Maziwa ya mtoto yanatoka machache, naombeni ushauri

Maziwa ya mtoto yanatoka machache, naombeni ushauri

64Bits

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
961
Reaction score
564
Habari zenu wote, wakubwa shkamooni. Hii ni mara yangu ya kwanza kuanzisha uzi humu ndani, na nimelazimika kufanya hivyo kwa tatizo linalonikabili.

Mwenyezi Mungu kanijaalia mtoto wiki moja iliyopita. Tatizo ni kwamba maziwa yangu yanatoka kidogo sana na sio mazito kwa hiyo mtoto hashibi.

Nimejaribu kumpa formula milk ila anayakataa. Nimefuata ushauri wa watu kadhaa na nikajaribu kula mtori, uji wa pilipili manga, supu nk lakini wapi.

Nimenunua breast pump ila hata niki pump yanatoka kidogo sana. Kuna anayejua chakula cha kula kitakachosaidia naomba aniambie.

Natanguliza shukrani za dhati
=============================================================================================
hongera kwa baby mamie!
fanya hiv
-relax to the maximum,stress na kunyonyesha haviendi
-kunywa maziwa mengi
-kunywa supu ya nyanya chungu chemsha zenywe tuu
-endelea kumpa dogo avute tu.usiache
-kila ukimka na kimsingi fanya mara nying tu uwezavyo,fanyia matiti yako massage kwa kitambaa/taulo lililochovywa kweny maji ya moto
-endelea kunywa huo uji wa pilipili manga,supu nyingi,ndizi
-wachana na uoga wa kunenepa,ukimaliza kulea mwanao utafanya tu diets kuna maclean 9 kibao!na mazoezi
Enjoy being a mother!
kisses kwa toto!

duh, nilikuwa nimeandika mengi, sijui yameenda wapi.

Kama unatumia dawa inaweza kuwa sababu, diclofenac ni hatari kwa maziwa, yanakausha kabisa waweza jikuta unatoa nido

Hapa sasa funga kibwebwe, kama una maziwa kidogo, kula kunaweza saidia, utakuwa shapeless kwa muda lakini ni wajibu wako kadogoo ashibe.

Baadhi ya vyakula vya kutumia
Uji wa pilipili manga
mbegu za maboga
legumes
soup ya nyama/samaki
veg soup
mtori
soup ya maboga
Chai ya rangi ya motooo
uji wa mchele aka bokoboko

Penda kujazia msosi walau nusu saa kabla ya kunyonyesha.

Afu usiache msosi wa kawaida pia.

Ila week ya kwanza huwaga majanga sometimes.

Hongera sana.
 
Jaribu tu mie nilikaa wiki mbili ndio yakaanza kutoka nilikuwa nampa maziwa ya kopo kipindi hicho ila hali ikizidi rudi hosp
 
Kunywa uji wa ulezi pia...ymikishindikana rudi hsptl
 
Fuata ushauri hapo juu,engine huchukua mpaka wiki mbili na uwe unamyonyesha kila saa ndio production inaongezeka .Ni hatari kuanza kumpa maziwa ya kopo kwani utakuwa hanyonyi na halo itazidi kuwa mbaya na hata maandalizi yake kwa afya ya mtoto SI vizuri
 
endelea tu kumnyonyesha anavyonyonya ndo yanapata motisha ya kujizalisha,kandamiza mauji namtori,maziwa yatakuja mpaka utakuwa unayakamua na mengine unahifadhi kwenye friza.endelea tu kumpa formula pia,ila umpropose nyonyo mara kwa mara
 
hongera kwa baby mamie!
fanya hiv
-relax to the maximum,stress na kunyonyesha haviendi
-kunywa maziwa mengi
-kunywa supu ya nyanya chungu chemsha zenywe tuu
-endelea kumpa dogo avute tu.usiache
-kila ukimka na kimsingi fanya mara nying tu uwezavyo,fanyia matiti yako massage kwa kitambaa/taulo lililochovywa kweny maji ya moto
-endelea kunywa huo uji wa pilipili manga,supu nyingi,ndizi
-wachana na uoga wa kunenepa,ukimaliza kulea mwanao utafanya tu diets kuna maclean 9 kibao!na mazoezi
Enjoy being a mother!
kisses kwa toto!
 
duh, nilikuwa nimeandika mengi, sijui yameenda wapi.

Kama unatumia dawa inaweza kuwa sababu, diclofenac ni hatari kwa maziwa, yanakausha kabisa waweza jikuta unatoa nido

Hapa sasa funga kibwebwe, kama una maziwa kidogo, kula kunaweza saidia, utakuwa shapeless kwa muda lakini ni wajibu wako kadogoo ashibe.

Baadhi ya vyakula vya kutumia
Uji wa pilipili manga
mbegu za maboga
legumes
soup ya nyama/samaki
veg soup
mtori
soup ya maboga
Chai ya rangi ya motooo
uji wa mchele aka bokoboko

Penda kujazia msosi walau nusu saa kabla ya kunyonyesha.

Afu usiache msosi wa kawaida pia.

Ila week ya kwanza huwaga majanga sometimes.

Hongera sana.
 
Tafuta mbegu za maboga, saga, tia kwenye juice au uji! Utatoa maziwa balaa! Ni recipie ya wa Mexico/Mehico! Ukinyunyiza pilipili manga baridaaaaa!
 
Tafuta mbegu za maboga, saga, tia kwenye juice au uji! Utatoa maziwa balaa! Ni recipie ya wa Mexico/Mehico! Ukinyunyiza pilipili manga baridaaaaa!

mmmmmmmmmh uko nje ya game ushauri wenye experience tu unazingatiwa lol
 
Back
Top Bottom