Tumefika salama. Kumshindikiza mzee wetu
=======
Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Masauni, amesema Rais amehuzunishwa sana na tukio hili, na kutoa wito kwa mtu yeyote kuacha kushutumu, badala yake kama mtu ana kielelezo aweze kukiwasilisha.
"Wanafamilia wajue Serikali ipo pamoja na nyie, na hakuna namna ya kuharakisha utoaji haki"
Pia, alitoa pole na rambirambi kwa familia ya mwathiriwa, akihimiza maombi kwa mwathiriwa.
Pia, soma=> Tafrani yazuka msibani Tanga: Waombolezaji wakataa dua ya Waziri Masauni wakimtaka ajiuzulu
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ameeleza kuwa Kibao alikuwa kiongozi mashuhuri na mtaalamu mahiri, aliyeshirikiana nao katika mikakati ya chama kabla ya safari yake kwenda Dar es Salaam.
Mnyika alilaumu Idara ya Usalama wa Taifa kwa kuhusika katika tukio lililosababisha kifo hicho, na akaunga mkono wito wa uwajibikaji, akisisitiza kuwa haki iliyo bora ni kusema ukweli mbele ya watawala dhalimu.