nilikuwa naomba kuuliza, nimazoezi gani ya mwili ambayo yanaweza kukupunguza mwili haraka zaid
@wakuonewa Mazoezi Makubwa kwa ajili ya afya yako na kupunguza mwili wako kwa haraka jaribu kila siku uwe unatembea mwendo wa kilometa5 kwenda na kurudi. Yaani kama ni wewe unafanya kazi jaribu
hapo unapoishi toka kwa miguu Asubuhi mapema nenda kazini na unaporudi nyumbani rudi pia kwa njia ya miguu nakupa siku 40 utapunguwa mwili wako .Na kila Asubuhi unapo amka chemsha maji ya Uvuguvugu glasi moja tiya ndimu au limau moja kubwa kamulia hayo maji unywe kabla ya kula kitu fanya hivyo katika maisha yako utapunguwa sana.
Kuhusu kula chakula
Jaribu kutumia sahani ndogo, na usichote chakula mara ya pili
(usiongeze), watafiti wameona kwamba mtu anayetumia sahani kubwa mara nyingi anakula chakula kingi kuliko akitumia sahani ndogo.Nusu au zaidi ya mlo uliochotea kwenye sahani iwe ni vyakula vinavyotokana na mimea hasa mboga mboga. Kama unakula
sandwich ya mkate, kula nusu na
ongezea kwa mbogamboga na matunda.Asubuhi ule mlo wa kushiba zaidi na jioni ule chakula kidogo/chepesi
(usishibe sana usiku).Usile kwa haraka, mara nyingi unapokula kwa haraka unakula chakula kingi na pia chenye nishati nyingi.Ongeza vyakula vyenye makapi mlo kwa wingi kama mbogamboga, nafaka zisizokobolewa
(whole-grains), mara
nyingi vyakula hivi huwezi kula haraka wala huwezi kula kupita kiasi.Jipe muda wa kutosha kutafuna vizuri, na mara nyingi vyakula bora kama ugali wa dona, mkate wa brauni,mahindi ya kuchoma au kuchemsha, maharage, kunde huhitaji kutafunwa vizuri hivyo huwezi kula kupita kiasi.Epuka asusa zenye mafuta mengi, sukari nyingi au chumvi
nyingi.
Jizoeshe matunda, hindi la kuchoma au vyakula vingine vya aina hiyo.Jipe muda kujitayarishia mlo ulio bora wenye mboga mboga nyingi. Kumbuka ni uhai wako. Labda umetumia dakika 10 zaidi kutayarisha mlo lakini
imekuepusha kutumia siku nzima au zaidi kwa daktari na kulipa gharama kubwa.Epuka kutumia vyakula vilivyotengenezwa kwa haraka
(fast food) kwenye migahawa, mara nyingi vina mafuta mengi, chumvi nyingi au sukari
nyingi. Na pengine unaona umekula asusa
(snack) (Junk Food)tu, kwa hiyo unakula tena mlo mzima. Kwa mfano watu wengine husema
I grabbed something kwa maana hajala vizuri kumbe ni kwa kuwa alikula bila mpango.Epuka kula ukiwa
unaangalia TV, unatumia computer au unafanya shughuli nyingine kwani una hatari ya kula kupita kiasi.Tuwazoeshe watoto ulaji bora unaoshirikisha mbogamboga na matunda, na aina za kunde, nyama kwa kiasi. Epuka kummzoesha
chumvi nyingi, mafuta mengi au sukari nyingi. Akishazoea itakuwa shida kuacha. Mpende mwanao, mfundishe vitu vitakavymrefushia maisha.Epuka
pombe na sigara Fanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 au zaidi kila siku, hata kutembea tu.Kumbuka mwili wako unatokana na unachokula na mazoezi unayofanya.