Mazishi/ misa ya Ivani live spark tv

mkuu ww unaelewa eeh!! yaani nasikia nyo nyo nyo nyingi? naona mvua imeanza kuwazingua
naelewa sana tu ug ni almost nyumbani. luganda hii lugha mgumu kiliko "kinyankole" wale wa (western akina m7.)
Akisema mwebale nyo nyo nyo dala anamaanisha asante asante sana
 
naelewa sana tu ug ni almost nyumbani. luganda hii lugha mgumu kiliko "kinyankole" wale wa (western akina m7.)
Akisenye mwebale nyo nyo nyo dala anamaanisha asante asante sana
huyu uncle wa marehemu anaonekana mtata sana sijui alikuwa anasoma nini hapo
 
Mungu alitoa na ametwaa jina lake kihimidiwe milele yeye ndiye anayejua sababu ya mavuno yake.Niseme watu wajue kwamba pesa na dhahabu ni Mali ya bwana.Elewa ukipewa pesa in mpango Wa Mungu kwako na ujue unapimwa.Hakika kitendo cha waombolezaji maarufu kwenye msiba Wa Ivan huko Uganda kutupwa pesa kaburini ambazo hatima yake ni kuoza ili hali wamezungukwa na watu masikini ni ishara mbaya kwa Ivan na kwa jamii Nzima na kwa dunia pia.sifahamu imani zao lakini hawafungamani na Mungu na ikiwa pesa ni karama Mungu atawajibu sawasawa na walivyotenda.ufahari sawa kama ndivyo Mungu anapenda na ikiwa ni kwa maagizo yake vinginevyo ni shida watubu.
 
Huyo mtoto wa nne sio huyo jamaa anajiita King Lawrence sijui nani mkuu!?
mmh king lawrence mbona ni mtu mzima mwenzie.....ni rafiki yake na umri hautofautiani sana.
 
Pesa sabuni ya roho yaani wakuu wamesimamisha shughuli kumzika tajiri, R.I.P ukiwa kapuku watu wanauliza kuna msiba wa nani?! wanaendelea kucheza bao kibarazani wala hawana muda na wewe.
Duh!! Aivani kamfunika daimondi vibaya saaana!!!
 
Kwa jins maisha yalivyo magumu hapa tz hela alizozikwa nazo Ivan the don zingechukua mda gan kaburin?
 
mmh king lawrence mbona ni mtu mzima mwenzie.....ni rafiki yake na umri hautofautiani sana.
Oooh..basi sawa. Maana alivyokuwa anadeka kwa Marehemu nilifikiri ndio first born wake kwa mama mwingine mkuu. Asante kwa kunielewesha.
 
Kwa jins maisha yalivyo magumu hapa tz hela alizozikwa nazo Ivan the don zingechukua mda gan kaburin?

Ni kumkufuru Mungu na kuukufuru ubinadamu kumzika mtu na fedha wakati katika jamii inayozunguka hilo kaburi kuna yatima, walemavu, wajane, wazee wasiojiweza, nk ambao hawana/hawapati mahitaji muhimu ya kibinadamu!!!
 
Hakika Mungu atuhurumie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…