Mkuu Chokochoko, nadhani utakuwa na tatizo tunaloliita "Lactose Intolerance"
Lactose Intolerance, ni kushindwa kwa mwili kuvumilia aina ya sukari inayoitwa Lactose, na hii hutokana na kukosekana kwa enzyme inayoitwa Lactase...Tatizo hili hutokana na
1. Kurithi: Kuzaliwa ukiwa na tatizo hili(ukosefu wa enzyme hii ya lactase)..mtu aliyezaliwana tatizo
hugundua/hugunduliwa mapema, hasa wakati wa utoto pale chakula pekee ni maziwa.
2. Magonjwa katika utumbo: Magonjwa yanoharibu sehemu chakula kinapofyonzwa(absorption villi) mfano Celiac sprue
nk..
3. Upungufu wa Lactase enzyme: Lactase ezyme(inayobadilisha sukari ya Lactose) hupungua kikawaida toka utotoni na
kubaki katika kiwango kidogo ukubwani na hii tunaiita (Adult type hypolactasia).
DALILI;
Mara nyingi dalili za tatizo hili huwa ni tumbo kujaa gesi, tumbo kuuma,kutoa hewa chafu, na wakati mwingine kuharisha mara baada ya mtu mwenye tatizo kutumia maziwa au vyakula vyenye maziwa!
MATIBABU/TIBA;
Lactose Intolerance hutibika kwa kujua chanzo/kiini chake ni kipi kama ambavyo nimeeleza hapo juu..yaani
1. EPUKA kutumia maziwa au vyakula vyenye maziwa mfano(Icecream, milkshakes,n.k)...
2. Iwapo ni ugonjwa katika utumbo, tiba kulingana na ugonjwa huo itatolewa.
3. Kutumia vyakula vingine vyenye kuwa na madini ya calcium, mfano(MAZIWA MGANDO/YOGURT, samaki, mboga za
majani kama vile spinach)...Hii ni kwa sababu maziwa ni chanzo kikubwa cha Vitamin D,na madini ya calcium ambayo
husaidia kuimarisha mifupa na meno...hivyo upungufu wa madini haya huweza kusababisha, mifupa kuvunjika kwa
urahisi kuliko kawaida.
MAZIWA YA MGANDO;
Haya unaweza kutumia na hayana shida yeyote hii ni kutokana kuwa maziwa yanapochachuliwa(fermented) huwa na aina ya HARMLESS bacteria(probiotics) ambao wao wenyewe wana enzyme ya lactase hivyo kusaidia katika kuibadilisha sukari ya lactose.