Mazishi ya Rais wa Falme za Kiarabu

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za weekend wadau,
Mapambano yaendelee hata kama mama anaupiga mwingi.

Jana zilitoka taarifa za kifo cha aliyekuwa raisi wa falme za kiarabu (U.A.E) Sheikh Khalifa bin zayed Al Nahyan baada ya kuugua kwa muda mrefu huku nafasi yake ikichukuliwa na mdogo wake.
Wadau kuna vya kujifunza hapa kwa mtu mkubwa kama yule na cheo alichokuwa nacho ila wamewahi kumzika bila kumchelewesha na wala kaburi lake halijajengewa.

Angalia picha za mazishi yake na kaburi lake hapa chini kwa kweli kuna la kujifunza hapa kumuweka marehemu kwa muda mrefu ni kumtesa na kukaribisha roho ya mauti na mambo yasiyofaa katika jamii.

NB: ni taarifa tu mijadala na mambo yasiyofaa hairuhusiwi kwenye mada hii.
 
Taratibu za mazishi ni suala la kitamaduni, kila tamaduni zina mifumo yao tofauti na jamii nyingine. Hata sisi waafrika ondoa tamaduni za hao waliotuletea dini na sisi kwa umaandazi wetu tumeacha ile mifumo ya makabila na koo zetu tunaiga koo za waarabu na wazungu. Mazishi hayakufikishi/ kutokufikisha mbinguni kama uliishi kwa matendo mema wewe ni wa.mbinguni tuu bila kujali umezikwa kichwa kinaangalia wapi au uliliwa na mamba. Kama ulikuwa ni mmoja wa wauaji kama wale waliomchoma moto binti wa watu huko Nigeria wewe ni wa motoni tuu bila kujali umezikwa vipi
 
Mda ukifika asicheleweshwe
Apumzike tu
Kwani mtu aliyekufa huwa anasema amechoka apumizishwe haraka.?

Nadhani hizi ni tamaduni za jamii husika.

Kuna makabila mtu akifa wanamzika baada ya muda wanaenda kufukua mifupa na kuiweka majumbani mwao.

Hao nao vipi marehemu alisema wamfukue kachoka kukaa kaburini?

Tumia akili.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawanaga mbwembwe sijui kupga sakafu ndani sijui na tiles. Unakufa unazikwa habari zinaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…