Mazoezi ya viungo ni muhimu kwa afya ya mwili na akili.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mara nyingi ni kawaida kukutana na wana jeshi wastaafu wakiwa 90+ na bado wanaendesha maisha yao ya kila siku bila msaada wa mtu.

Yale mazoezi wanayoyapata jeshini yanawasaidia sana kuimarisha mwili. Pamoja na kula vyakula bora.

Unapotoka kukimbia au kufanya maoezi ya kutoa jasho, hata kama nyumba yako iko kwenye harakati za kupigwa mnada ubapata wasaa wa kuyasahau kidogo na mwili pamoja na akili kupata mapumziko ya muda.

Kama hujawahi kukimbia kuishiwa na pumzi kusikukatishe tamaa. Kimbia kwa dakika tano, Tembea dakika kumi. Ukiwa na control nzuri ongeza muda wa kukimbia kidogo kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…