Mazishi ya Global Publishers...

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Ongezeko la kasi ya utumiaji wa mitandao ya kijamii inaweza kuwa Great depression kwa kaka manager wa kampuni ya GPL bwana Eric james Shigongo.

Tofauti na miaka iliyopita ambapo magazeti yake (ijumaa,risasi,uwazi,ijumaa wikienda na risasi mchanganyiko) yalikuwa ndo habari ya mujini kwa kuongoza kwa kusomwa na watu wengi zaidi Tanzania, ivi sasa mambo yameenda ndivyo sivyo baada ya mitandao ya kijamii kama instagram, Jamii forum, Facebook na mengineyo kuongoza kwa kutumiwa na wananchi wengi zaidi. baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa tishio kubwa sio tu kwa mastaa na mashabiki wao, unaambiwa hadi waandishi wa habari wamekuwa wadogo kwa kasi ya hali ya juu na ya ajabu iliyoanzishwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo kwa kutoa habari nyeti kuhusu baadhi ya mastaa apa bongo.

Ni ukweli usiopingika magazeti ya shigongo yamebaki kuwa sehemu ya kuuzia sura wasanii na sio kwa habari moto kama ilivyokuwa apo awali.
ujio wa kasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii unamnyima usingizi mfanyabiashara huyu, sio tu kibiashara hata kwa maisha yake binafsi.
Kwa kuonyesha udhaifu wao wa kufulia ki habari , waandishi wa magazeti ya GPL wamekuwa wakihangaika kwenye mitandao ya kijamii kutafuta habari za kuandika magazetini , kitu ambacho kimepunguza msisimko wa habari.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo wamekuwa wakiandika scandal chafu na nyeti kuhusu mastaa mbali mbali.
Ujio huo wa wa kasi ya watu wa kwenye mitandao ya kijamii wanaosemekana kuwa ni watu wa karibu na baadhi ya mastaa , umewakosesha raha baadhi ya waandishi.
 
Bora yafe yaani siyapendi hatari...

Suala la social networks sio siri linaua mno soko la magazeti na vyombo vya utangszaji kwa ujumla na kwa nchi zilizoendelea hali ndo inatisha zaidi...

unaenda kununua mwananchi unakutana na habari uliyoisoma jf unaghairi kununua....
 
Ah sio sredi hiii banaaaaaaa
Binamu vipi!
 
Fungua thread ya Ukweli Warumi Tuchane, hii haijakaa inavyostahili, au ushachukua chako Mkuu?
Wizi wa huyu tunaujua, kuanzia copy and paste mpaka wa Movies kuzifanya kuwa story, lete uzi wa maana.
 
Eti unanunua gazeti kusoma nani kafumaniwa,sijui diamond kafanya sijui nin na nin,nashangaa sana hasa kama ni mtu mzima!

Magazeti gani hukuti matangazo ya ajira,matokeo ya mitihani ya form 4 au 6,hata taarifa kwa umma zitolewazo na govt,hakuna.
 
We badirisha style yako ya uandishi !
Hakuna anaetaka kusoma wall of text!

Ndomaana kuna aya!!

Sent !
 
Haya magazet pendwa ni ------- sana, nanasgaka na taaluma zao, hopeless
 
Hivi magazeti yote ya udaku bongo ni yake tu?
 
Magazeti hayawezi kufa. Kuna tofauti ukisoma kitu kwenye mtandao na ukisoma kwenye gazeti.

Ukiwa na gazeti unasoma vizuri sababu kuna habari nyingi tofauti. Ata wakija wageni unawapa wasome.

Pia ukiboreka unasoma habari muda wote. Biashara ya magazeti inazidi kukua kamwe haiwezi kufa.
 
Uingereza wameanza kujua mambo ya mitandao kabla mleta mada hajaja mjini, lakini gazeti la udaku la The Sun linachapishwa zaidi ya nakala milioni 2 kwa siku. Halafu haujui tu, wanaume wanaponda magazeti haya lakini wake zao ndiyo wanayasoma, waulizeni kuna nini, huenda kuna kitu wanakipata. Otherwise alipofikia Shigongo siyo pa kusema magazeti yake yatakufa, huyu ni kijana mwenzetu amefanikiwa, na sisi tubuni miradi yetu tusonge, tuache wivu wa kike!
 
Fact!


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hizi ni takwimu za wapi? ni lini hayo magazeti yanayopendwa na watu wenye ulemavu wa akili yaliwahi kuongoza kwa mauzo?
 


Chanzo cha takwimu zako? Usikimbilie kuropoka bila kuelewa unazungumza nini, Shigongo hawezi kucompete na mitandao ya kijamii na hata unapozungumzia zama hizo wakati internet bado haijawa popular kama sasa, ni vitu visivyo na uwiano kwa sababu zama hizo computer zenyewe hazikuwa zimesambaa kama sasa na pia sasa vifaa vya kuaccess internet vimekuwa vingi na vinavyoweza kumfikia mtu yeyote popote tofauti na zama hizo hivyo taarifaa inasambaa haraka kupitia mitandao kuliko magazeti, take it or leave it lakini ndio ukweli.
Angalia mmiliki wa facebook, mbona ni bilionea, kama magazeti yanalipa, Shigongo angekuwa ni bilionea in dolars pia, lakini Zuckernburg amewazidi utajiri hata wenye kumiliki hayo magazeti unayoyasema kwa sababu uhitaji wa taarifa za mtandao ni mkubwa kuliko hayo magazeti ya udaku.
Muwe mnakaa kimya wakati mwingine.
 
Mh..ngoja nikapitie financial statements za hao GPL kwa kipindi cha miaka 10 nione trend ipo vipi then nitakuja kuchangia
 

iv we unalipwa. na jf? swali 2
 
Me nahisi mleta mada ana bifu tu Shigongo. Hamna evidence yoyote ndani ya hiyo mada haswa ukiangalia mazingira ya Tanzania watumiaji ws internet bado ni wachache sana.

Otherwise mimi magazeti ya udaku siyapendi kabisa maana hayana chochote cha kujifunza zaidi ya kuharibu. Ni mbaya zaidi pale ninapoona wanaume wazima wakifuatilia udaku kwenye hayo magazeti.

Namshauri tu shigongo atoe vitu ambavyo vitajenga maadili ya mtanzania badala ya kuzidi kubomoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…