Mazishi ya Rais wa Falme za Kiarabu

Kujengea sio DHAMBI, ila inashauriwa yasijengewe ili kuweza kupata eneo la kuzika watu wengine.

Usipoteshe watu na usitengeze nafasi ya kuwaona waislam wenzako wamekosea bali toa elimu watu waelewe.
Hizi habari umezipata wapi ? Kujengea ni dhambi na ukifanya hivyo ni madhambi kinachotakiwa kufanywa ni kuweka alama ambayo ndugu au jamaa akienda muda wowote anajua ndugu yao alizikwa wapi.

Na nukuu :

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kaburi kutiwa chokaa (liwe imara), kuketiwa juu yake na kujengewa. [Muslim]

Kutokana na Hadithi hii, swahaba Ali bin Abi Twalib kipindi cha utawala alipata habari kuna sehemu watu wanajengea makaburi, akatuma mtu au watu na kuwaamuru wakikuta kaburi lolote limeinuka kwa kujengewa basi wavunje hichi kilichojengwa.

Sasa unaposema inafaa kujengewa unatumia mafundisho ya nani katika Uislamu ?
 
Kwenye masuala ya Dini tumia lugha laini ili uweze mshawishi mtu akubaliane na Dini yako. Usimkejeli, Dhihaki, wala kuonesha kuwa yeye ni muongofu sana. Mlinganie kwa utaratibu, ujue wengi wetu tunachukia UISLAM kwa kusikia au kufuata mkumbo.
 
Sema ndio hivyo kwasababu ni mtu mkubwa bila shaka amefanyiwa vipimo vyote na kuhakikisha amekufa kweli

Ila huku kimtaa mtaa ukazimia masaa matano usitingishike utajikuta chafya imekubana ukiwa ndani ya kaburi
Watu wana welimu juu ya haya mambo, sisi wengine tumefundishwa namna ya kumjua mtu amekufa, ndiyo maana sheria ikapita.

Wanazuoni wetu wanakufa saa kumi na mbili jioni saa mbili usiku amezikwa, mara nyingi huzikwa usiku.
 
Unapotaka kutoa ELIMU muhimu, anza kwanza na QURAN kisha kazia kwa kutumia HADITHI na ukizingatia maneno ya MTUME MUHAMMAD S.A.W.

Sio umesoma Juzuu moja unajikuta ushakuwa Ustadhi.

Sasa nakuelimisha hapa, haijakatazwa kujengea, inashauriwa usijengee ili ipatikane nafasi ya wenzako kuzikwa hapo hapo. Ikumbukwe kaburi moja laweza chukua watu 40.

Pia zingatia hivyo Vibao ambayo wanaweka kwenye hayo makaburi ni ishara ya kutambua kuwa hili ni kaburi la fulani. Je hapo ikotokea mtu mwingine inatakiwa azikwe hapo watazika wakati nyie mshaweka alama yenu na jina la marehemu?

Aina hii ya Waislam ndio wanafanya Uislam uonekane hauna maana.

Zingatia DHAMBI ni suala ambalo hata ALLAH S.W amelikataza. Mambo mengine yaliyofanywa na mtu ni SUNNA na unaweza kufanya au kuacha.
Weka Aya hapa kwamba imekatazwa.
 
Hapo ndipo Mungu anasema kila kitu chako kitabakia isipokuwa matendo yako uliyofanya
 
Kwenye masuala ya Dini tumia lugha laini ili uweze mshawishi mtu akubaliane na Dini yako. Usimkejeli, Dhihaki, wala kuonesha kuwa yeye ni muongofu sana. Mlinganie kwa utaratibu, ujue wengi wetu tunachukia UISLAM kwa kusikia au kufuata mkumbo.
Angetulia mambwa kama hayo kuyatukana tu hayana staha lijinga kabisa kulet ujuaji

Ndo maaana yanauliwa kwa dhihaka
 
Taratibu za mazishi ya kiafrica ni zipi
 
Unapotaka kutoa ELIMU muhimu, anza kwanza na QURAN kisha kazia kwa kutumia HADITHI na ukizingatia maneno ya MTUME MUHAMMAD S.A.W.
Haya amekufundisha nani ? Mtume alipewa Qur'aan na Hadithi, sasa unapoweka sharti kwamba lazima uanze na Qur'aan, ni ishara kwamba Uislamu huujui.

