kasimba123
JF-Expert Member
- Apr 18, 2010
- 1,753
- 816
Pamoja na yote ila ni fundisho kubwa sana kwa sisi tulobaki.....mtu akipata mafanikio anakaa mbali sana na familia kiasi cha kuwa anamilikiwa na jamii zaidi ya familia yake (sikatai kupendwa na watu wanaokuzunguka hata kushirikiana nao) ila haya ya kamati ya mazishi ya style hii ni indicator ya modern culture kutawala sana maisha kiasi cha kukosa hata uamuzi wa kifamilia kwenye mambo ya maana, makubwa na mazito it be a sad or happy moment.
Mytake; Kwa yaliyotokea yawezekana kuwa hata yeye marehemu alikuwa anawachukulia wazazi wake "poa" mbele ya marafiki zake ndo maana hiyo kamati ilikuwa na nguvu to that extent.......tumeona misiba mingi ya watu wa caliber tofauti tofauti oftenly last say hutoka kwa wazazi au familia husika, wengine mnakuwepo kutoa ushauri na kuhakikisha mipango ya familia inaenda sawa. In other words tunapopata mafanikio kwa umakini tupiganie sana umoja na ustawi wa familia zetu ili iwe kimbilio wakati wa maisha, ugonjwa na umauti na kamwe hatutokaa tujute.....we shud never leave our parents and families exposed, spineless and with an egg shell status.....we shud always avoid these at any cost
Ushauri: Kama umeamua kuishi hiyo modern culture then weka will mapema kama wafanyavyo hao walioianzisha ili kuja kupunguza mivutano kama hii otherwise tegemea familia yako kuyumba sana sana pindi utakapo oa, zaa, ugua au aga dunia
Ni maoni tuuu
mkuu inawezekana ni matumizi mabaya ya hela,pia msimba mkubwa kama ule nadhani pia matumizi yatakuwa mengi...ila kama kweli kuna hujuma imefanyika basi ubinadam kazi
wanabodi hiyo source ni ya kuaminika ee..naona hakuna aliyehoji chanzo!![/QUOTEGAZETI LA SAYARI MKUU!
naskia milion 30 zilitumika kununulia suti nyeusi za tukio..
hahahaaa, unamaanisha nini mkuu?Nilivyo sikia tu Ruge yupo kwenye kamati nilitegemea hayo lazima ya tokee
Wengi mtakuwa mmefatilia kwa karibu yote yaliyotokea katika kifo cha Msanii Steven Kanumba. Baada ya kifo hiki watu mbalimbali wakiwemo wabunge wamezidi kupaza sauti zao kutaka kifanyike kitu ili kazi za wasanii zisiimbiwe. Hii ndio iliyonipelekea kuandika hili ili kuona changamoto hii tutaikabili namna gani.
Wote tulishuhudia Clouds FM radio na TV zikirusha na kutangaza live matukio yote ya kifo cha Kanumba. Ila sina uhakika kama Familia ya Marehemu Kanumba ilitoa idhini ya chombo hicho cha habari kufanya hivyo walivyofanya. Na kama walipata ni kiasi gani familia imelipwa kwa ajili hiyo. Na kama hawajafanya yote hayo (Kupata ruhusa na kuliilipa familia) basi wamefanya WIZI mkubwa.
Hakuna atakayebisha kwamba Chombo hicho cha habari kimejinufaisha sana na msiba ule kwa njia mbali mbali. Kwanza watu wengi kukijua kuwa kipo, watu wengi kununua starTY ili tu wanase Clouds TV na kushuhudia matukio ya msiba wa Kanumba na pili kuwanyima haki wanafamilia kuja kutoa DVD za coverage yote ya musiba wa Kanumba na kupiga pesa kidogo kwa ajili ya maisha.
Wote wanajua wenzetu walivyofaidika kwa kuuza rights za matangazo. Mfano kifo cha Michael Jackson, Whitney Huston na hata mjuu kuu wa mandela aliyetaka kuuza rights za kurusha kifo cha Mandela kabla hata hajafa.
TUTAMALIZAJE WIZI HUU WA VYOMBO VYA HABARI KAMA CLOUDS RADIO AND TV. Nipo tayari kufungua kesi ya madai kwa niaba ya familia ya Kanumba ili Clouds Walipe maana wamefaidika.[/QUOTE
Waliokula hela za msiba watapata matatizo makubwa sana,mi yangu macho mi kinachonishangaza walishatangaza kuwa mtu asiye mwanachama wao hawataenda ilikuaje tena kuwa mpaka kwn kamati? wewe JB na wenzako mmeshalaanika mtabakia kununua vigari vitagongwa mtabaki km mlivyo. maneno ya watu ni mabaya sn nyie hata kwa siri rudisheni,hata haya hamna looooh! usuper star wa njaa tu nyie ndio mngeongoza kwa kutoa michango mikubwa kinyume chake nyie ndio mnaiba mtapukutika km ***** mi nipo hapa!
