Mwanamke asipo mnyonyesha mtoto kwa zaidi ya siku moja maziwa yake huchacha na kuharibika.
Wanawake hushauriwa kumwachisha mtoto ziwa ili asidhurike kwa sababu maziwa hayo hukosa tena sifa ya kutumiwa na mtoto.
Ukweli upoje?
Ukweli upoje?
- Tunachokijua
- Maziwa ya matiti ya binadamu ni maziwa yanayotolewa na mama ili kumnyonyesha mwanawe. Maziwa hayo hutoa chanzo msingi cha lishe kwa watoto kabla ya wao kupata uwezo wa kula vyakula vingine, yaani watoto wachanga hadi umri kadiri wanavyoweza kuendelea kunyonyeshwa.
Maziwa ya mama huchacha?
Suala la Maziwa ya Mama kuchacha au kuharibika yakiwa Kifuani ni Imani potofu ndani ya Jamii, ni jambo ambalo halina ukweli kwasababu Maziwa hayachachi yakiwa ndani ya Mwili hata asiponyonyesha.
Endapo Mama ameajiriwa anashauriwa kufanya maandalizi mapema ya kukamua Maziwa na kuyagandisha kwenye Jokofu/Friji ili aweze kuyatumia kumlisha Mtoto pale likizo ya Uzazi inapomaliza.
Maziwa ya mama yaliyokamuliwa huweza kukaa na kuwa salama kwa lishe ya mtoto ndani ya miezi 6 kama yamegadishwa na siku 4 kama yamehifadhiwa kwenye jokofu bila kuganda, pia hukaa masaa 8 bila kuwekwa kwenye jokofu.
Hivyo, kwa sababu yoyote ile, mtoto hapaswi kuachishwa maziwa haya kwa kuwa hubeba virutubisho muhimu vinavyofaa kwa ukuaji bora wa afya ya mwili na akili.