Unatakiwa ujifunze mambl mengi sana kuhusu Uislamu, kwanza huu unadishi wa "S.A.W" u aonyesha wazi kabisa huujui Uiaslamu.

Sio umesoma Juzuu moja unajikuta ushakuwa Ustadhi.
Ukikosolewa unatakiwa ukubali kosa, kuendelea kuminyana na watu ambao maisha yetu tumeyatoa kwa ajili ya kujifunza hii DINI (Uislamu) unajichoresha na mwisho wake utaangukia pua.
Sasa nakuelimisha hapa, haijakatazwa kujengea, inashauriwa usijengee ili ipatikane nafasi ya wenzako kuzikwa hapo hapo. Ikumbukwe kaburi moja laweza chukua watu 40.
Nionyeshe wapi Mtume ameruhusu makaburi kujengewa ? Kijana hii ni dini usilete maoni yako binafsi au habari za masheikh wako, dini "Amesema Allah au Amesema Mtume", sasa nimekuwekea Hadithi unaikataa, umeisoma hiyo Hadithi ?
Pia zingatia hivyo Vibao ambayo wanaweka kwenye hayo makaburi ni ishara ya kutambua kuwa hili ni kaburi la fulani. Je hapo ikotokea mtu mwingine inatakiwa azikwe hapo watazika wakati nyie mshaweka alama yenu na jina la marehemu?
Hiyo ndiyo inayotakiwa na nimeielezea hapo juu, kwamba ni alama kwa ajili ya kumtambua ndugu yako na zamani walikuwa wanaweka mawe. Hata hizi habari za kuandika jina la maiti, tarehe ya kuzaliwa na aliyi kufa, hili pia halifai.

Suala la kuzikwa huwa linakuja baada ya kupita kitambo. Ndiyo maana ikawa haramu kujengea makuburi kwa namna yoyote ile.
Aina hii ya Waislam ndio wanafanya Uislam uonekane hauna maana.
Aina yako wewe ndiyo inafanya mafundisho sahihi ya Uislamu yasifanyiwe kazi na hili ni jambo baya sana.

Unatakiwa kijana ukitengeneze kiti chako kwanza kabla ya kuking'arisha.

Ukija kuendelea kujadiliana na mimi nataka uniwekee vitu vifuatavyo :

1. Qur'aan
2. Hadithi
3. Kauli za Maswahaba
4. Kauli za Wanazuoni

Usiniletee stori za vijiweni na maoni ya wat wajinga wasi usoma Uislamu na kuleta ujuaji kama wewe.

Shukrani.
 
Mzee wewe ni Ustadhi ubwabwa, pamoja na elimu dunia ila hii ya Dini sidhani kama unaweza nifikia hata nusu yake.
Unaingia google unaokota hadithi unaweka.

Kuna Hadithi za aina mbili mzee.

Au wewe ukiambiwa Hadithi basi unaokota tu.

IQRA (SOMA) narudi SOMA, NENDA KASOME kisha njoo hapa na hoja zako za kitoto.

Weka hapa UHARAMU WA KUJENGEA KABURI kama kweli una uelewa na Dini yako. Maana kila katazo kina msingi wake. Haya tuambie hapa msingi wa UHARAMU WA KUJENGEA KABURI UKO KWENYE NINI??
 
Mzee umetisha hapa hata mimi nilikua sijui. Ila umenifundisha..kongole mkuu!
 
