Mazungumzo mafupi na wanagerezani - Gerezani Day

Mazungumzo mafupi na wanagerezani - Gerezani Day

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MAZUNGUMZO MAFUPI NA WANAGEREZANI - GEREZANI DAY

Leo nimezungumza katika Gerezani Day. Hadhira yangu ndani kuna wajukuu wa wapigania uhuru.

Nilizungumza kisa ambacho kiliwachukua sana wasikilizaji wangu.

Kisa cha Nyerere alipopita Mtaa wa Sikukuu na Lindi na "Motorcade," yake ya mapikipiki anakwenda Gerezani kufungua viwanda vidogo vidogo.

Ilikuwa katika miaka ya 1970.

Kwenye kona ya mtaa wa huo akamuona Bi. Mruguru bint Mussa mama yake Abdul kasimama pamoja na wananchi wengine wanaangalia "motorcade" ya rais inapita.

Nyerere bila shaka alikuwa akiangalia nje na kujikumbusha mitaa yake akipita akiwa na Abdul Sykes wanakwenda kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata au kwa mama yao Bi. Mruguru Kirk Street (sasa Lindi). Nyerere akamuona Bi. Mruguru kasimama.

Nyerere akasimamamisha msafara wake akafungua mlango wa Benz lake akatoka nje ya gari na kumwendea Bi. Mruguru kumsalimu.

"Motorcade" na walinzi wa Mwalimu walipogundua kuwa gari ya rais imesimama njiani ghafla ikawa mtafaruku mkubwa.

Walinzi wameruka katika magari yao.

Dakika si dakika Nyerere kazingirwa na walinzi wake wamemweka katikati yao.
Nyerere akaendelea kusalimiana na Bi. Mruguru.

Kisha wakaagana na Nyerere akaingia kwenye gari lake akaondoka.

Katika hadhira yangu wako ambao wao historia hii ni ngeni kabisa sura zao na ule utulivu waliokuwanao katika kunisikiliza natambua kutokana na uzoefu kuwa nimewagusa khasa.

Hawa hawakupata hata kumuona Nyerere katika ''motorcade'' ya mapikipiki achilia mbali kuona sura yake.

Hapo namweleza nani Bi. Mruguru na upi uhusiano wake na Nyerere.
Hii ni historia ya 1950s. Nyerere na hawa waliopewa mitaa wako bega kwa bega kupigania uhuru wa Tanganyika.

Namleta Bi. Tatu bint Mzee katika Halmashauri Kuu ya TANU 1955 kikao kinafanyika nyumbani kwa Clement Mtamila kama Chairman wa TANU wanajadili barua ya waajiri wa Nyerere, wamishionari wanamwambia achague siasa au kazi ya ualimu.

Nawaeleza WanaGerezani kuwa hapo aliposimama Nyerere na Bi. Mruguru nyuma kidogo ndipo ilipokuwa nyumba ya Mtamila. Namleta Abdul Sykes.

Baada ya mazungumzo yangu vijana wananiambia wao hawajasomeshwa historia hii ni mara yao ya kwanza kuisikia kutoka kwangu.

Picha ya kwanza: Kulia ni Mussa Abbas Sykes na kushoto ni Abbas Mussa Sykes kitukuu cha Bi. Mruguru bint Mussa akiwa katika Gerezani Day.

Kwa kijana Abbas mjukuu wa Balozi Abbas Sykes hii ni historia ya wazee wake vizazi vitatu, zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Ikiwa historia hii isingehifadhiwa leo angekuwa hana historia yake.
Hajui alikotoka.

1658115971984.png
1658116010068.png
 
Back
Top Bottom