Maziwa/Nazi hupunguza kiungulia kwenye maharage

Maziwa/Nazi hupunguza kiungulia kwenye maharage

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Katika makala iliyopita Nilifundisha namna ya kupoa asidi iletayo kiungulia kwenye maharage,na tuliona kwamba huwezi kutoa asidi(phytic)yote kwenye maharage ila unaweza kuipunguza kwa kiasi kikubwa ili kuepusha kiungulia.Kwa mantiki hiyo basi,bado kuna kiasi kidogo cha asidi kinachobaki,kuna watu wachache ambao hata kiasi hicho kidogo cha asidi hutosha kuwapa kiungulia.
Kuna namna ya kukata Asidi kidogo inayobaki kwenye maharage baada ya kuyaloweka,unaeweza ongeza maziwa au nazi.

Ili kuelewa kwanini maziwa na nazi vinakata asidi iliyopo kwenye maharage,nilazima utambue kwamba maziwa na nazi ni BUFFERs(kiingere)buffer ni mchanganyiko wenye asidi na base kwa pamoja. niwarudishe secondary,enzi zile ukiwa kidato cha pili ulijifunza kuhusu acid and base.Naamini mwalimu wako alikwambia base inauwezo wa ku neutrolise acids.Hicho ndicho kinachotokea unapoweka maziwa kwenye maharage,base iliyo kwenye maziwa inakata/ neutrolise ile phytic acid iliyo kwenye maharage.

Mahitaji
Maharage yaliyochemshwa yakaiva
mafuta ya kula
vitunguu maji
Nyanya
vitunguu swaumu
chumvi
Maziwa
Njia
1.Chemsha maharage adi yaive nay awe laini,hakikisha maji yamekauka kabisa kwenye maharage kabla hujaepua jikoni.Maharage yakiiva na kulainika hupasuka yenyewe


  • Usiweke chumvi unapochemsha maharage,chumvi hufanya maharage yawe magumu
2.Katika sufuria,unga kitunguu na nyanya kama kawaida,ila unapoweka nyanya weka na kitunguu swaumu.kaanga adi viive na mafuta na nyanya vitengane ndani ya sufuria.

  • Kawaida mafuta huja juu na nyanya hubaki chini.
3.Ongeza maharage na chumvi kwenye nyanya iliyoiva ,geuza na kaanga kwa muda ili nyanya na maharage viungane na kua kitu kimoja.


4.Ongeza maziwa fresh,kisha koroga ili kuchanganya.weka maziwa yakutosha ili kupata mchuzi wakutosha.maharage hupendeza zaidi yakiwa na mchuzi.Watoto wengi wanapenda mchuzi wa mahage na si maharage yenyewe.



  • Unaweza weka maji na maziwa ,katika hili,tanguliza maji yakishachemka ndipo uweke maziwa na uchemshe zaidi.
5.Wakati maziwa yanachemka,koroga kila mara ili kuhakikisha maharage hayaungui kwa chini.chemsha adi pale utakapoona maziwa yameiva na mchuzi umekua mzito.katika moto wa wastani,isizidi dakika sita.yakiwa tayari epua jikoni,tayari kwa kula.


Maelezo ya ziada
Kama unaamua kutumia nazi,upishi ni kama huu nilioelezea,ila tu pale nilipoatumia maziwa unaweza tumia nazi.
Unapochemsha na kuivisha maharage ,Hakikisha mchuzi au maji yote yamekauka kwenye maharage ,ili kutunza ladha na utamu wa maharage.wengi mnapenda kuacha mchuzi ili muutumie wakati wa kuunga maharage.Unapoongeza mchuzi huo baada ya kuunga,unapunguza nguvu ya maziwa au nazi,na zaidi ya hapo ubaharibu utamu au ladha ya maharage kwani maziwa na nazi huleta ladha nzuri kwenye maharage.
Maharage ni chakula kizuri sana na kitamu,ila kiungulia,gesi tumboni na upishi mbaya unachangia sana watu wengi kutokula maharage,au kutokuyapenda.

Langu mmoja tu,kukufumbua macho,na kama kawaida utendaji ni juu yako.Ipe familia yako maharage bora sio bora maharage.
 
Nimekuwa nikikwepa kuunga Maharage kwa Nazi kwa Miaka kadhaa sasa kwa kuepuka Kiungulia! Tulikuwa tunaishia kuunga na Mafuta,basi! Nitajaribu kufwata Maelekezo yako na hatimae kukupa Mrejesho!..
 
Asante sana mkuu MziziMkavu, kwa muda mrefu katika familia yetu nyumbani tumekuwa tukitumia sukari ili kupunguza acid katika maharage.

Tukipika maharage hatuweku chumvi bali tunaweka sukari, hakika acid yote huisha na hakuna anayelalamika kuumwa tumbo wala kiungulia make kuna wagonjwa wa ulcers nyumbani. Na mimi ni mmojawapo na shahidi kwa hili
 
Last edited by a moderator:
Mie maharage lazma niyaroeke over night alafu nkiyapika naweka tangawizi na saumu basi kishwa habar yake hupati kiungulia wala gesi ila mie napendelea kuweka nazi
 
Aisee maharagwe ni balaa, nahisi nina immunity kubwa na hii mboga. Sijaacha kuyamiss, pamoja na kula takribani six years katika shule za bweni za serikali, bado ninayapenda hata sasa katika ukubwa wangu. Haipiti siku tatu sijala hii mboga.

Mzizi mkavu umeongeza kitu, nadhani baada ya njia hii ya kupunguza gesi naweza kula kila siku sasa.
 
Aisee maharagwe ni balaa, nahisi nina immunity kubwa na hii mboga. Sijaacha kuyamiss, pamoja na kula takribani six years katika shule za bweni za serikali, bado ninayapenda hata sasa katika ukubwa wangu. Haipiti siku tatu sijala hii mboga.

Mzizi mkavu umeongeza kitu, nadhani baada ya njia hii ya kupunguza gesi naweza kula kila siku sasa.

Naona hujanishinda mimi mkuu. Napenda maharage balaa.
 
nimependa sana hiingoja nikapike na mimi...asante sana kaka MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
mkuu, leo nimeperuzi kuhusu hii mboga sasa nishapata mapishi kama matano. wacha niliunge:flame:
 
Hii kitu lazima niitest ndani ya wiki hii.
Nalog off

Yani ukijaribu huu upishi utataka ule maharage kila sikuu....hapa me nimetoka kuyapika tena jana tuu na leo nayamalizia kiporo....yani hata hayaleti gesi tumboni...

Thanx MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Ooh kumbe ndio maana nikila Maharage ambayo hayana nazi napata kiungulia sana
 
Back
Top Bottom