DOKEZO Mazingira ya Soko la Samaki na Dagaa katika Mwalo la Mswahili - Mwanza siyo rafiki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257

Wafanyabishara Soko la Samaki na Dagaa katika Mwalo la Mswahili hapa jijini Mwanza wameendelea kufanya shughuli zetu katika mazingira yasiyo rafiki.

Soko hill lipo kando ya Ziwa Victoria ambapo shughuli zote zinafanywa pembezoni mwa ziwa hilo kama kuosha samaki, hali hiyo inaweza kuwa mbaya kiafya kwa kuwa maji ya kandokando ya Ziwa yanaweza kuwa na uchafu lakini pia kupitia kuosha uchafu unaongezeka eneo husika.

Jambo lingine ni kuwa mazingira hayo ya uchafu yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya milipuko kwani sehemu kubwa ya soko ina maji ambayo si alama.

Kutokana na hicho kinachoendelea kumekuwa na harufu kali, kingine kinachokera ni maeneo hayo hakuna sehemu ya kuhifadhia takataka, mifereji nayo haridhishi hata huduma ya vyoo sio nzuri.

Inakuwaje sehemu ya kuuzia chakula kama hiyo kutowekwa safi au kuzingatiwa ubora, Bwana Afya yuko wapi na wenzake?


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…