Mazoezi ya nusu saa yahairisha mechi ya Simba vs Yanga

Mazoezi ya nusu saa yahairisha mechi ya Simba vs Yanga

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Leo 18:50hrs 08/03/2025

Simba ina sifa ya kugoma ila Yanga ina sifa ya utii na kufuata kanuni,sasa leo sababu ya utoto kabisa imehairisha mechi,hawakufikiria gharama za watu kutoka mikoa 31 waliokuja Dar es Salaam kuangalia mechi ya Simba na Yanga,mtaani watu wamepamba Maputo rangi nyeupe na nyekundi,njano na kijani,wengine leo hatujafunga halafu mechi inahairishwa!?

Ipo siku wachezaji watawasusia tiefuefu na timu wacheze wenyewe uwanjani bila mashabiki na mapato ya uwanjani ili liwe funzo waache kucheza na akili na pesa za mashabiki. Tofauti na hivyo hivi vilabu na hao tiefuefu/bodi hawataacha huu ujinga kamwe,bodi ni lazima itoe tamko la kikanuni kuonesha kuwa kuna sababu ya kikanuni iliyopelekea mechi kuhairishwa,Yanga ilivyoenda Congo kuikabili Mazembe ilifanyiwa figisu sana ila wanaume hawa waliingiza timu na wakapata matokeo.

Tujiulize,hivi inawezekana vipi kuahirisha mchezo wenye mhemko mkubwa kama huu huku watu wakiwa tayari wako uwanjani na kwa sababu ambazo actually ni za kitoto sana na zilipaswa kushughulikiwa mapema kabla..? Yani wiki nzima haijawatosha kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Mkapa na kupata fitness ila wanaamini masaa ya usiku yasiyozidi sita yatawapa fitness ya kuifunga Yanga! Simba wakubali tu wameiogopa Yanga,nyingine ni visababu visivyokuwa na kichwa wala miguu.

Tukiachana na Ushabiki pale hakuna kanuni inayoibeba Simba ya kutofika uwanjani, hiyo kanuni hakuna ndio maana kwenye taarifa ya klabu hakuna nukuu ya kifungu cha kugomea mechi ila kwenye kanuni kuna kifungu cha adhabu ya timu ambayo inagomea mechi kutokana na makosa ya kikanuni😀! Ukitaka kuamini tuwaulize bodi na tiefuefu,je SIMBA ametumia kifungu gani kugomea mechi, hakipo.

Kanuni iliyotumika hapo inaitwa UTU UZIMA DAWA,hapa SIMBA anajua anachokifanya tena vizuri mno kete imesukumwa, sasa tiefuefu na bodi rasmi wamewekwa mtegoni endapo mechi italazimika kusogezwa mbele YANGA watauliza ni kwa mujibu kwa kifungu kipi? Endapo Yanga atagoma kucheza mechi iliyosogezwa mbele je bodi na tiefuefu wataihukumu Yanga kwa kifungu kipi? Hapo ndipo utata ulipo leo kwa utoto wa Simba kugomea mechi.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effects of microfinancing on poverty reduction.
 
Kuna mmasai kauza ng'ombe ili aje kuangalia mechi.
 
Kukiwa na makosa basi yasemwe lkn tukisimamia ushabiki basi sote tunadidimiza tasnia ya michezo hususani mpira wa miguu kwa kupitia usimba na uyanga.
Mleta mada eneo kubwa kaonesha ushabiki wa klabu yake ya yanga hivyo watu wengine kuona hakuna haja ya kutilia maanani wazo lake.

Kwa kweli kwa kuzingatia haki ya mashabiki, bodi ya ligi inamakosa na sio simba au yanga kwenye kuahirishwa mchezo huu. Watu wamepta hasara kubwa wamehatarisha maisha yao kwa kusafiri umbali mrefu alafu mnahairish mechi kirahisi kiasi hiki.
Ili kupta nguvu ya kutoa adhabu kwa wenye makosa bodi ya ligi haikupaswa kuahirisha mechi hii. Ili atakayegomea akutane na rungu la haki.
Sasa bodi imehairisha ikimaanisha nini kwenye barua inajichanganya mara simba hawakutoa taarifa kwa kuitumia haki yao ya kifung 17:45 ya shirikisho la mpira tanzania ikimpa haki mgeni kufanya mazoezi walau mara moja siku moja kabla ya mchezo kuchezwa.
Lkn bado inajichanganya kuwa mabaunsa wa yanga kwa waliotambulika kwa uchache wao waliwazuia simba kutumia haki yao ya kikanuni.....
Hapa walimaanisha simba walipaswa kuingia na kufanya mazoezi lkn ni hao hao wanaosema simba akutoa taarifa za kwenda kufanya mazoezi sasa kwa akili ya kawaida simba wangepokelewa na nani pale uwanjani walipozuiliwa na mabaunsa wa yanga ambao tff inadai waliwanyima simba haki ya kufanya mazoezi?

Kwa upande wangu tatizo naliona TFF na hivi virabu vinajua udhaifu aliona bwana TFF. Watatuendesha sana mpaka tukome kama chama chetu cha soka hakitakuwa imara katika kusimamia sheria na kanuni za mpira.
 
Siasa chafu, uchawa unauwa nchi. Kuja ku overcome hili tatizo la Uchawa itachukua muda sana
 
Kwa akili zako basi hata warm-up kabla ya mechi haina faida
 
Back
Top Bottom