The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Misa ya Mazishi ya Baba Mtakatifu Francisko itafanyika Jumamosi ijayo, tarehe 26 Aprili 2025, mbele ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, kama ilivyoelezwa katika ‘Ordo Exsequiarum Romani Pontificis.’
Hayo yametangazwa na Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa, tarehe 22 Aprili, huku ikiripoti kwamba ibada ya mazishi itaongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali.
Ibada ya mwisho “Ultima commendatio na la Valedictio.”Kisha jeneza la Papa litapelekwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na kutoka hapo hadi kwenye Kanisa la Mtakatifu Maria Mkuu kwa maziko.
Viongozi kadhaa wa nchi na serikali wametangaza ushiriki wao.
Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alizozana mara kwa mara na papa kuhusu uhamiaji, alisema yeye na mkewe watasafiri kwa ndege hadi Roma kwa ajili ya ibada hiyo.
Miongoni mwa wakuu wengine wa nchi wanaotarajiwa kuhudhuria ni Javier Milei, rais wa Argentina asilia ya Francis, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, kulingana na chanzo katika ofisi yake.