Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NAIBU WAZIRI SILINDE - MAZIWA YASIYO SALAMA NI HATARI KWA MLAJI
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde ameonya kuwa matumizi ya maziwa yasiyo salama huhatarisha maisha ya mlaji kutokana na kutumika kama njia ya kusafirisha magonjwa ya mifugo kwenda binadamu.
Mhe. Silinde amesema hayo kwenye sherehe za ufunguzi wa Maadhimisho ya kitaifa ya Wiki ya unywaji maziwa duniani iliyofanyika Mei 30, 2023 kwenye viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora.
“Mwaka huu maadhimisho haya ya Wiki ya unywaji Maziwa kitaifa tumeyaelekeza kwenye kusisitiza matumizi ya maziwa salama kwa sababu kumekuwepo na magonjwa mengi sana yanayosababishwa na maziwa yasiyo salama, mfano ugonjwa wa kutupa mimba ambapo mtu akinywa maziwa yanayotokana na ng’ombe anayeumwa ugonjwa huo naye huanza kuathiriwa na tatizo hilo hapo hapo” Ameongeza Mhe. Silinde.
Mhe. Slinde amewataka Wananchi wote waliopo karibu na mkoa wa Tabora kufika kwenye maonesho hayo ili wapate elimu ya kutosha kuhusu sheria namba 8 ya maziwa ambayo inaanisha kila kitu kuhusu maziwa salama.