Nimefurahishwa sana na majaribio ya treni ya umeme kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma. Kwa kweli imenifurahisha sana kwa muda uliotumika mpaka Dodoma. Pamoja na hayo ninaona changamoto zilizopo huko mbeleni. Kwa Watanzania kama hatutakuwa maakini treni hii haitadumu kama ilivyoanza.
Mwanzo utakuwa mzuri lakini siku zitakavyokuwa zinasogea huduma zake zitakuwa haziridhishi kwa sababu ile ya kukosa uendelevu. Nitoe mifano niliyoyaona kwa miradi michache iliyopo Tanzania. Kwanza mabus ya mwendo kasi yalianza vizuri sana na wananchi tukafurahia huduma yao lakini leo hii usafiri huu umekuwa kero kubwa na matatizo haya yote tumeyaleta sisi Watanzania.
Hatuna utunzaji na uendelevu. Nia kubwa yetu Watanzania wachache ni Chukua chako Mapema. Pili, ni Uwanja wa Mkapa. Uwanja huu mwanzoni ulikuwa ni uwanja wa mfano katika nchi za Afrika Mashariki. Niliwahi kwenda siku moja kwenda kuangalia mechi hapo uwanjani.
Niliyoyaona kwenye vyoo vya uwanja huo ni ya aibu nakutisha. Watu wazima wanakojoa kwenye sinki za maji ya kunawia. Ninayasema haya kwa sababu yanauma na Watanzania hatuthamini chetu na kukitunza. Nina ushauri kwa Serikali.
Mradi wa treni ya umeme pindi itakapoanza ni budi serikali ikatafuta mwekezaji mahiri atakayeweza kusimamia uendeshaji wa shughuli zote za treni hii ya umeme vinginevyo ninawapa miaka mitatu mtaona majibu. Tuige mfano wa jirani zetu wa Kenya, treni yao inasimamiwa na Wachina.