Michael mbano
JF-Expert Member
- Apr 4, 2022
- 820
- 570
Kuna wakati mtu unapatwa na hasira unaenda ofisi fulan unamkuta mhudumu anaongea na cmu tena umbea au stori tu halafu hakati kukusikiliza.Heri kama anaongea na bosi napo akimaliza anapaswa aseme samahani utaratibu mwingine uendelee.Ajabu mtu anayeleta dharau ukute anaelimu ndogo kuliko wewe alipata kazi kimichongo tu.Kweli ofisi ingekuwa yako ungefanya hivi?Mjirekebishe.Tume ya utumishi wa uma na maadili fanyeni kazi.Hizi ofisi za Serikali siku hizi mambo yamerudi vile vile kama zamani sikuwahi kuombwa rushwa leo nimeombwa rushwa watumishi wanafanya kazi utafikiri za baba zao.
Kweli mtu nimetuma barua toka mwezi wa tatu kila ukienda haijajibiwa kumbe kuna mtu kaweka barua pembeni kisa anataka rushwa sasa si angeniambia kipindi kile kile ningekuwa nishampa hiyo rushwa.
NB: Watumishi tufanye kazi kwa weredi jamani utakuta mtu kitu ni cha kukaa saa moja lkn watakuweka hata saa sita siyo fair inakera sana.