Mazungumzo ya simu ya Rais Trump akimshinikiza Katibu Mkuu wa Jimbo la Georgia kubadili matokeo ya uchaguzi ya jimbo la Georgia

Mazungumzo ya simu ya Rais Trump akimshinikiza Katibu Mkuu wa Jimbo la Georgia kubadili matokeo ya uchaguzi ya jimbo la Georgia

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Rais wa Marekani, Donald Trump alimshinikiza Katibu Mkuu wa jimbo la Georgia kwa chama cha Republic, Brad Raffensperger kutafuta idadi ya kura za kutosha kubadilisha matokeo ya jimbo hilo akimtishia kuweza kutenda 'kosa la jinai' katika mazungumzo ya simu yaliyodumu kwa muda wa saa moja, gazeti la Washington Post limebaini.

Rais Trump amekuwa akidai kuwa kuna wizi wa kura katika uchaguzi wa Marekani uliofanyika miezi miwili iliyopita, uchaguzi uliomwezesha mgombea wa urais kwa chama cha Democrat, Joe Biden kushinda kwa kupata kura milioni 81.2 dhidi ya Donald Trump aliyepata kura milioni 74.2. Katika jimbo la Georgia, Joe Biden alimshinda Rais Trump kwa kura 11,779.

"Ninataka tu kupata kura 11,780, ikiwa ni nyongeza ya kura moja kuliko tunayohitaji," Rais Trump alimwabia Raffensperger kwa njia ya simu, akimtishia kuwa anaweza kushtakiwa kwa kutenda kosa la jinai asipokubaliana na haja yake.

"Unajua [Wademokrat] walichokifanya na hautaki kukiripoti," alisema rais Trump kwa njia ya simu. "Unajua ni kosa la jinai - hilo ni kosa la jinai. Na unajua, hutakiwi kuruhusu hilo. Ni hatari kubwa kwako na kwa Ryan, mwanasheria wako. Ni hatari kubwa."

Sikiliza sehemu ya mazungumzo ya Rais Trump na Raffensperger. Sauti ya Mshauri wa Raffensperger, Ryan Germany inasikika pia.


Uchaguzi wa Marekani umekamilika, na majimbo yote ya Marekani yamekwisharasimisha matokeo ya uchaguzi. Jitihada za Rais Trump kutafuta njia za kisheria kubadili matokeo zimegonga mwamba kutokana na kukosa ushahidi wa madai yake ya wizi wa kura, ikiwamo katika Mahakama Kuu.

Matokeo hayo yanatarajiwa kuidhinishwa siku ya Jumatano na Baraza la Congress.
 
Na mimi nayatafuta mazungumzo ya Uongo ndugu zangu?
 
Hivi Trump hakujua kama anarekodiwa?au hakufikiria kwamba mazungumzo yake yanaweza kurekodiwa?
 
Wamarekani hapa waliingia cha kike kama sisi mwaka 2015. Bora yao wana taasisi imara na zenye nguvu zisizoendeshwa na kauli za mtu yeyote vinginevyo kungenuka vibaya sana.
 
Back
Top Bottom