliyopo nchini Tanzania, kuwepo kwa uzio au ukuta kwa ubora wa hali ya juu kama vile mimea katika mito mbalimbali huwezesha kuzalisha nishati ya umeme kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania, miaka kadhaa iliyopita kumekuwa na janga la upungufu wa nishati ya umeme nchini Tanzania kulingana na ukosefu wa vyanzo vya kuzalisha umeme ikiwemo maji yatokanayo na mito hivyo basi tukitunza mito yetu itatuwezesha kuweka akiba ya uwepo wa maji yanayotumika kuzalisha umeme kwa miaka na miaka na kwa vizazi hadi vizazi, ukiangalia kwa upande wa ongozeko la pato la nchi linategemea zaidi nishati ya umeme maana shughuli nyingi zinategemea uendeshwaji wake kwa kutumia nishati hiyo ya umeme

NISHATI YA KUPIKIA YA GESI ASILIA
Tanzania ndo nchi pekee gesi asilia inapopatikana ila uzalishaji wake ni hafifu embapo husababisha kuwepo kwa nishati ambazo si staili kwa Maisha ya binadamu kama kuni, mkaa n.k gesi asilia ni nishati safi na yenye ufanisi ambapo inaweza kutumika kama nishati ya kupikia , pia ni njia salama na ya kirafiki kwa mazingira kuliko matumizi ya nishati nyingine zote na hii gesi mara nyingi huundwa kutokana na mabaki ya viumbehai vinavyooteaa chini ya ardhi

MABADILIKO YANAYOTAKIWA KUTEKELEZWA NA WIZARA KATIKA SEKTA YA NISHATI YA KUPIKIA YA GESI ASILIA

Wizara husika inatakiwa kuweka mkakati mzuri wa uchimbaji wa visima virefu mahala ambapo hii nishati inapatikana, inavyosemekana gesi asilia hupatikani chini ya ardhi hinyo basi bisima vinapochimbwa vinasaidia kuweka kama alama maeneo ambayo yako na hizo gesi ili baadae iweze kurahisisha kazi katika uchimbaji wa gesi hivyo hata kama ikipita miaka kadhaa pasiwe na shaka ya upatikanaji wa gesi hiyo.

Pia wizara inatakiwa kuweka au kuwekeza technolojia ya kisasa katika uchimbaji na uzalishaji wa gesi hiyo, hapa inatakiwa wawepo wataalamu watakaowezesha uchimbaji wa mafuta ya gesi hiyo walio na ujuzi wa hali ya juu kuhusu namna ya kuchimba hiyo gesi katika miaka zijazo.

Pi serikali iwekeze zaidi kununua bomba na pampu za kunyonya gesi asilia iliyko ardhini, pampu na bomba hizo zitasaidia kuondoa gesi hizo kutoka kwenye visima vilivyochimbwa chini ya ardhi
Screenshot_20240623-065858_1.jpg


UMUHIMU WA GESI ASILIA
Gesi asilia hupelekea kupungua kwa uchafuzi wa mazingira kwa kukata miti hivyo kwa ajili ya kuni au mkaa katika nchi na itasaidia kila mwananchi aweze kupata njia mbadala ya kupikia tofauti na njia zisizostahili

Pia gesi asilia husaidia kuwepo na mpangilio mzuri wa mvua , hii hutokana pale watu watakapoacha kukata miti hivyo inaweza kupelekea mvua kutokea kwa wingi na kusaidia katika sekta nyingize kama vila kilimo na n.k kwa kufanya hivyo Tanzania yetu itahama kutoka katika Uchumi wa mwisho na Kwenda uchumi wa kati
 

Attachments

  • IMG_20240622_223555.jpg
    IMG_20240622_223555.jpg
    61.2 KB · Views: 2
  • IMG_20240622_195613.jpg
    IMG_20240622_195613.jpg
    75.7 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240622-192750.png
    Screenshot_20240622-192750.png
    399 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240622-195535.png
    Screenshot_20240622-195535.png
    608.6 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240622-195531_1.jpg
    Screenshot_20240622-195531_1.jpg
    230.2 KB · Views: 2
Upvote 5
Back
Top Bottom