Swali zuri sana

♦️Mungubalivyoumba wanadamu kila jamii aliipendelea kwa vitu tofauti

♦️Waafrika wote, tulinyimwa maandishi isipokuwa Ethiopia lakini, waarabu, wahindi, wachina, wayahudi walipewa herufi za maandishi ya asili

♦️ Sisi waafrika tofauti na waarabu tulipewa Lugha nyingi sana , kila kabila na Lugha yake , hivyo na mfumo wake tofauti wa mila na mazishj

♦️Lakini waarabu wana lugha moja kuu, mila za aina moja kuu, maandishi yao ya asili, ndio maana wana mfumo mmoja wa mazishi

♦️Ukitaka kujua jirani zao wsyahudi nao wana mfumo tofauti kabisa wa mazishi na sio huo wa kiarabu. Fuatilia hata mazishi ya Yesu mnaojidanganya kuwa alikuwa Muislam ujue mazishi na kaburi lake lilikuwaje , ni tofauti na wazungu wazikavyo, ni tofauti na waarabu na ni tofauti na waafrica
 
Binafsi huwa siafiki ujenzi wa kaburi kulijengea, watu wote tukijengea kaburi ni kumaliza nafasi. Unless labda ule ujenzi kama wa wazungu..ila huu wa kikawaida unakula nafasi na kuwanyima wengine nafasi ya kuzika.
 
Yule Mzee mbabaishaji walimtembeza nchi nzima hadi akawaozea

Pale uwanjani wakati wa Kuaga, kuna familia ilipoteza wapendwa wao 4 sababu ya kukanyagana pasipo sababu, eti kisa kuaga Maiti .

Mambo ya ajabu sana,unatoka huko kwako mzuka kibao eti unawahi kuaga maiti ,matokeo yake na wewe unakuwa maiti.
 
Binafsi huwa siafiki ujenzi wa kaburi kulijengea, watu wote tukijengea kaburi ni kumaliza nafasi. Unless labda ule ujenzi kama wa wazungu..ila huu wa kikawaida unakula nafasi na kuwanyima wengine nafasi ya kuzika.

Hili suala ilitakiwa Mamlaka za miji ipige marufuku ,kuna maeneo siku hizi ukihudhuria mazishi unakuta wamejenga na vijumba makaburini, Mambo ya hovyo sana.
 
Hili suala ilitakiwa Mamlaka za miji ipige marufuku ,kuna maeneo siku hizi ukihudhuria mazishi unakuta wamejenga na vijumba makaburini, Mambo ya hovyo sana.
Kabisa mkuu. Mimi napinga kabisa..na hili ni kwa watu wa imani zote. Maana hata waislam japo wanasema kujengea ni dhambi, lakini ukienda makaburi yao unakuta wamezungushia kaburi. Mi naona si sawa, inanyima nafasi wengine kuzika.
 
Nimecheka sana. Kijana nikikwambia sisi haya ndiyo maisha tuliyo yachagua unatakiwa uelewe nini namaanisha.

Mtume akikataza jambo ujue kulifanya kwake ni makosa na ukifanya unapata dhambi, sababu unakuwa umemuasi Allah.

Unaposema Hadithi ziko aina mbili, ukaishia hapo unaonekana elimu ya hadithi huijui, ulitakiwa umalizie kwa kuzingatia nini ? Je kwa kuzingatia riwaya au nini ? Bado unaendelea kuonyesha ujinga ulio nao kwenye dini.

Nimeshakuwekea Hadithi inayo onyesha uharamu wa Hadithi, sasa wewe weka hata hadithi dhaifu inayo onyesha kuwa inafaa kujengea kaburi.

Msingi wa katazo upo katika utiifu, kutumia mali vibaya na hupelekea watu kuabudu makaburi.

Sasa naona unanipigisha stori kijana, huna hoja unanipotezea muda.
 
Hao ni waarab, masuala ama taratibu zao hazituhusu.....hata hapa Afrika, kila nchi ina taratibu zake katika kuzika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…