64Bits
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 961
- 564
Habari zenu wote, wakubwa shkamooni. Hii ni mara yangu ya kwanza kuanzisha uzi humu ndani, na nimelazimika kufanya hivyo kwa tatizo linalonikabili.
Mwenyezi Mungu kanijaalia mtoto wiki moja iliyopita. Tatizo ni kwamba maziwa yangu yanatoka kidogo sana na sio mazito kwa hiyo mtoto hashibi.
Nimejaribu kumpa formula milk ila anayakataa. Nimefuata ushauri wa watu kadhaa na nikajaribu kula mtori, uji wa pilipili manga, supu nk lakini wapi.
Nimenunua breast pump ila hata niki pump yanatoka kidogo sana. Kuna anayejua chakula cha kula kitakachosaidia naomba aniambie.
Natanguliza shukrani za dhati
=============================================================================================

hongera kwa baby mamie!
fanya hiv
-relax to the maximum,stress na kunyonyesha haviendi
-kunywa maziwa mengi
-kunywa supu ya nyanya chungu chemsha zenywe tuu
-endelea kumpa dogo avute tu.usiache
-kila ukimka na kimsingi fanya mara nying tu uwezavyo,fanyia matiti yako massage kwa kitambaa/taulo lililochovywa kweny maji ya moto
-endelea kunywa huo uji wa pilipili manga,supu nyingi,ndizi
-wachana na uoga wa kunenepa,ukimaliza kulea mwanao utafanya tu diets kuna maclean 9 kibao!na mazoezi
Enjoy being a mother!
kisses kwa toto!
duh, nilikuwa nimeandika mengi, sijui yameenda wapi.
Kama unatumia dawa inaweza kuwa sababu, diclofenac ni hatari kwa maziwa, yanakausha kabisa waweza jikuta unatoa nido
Hapa sasa funga kibwebwe, kama una maziwa kidogo, kula kunaweza saidia, utakuwa shapeless kwa muda lakini ni wajibu wako kadogoo ashibe.
Baadhi ya vyakula vya kutumia
Uji wa pilipili manga
mbegu za maboga
legumes
soup ya nyama/samaki
veg soup
mtori
soup ya maboga
Chai ya rangi ya motooo
uji wa mchele aka bokoboko
Penda kujazia msosi walau nusu saa kabla ya kunyonyesha.
Afu usiache msosi wa kawaida pia.
Ila week ya kwanza huwaga majanga sometimes.
Hongera sana.