Mbona hawakurusha moja kwa moja msiba wa mzee kipara.....clouds wezi sana....wanafata kwenye maslahi tu..!!! Kwanza matangazo ya tv live hawawezi.....ili boa kishenzy siku ile...!!!
Ni kawaida ya watu waOVU kupenda kuvaa mamiwani makubwa myeusi kuficha Sura zao huku dhamira zikiwasuta. Walikuwa wapigaji hawa.KAMATI YA MAZISHI YA KANUMBA NA KASHFA YA KUCHAKACHUA MICHANGO
Hawa wenye suti na miwani myeusi ndio baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wanaodaiwa kufanya upigaji huo wa fedha za michango ya msiba
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka ndani ya familia ya Kanumba, kamati hiyo imedaiwa kufanya uchakachuaji wa michango hiyo inayokadiriwa kuwa mamilioni ya fedha, achilia mbali
vitu kadhaa, yakiwemo magunia 32 ya mchele. Chanzo hicho kimeidokeza Sayari kuwa, dalili za hali hiyo zilianza kujitokeza mapema kabisa pale mwanandugu mmoja alipoenguliwa kwenye kamati hiyo, kwa kile kinachoelezwa, kamati hiyo kufanya jukumu hilo kwa uhuru zaidi.Dalili nyingine, ni kitendo cha wajumbe wa Kamati hiyo kutoweka baada ya mazishi hadi walipofika nyumbani kwa marehemu Alhamisi usiku.Kwamba, pamoja na mambo mengine, kwenye kikao kilichofanyika siku hiyo kati ya wanandugu na kamati hiyo, Mama Kanumba amezuia kuzungumzia suala la michango. "Mama Kanumba ametakiwa asiseme lolote kwa Waandishi wa Habari kuhusu michango&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; kaelezwa kama atafanya hivyo, huenda asipate kitu kabisa," alisema ndugu huyo. Kwa mujibu wa chanzo hicho, Kamati hiyo imetoa onyo hilo kwa vile tangu kwisha kwa maziko ya Kanumba, wamekuwa wakipata usumbufu wa simu watu kuulizia kilichokusanywa na kilichobaki.Chanzo hicho kimedokeza kuwa, baada ya kamati hiyo kukutana na wanafamilia kwa mara ya kwanza baada ya ukimya mrefu, ilisema michango yote ni sh mil 51.Kati ya fedha hizo, gharama za mazishi ni shilingi mil 48 huku kukiwa na deni la sh mil 2 za ukarabati wa barabara Leaders kutokana na uharibifu uliofanywa na waombolezaji.Chanzo hicho kimedokeza kuwa, walipohoji fedha zilizochangwa kupitia M-pesa kupitia namba ambayo ilitangazwa, walielezwa ilipatikana sh 20,000 tu.Kilisema, kiasi hicho ni kiduchu mno kwa sababu mashabiki wa Kanumba wa Mwanza pekee, walichanga sh 300,000.Kilidokeza kuwa, pia kulikuwa na gunia 32 za mchele zilitotolewa na msamaria, hazijulikani zilipokwenda. "Licha ya kutolewa gunia 32 za mchele, hazijulikani zipo wapi&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];. fikiria hata mfiwa, anakosa hata gunia moja la kwenda kuanzia maisha mapya bila mwanaye," kilidokeza chanzo hicho. Kilipoulizwa kwanini hawakuweka ndugu kwenye kamati hiyo tangu mapema, kilisema alikuwemo, lakini akaenguliwakwa kwa zengwe.Uratibu wa msiba huo ulikuwa chini ya Kamati iliyokuwa chini ya Gabriel Mtitu na wajumbe kama Ray, Cloud, Steve Nyerere, Hapines Magese, Mtitu William, Jacob Steven na wengineo.Sayari ilipomtafuta Mtitu kwa njia ya simu jana, alisema kutokana na usumbufu ambao wanaupata kwa wengi kutaka kujua juu ya michango hiyo ya msiba, Kamati yake imeamua kukutana na waandishi wa Habari kesho Jumanne kuweka kila kitu bayana."Kuna mengi yanasema hadharani na chini ya zuria kuhusu rambirambi, kwa lengo la kuweka bayana kila kitu, tumepanga kukutana na waandishi wa Habari Jumanne (kesho) kuanzia majira ya saa nne," alisema Mtitu. CHANZO:GAZETI LA SAYARI