Unapotaka kutoa ELIMU muhimu, anza kwanza na QURAN kisha kazia kwa kutumia HADITHI na ukizingatia maneno ya MTUME MUHAMMAD S.A.W.
Haya amekufundisha nani ? Mtume alipewa Qur'aan na Hadithi, sasa unapoweka sharti kwamba lazima uanze na Qur'aan, ni ishara kwamba Uislamu huujui.
Unatakiwa ujifunze mambl mengi sana kuhusu Uislamu, kwanza huu unadishi wa "S.A.W" u aonyesha wazi kabisa huujui Uiaslamu.
Sio umesoma Juzuu moja unajikuta ushakuwa Ustadhi.
Ukikosolewa unatakiwa ukubali kosa, kuendelea kuminyana na watu ambao maisha yetu tumeyatoa kwa ajili ya kujifunza hii DINI (Uislamu) unajichoresha na mwisho wake utaangukia pua.
Sasa nakuelimisha hapa, haijakatazwa kujengea, inashauriwa usijengee ili ipatikane nafasi ya wenzako kuzikwa hapo hapo. Ikumbukwe kaburi moja laweza chukua watu 40.
Nionyeshe wapi Mtume ameruhusu makaburi kujengewa ? Kijana hii ni dini usilete maoni yako binafsi au habari za masheikh wako, dini "Amesema Allah au Amesema Mtume", sasa nimekuwekea Hadithi unaikataa, umeisoma hiyo Hadithi ?
Pia zingatia hivyo Vibao ambayo wanaweka kwenye hayo makaburi ni ishara ya kutambua kuwa hili ni kaburi la fulani. Je hapo ikotokea mtu mwingine inatakiwa azikwe hapo watazika wakati nyie mshaweka alama yenu na jina la marehemu?
Hiyo ndiyo inayotakiwa na nimeielezea hapo juu, kwamba ni alama kwa ajili ya kumtambua ndugu yako na zamani walikuwa wanaweka mawe. Hata hizi habari za kuandika jina la maiti, tarehe ya kuzaliwa na aliyi kufa, hili pia halifai.
Suala la kuzikwa huwa linakuja baada ya kupita kitambo. Ndiyo maana ikawa haramu kujengea makuburi kwa namna yoyote ile.
Aina hii ya Waislam ndio wanafanya Uislam uonekane hauna maana.
Aina yako wewe ndiyo inafanya mafundisho sahihi ya Uislamu yasifanyiwe kazi na hili ni jambo baya sana.
Unatakiwa kijana ukitengeneze kiti chako kwanza kabla ya kuking'arisha.
Ukija kuendelea kujadiliana na mimi nataka uniwekee vitu vifuatavyo :
1. Qur'aan
2. Hadithi
3. Kauli za Maswahaba
4. Kauli za Wanazuoni
Usiniletee stori za vijiweni na maoni ya wat wajinga wasi usoma Uislamu na kuleta ujuaji kama wewe.
Shukrani.