Juma jaibu kuhanga
New Member
- May 18, 2024
- 4
- 5
Utunzaji wa mazingira ni muhimu katika maendeleo ya taifa ili kufikia Tanzania tuitakayo ni vyema serikali,jamii na wadau kusimama kidete katika kupinga uharubifu wa mazingira kwa kufanya mambo yafutayo.
Je jamii inajua kama suala la kulinda na kutunza mazingira ni jukumu lao au la serikali pekee? Katika jamii ya leo bado raia wanaona suala la mazingira sio lao kabisa hii inatokokea kwa sababu ya kutokuwepo kwa ushirikishaji wa jamii moja kwa moja katika hatua zinazofaa ili kulinda mazingira kutokana na jiografia ya jamii husika licha uwepo wa kampeni mbalimbali za kitaifa za utunzaji wa mazingira bila kujali jiografia ya jamii.
Serikali haina budi kuanzisha sera na kampeni ya kuivesha jamii jukumu la utanzaji mazingira bila kujali hali na changamoto yeyote ile za kiitikadi na mwelekeo katika utekelezaji wake wa upingaji wa uhalibifu wa mazingira uwepo wa mazingira sahihi na tulivu yanasaidia chachu ya maendeleo na kuvutia wawekezaji na kupambana na magonjwa ya mripuko ambayo kwa kiasi kikubwa yanatokea kwa sababu ya uchafu na utunzaji hafifu wa mazingira katika jamii. Hivyo basi jamii ijuzwe juu ya jukumu la utunzaji wa mazingira ni la jamii husika sio tu la serikali.
Kila kata wawekwe maafisa mazingira.Suala la utunzajia wa mazingira kuwaachia watendaji na wenyeviti inapelekea kutotoa elimu ya kutosha kwa jamii kutokana na kutokuwa na maarifa zaidi juu ya elimu ya mazingira. Tanzania ili ipige hatua katika kuboresha mazingira wataalam wa mazingira wasambae nchi nzima ili kuweza kutoa semina elekezi na shamba darasa ili kuboresha mazingira kwa wakati stahiki.
Serikali iandae mpango wa kudumu na endelevu katika suala nzima la kuweka maafisa wa mazingira ili waweze kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kukabiliana na uchafuzi wa mazingira hususani maeneo ya mjini. Pia hao maafisa wa mazingira wapewe jukumu la kutembelea nyumba za wananchi na kuona jinsi maendeleo yao ya utunzaji wa mazingira binafsi yanavyoendelea.
Pia suala la kutoa elimu kabla ya athari kubwa kutokea.Katika jamii yetu ya leo maeneo mengi hupatiwa elimu baada ya athari kutokea mfano kipindupindu n.k.
Jamii ijuzwe suala la kutunza mazingira ni la mda wote bila kujali hali yeyote katika jamii.kama walivyosema wahenga tahadhari kabla ya hatari. Suala la jamii kuwekwa wazi juu ya athari ya uchafuzi wa mazingira linavyoathiri uchumi na jamii bila mficho litasaidia wananchi wengi kujikita katika tahadhari ambayo ni kulinda mazingira kwa chachu zaidi ili kukwepa mikono ya hatari na matokeo hasi ya uharibifu wa mazingira.
Vilevile kuanzishwe kwa utaratibu wa kutoa zawadi kwa kata zinazofanya vizuri katika utunzaji wa mazingira kwa kila tarafa angalau kwa kila baada ya miezi miwili. Hii itasaidia kijenga chachu kuanzia viongozi hadi wananchi katika kuboresha na kubuni mbinu mbalimbali za utunzaji wa mazingira kwa kuhofia orodha ya kata zinazofanya vizuri katika kutunza mazingira itapotoka, Hii itasaidia kujenga tabia mazoea ya kukemea uharibifu wa mazingira kwa kuhofia aibu ya kuwa wa mwisho.
Kutoa vibali maalumu katika kipindi cha kusafisha mashamba ambacho kitambatana na ukaguzi kabda ya kuanza zoezi la uchomaji moto ambayo ni njia inayotumiwa na wananchi wengi,Huu uchomaji olela unapelekea kuchoma hadi misiti iliyokaribu na mashamba hayo na kupelekea hatari ya ukame na kupoteza miti mingi bila sababu ya msingi.
Hivyo basi suala la vibali litasaidia usalama wa misitu na viumbe vyake katika nchi ya Tanzania. Hivyo basi utoaji wa vibali hivyo lazima uendane na ukaguzi madhubuti wa mashamba hayo kabla ya uchomaji. Hii itasaidia usalama wa mazingira bila kuathari mazingira mengine.
Kuweka kwa vibao na mabango ya ILANI juu ya katazo la utupaji wa taka ovyo kila mahali sio tu maneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu kam vile stendi za mabasi,mashuleni.jamii haina budi kujua suala la utanzaji wa mazigira ni kila mahali bila kujali macho ya watazamaji.suala la mabango litasaidia kuwakumbusha wananchi juu ya uwepo wa sera na katazo la uchafuzi mazingira kila mahali bila kujali hali yeyote hile inayoikumba jamii husika.
Kutunga sera inayoelekeza hatua stahiki zinazotakiwa kuchukuliwa na kuwekwa wazi kwa jamii kutumia vyombo ya habari na mitandao ya jamii kwa kuandaa makala na semina za wazi ili wananchi waweze kupata elimu juu ya utunzaji wa mazingira ambato itasaidia upatikanaji wa maarifa na ujuzi kwa jamii kwa haraka zaidi na itapelekea kudumu wa maarifa hayo.
Wizara zinazohusika na mazingara ziandaa filamu zinazoeleza utunzaji wa mazingara kwa kutumia wasanii maarufu nchi na kuwashawishi kuweka vionjo vya utunzaji wa mazingira katika filamu zao ili kuweza kufikiksha ujumbe kwa jamii kwa kuwa jamii ya sasa inawafuatilia sana wasanii kwa kina zaidi kuliko hata hutuba za viongozi
Mwisho, suala la utunzaji wa mazingira ni vyema likaanza kwa kufuatilia mienendo ya mtu mmoja mmoja na kufutaia kitaifa ili kujenga.

Upvote
0