Vidonda vya tumbo ni tatizo linalosumbua watu wengi. Husababisha maumivu makali sana, kiasi cha kufanya liwe tatizo lisilovumilika kirahisi.
Katika kutafuta tiba, baadhi ya watu hutumia dawa za hospitalini, huku baadhi wakitumia dawa za asili.
Pia, maziwa ni miongoni mwa dawa zinazo zungumzwa sana. Ni kweli kuwa maziwa hutibu tatizo la vidonda vya tumbo?
Katika kutafuta tiba, baadhi ya watu hutumia dawa za hospitalini, huku baadhi wakitumia dawa za asili.
Pia, maziwa ni miongoni mwa dawa zinazo zungumzwa sana. Ni kweli kuwa maziwa hutibu tatizo la vidonda vya tumbo?
- Tunachokijua
- Vidonda vya tumbo ni michubuko inayotokea kwenye kuta za mfumo wa chakula, hasa kwenye sehemu ya tumbo au pia sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo.
Ukubwa wa vidonda hivi hutofautiana, kuanzia millimita chache hadi sentimita kadhaa.
Dalili za ugonjwa huu mara nyingi hutegemea umri pamoja na eneo husika vilipo vidonda hivi. Miongoni mwake ni -
- Maumivu makali ya kuvuta kwa misuli, au kuwaka moto kwa misuli ya tumbo
- Tumbo kujaa gesi mara kwa mara
- Kiungulia
- Kichefuchefu
- Kujisaidia choo chenye damu, au choo cheusi
- Kutapika uchafu wenye damu, au wenye rangi ya weusi
- Kupata maumivu kifuani, kama moto unaochoma
Matibabu
Matumizi ya dawa za antibayotiki hufaa wakati huu, pia dawa za kudhibiti uzalishwaji wa asidi nyingi hupaswa kumezwa.
Ikiwa changamoto hii itaendelea kujirudia, pia ikiwa changamoto zinazosababishwa na ugonjwa huu kama vile kuziba kwa utumbo au kuvuja kwa damu tumboni zitatokea, upasuaji huwa ni chaguo sahihi.
Matumizi ya Maziwa kama tiba
Baadhi ya watu hudhani kuwa maziwa fresh husaidia kutibu tatizo hili. Madai haya hayana ukweli.
Maziwa huleta ahueni ya muda mfupi kwa kutengeneza utando juu ya kuta za vidonda. Aidha, aina hii ya maziwa huongeza uzalishwaji wa asidi tumboni pamoja na vimeng’enya vingine ambavyo baada ya kuisha kwa utando wa maziwa husababisha maumivu makali zaidi pamoja na kuongeza ukubwa wa tatizo.
Uthibitisho mwingine unatolewa pia na tovuti maarufu ya Afya, WebMD inayotoa maelezo kuwa maziwa yanaweza kuongeza ukubwa wa tatizo kwa kuzalisha asidi nyingi zaidi.
Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa Mtu mwenye vidonda vya tumbo hashauriwi kutumia maziwa fresh kwa kuwa hayana uwezo wa kutibu na kufuta uwepo wa tatizo hili.