BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Baada ya watu 191 kunusurika kwenye tukio la moto katika jengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), tukio hilo limetajwa kuwa ni mazoezi ya kukabiliana na majanga ya moto.
Licha ya kunusurika huko mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo alikimbizwa katika kituo cha afya cha Makole kupatiwa matibabu baada ya kuvuta moshi.
Tukio hilo lilitokea saa 3.54 asubuhi ambapo baada ya moto huo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika na kuanza kuuzima, zoezi lilochukua dakika tano huku wananchi wakishuhudia.
Wafanyakazi wa TRA waliokuwa ghorofani walishuka huku baadhi ya wateja wakitoka nje na kuanza kukimbia.
Barabara ya jirani na jengo hilo ilifungwa huku baadhi ya watu wakikatazwa kuingia katika jengo hilo na waliokuwepo hawakutakiwa kutoka.
Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Kabula Mwamezi amesema walikuwa wakifanya zoezi hilo kupima utayari wa wateja na wafanyakazi wa mamlaka hiyo pindi litakapotokea janga la moto.
Amesema anashukuru kila mmoja amekuwa na utayari na wameona kwa vitendo kama likitokea tukio wanatakiwa kufanya nini.
“Sasa turudi ndani tuendelee na kazi kama kawaida tulikuwa tunafanya mazoezi kwa vitendo,”amesema Meneja huyo.
Kamanda wa Zimamoto na Ukoaji, Mkoa wa Dodoma, Julishaeli Mfinanga amesema wamefanikiwa kuwaokoa watu 191 waliokuwa ndani ya jengo hilo ambao ni wateja na wafanyakazi.
Amesema baada ya kupokea simu kutoka TRA walitumia dakika tatu kufika katika jengo hilo na kuanza kuokoa watu pamoja na kufanya jitihada za kuuzima moto huo.
“Mtu mmoja alipatwa na mshtuko na tulimkimbiza hospitalini anaendelea vizuri. Niwapongeze wafanyakazi kwa kuwa na utayari,”amesema Kamanda huyo.
MWANANCHI