Vipi mkuu
tpaul ulipona hili tatizo baada ya kutumia hayo mafuta uliyoambiwa na
Remote maana hata mimi nina tatizo hili mwaka wa 10 sasa na nimejaribu kila mafuta lakini bado. Ila hayo ya Movt sijajaribu, mtupe mrejesho mlioyatumia.
Pole sana mkuu. Hili tatizo hata mm limenisumbua kwa muda mrefu sana pamoja na kupaka kila aina ya mafuta yakiwamo hayo ya MOVIT. Mafuta ya movit sio kwa ajili ya tiba bali ni kwa ajili ya kinga na urembo kwa akina mama (yame-contain a little amount of sulphur ambayo haiwezi kutibu mba). Ukiona mtu amepaka haya mafuta amepona, basi huyo hakuwa na mba ila harara tu.
Baada ya kuteseka na mba za kichwani (dandruff) kwa muda mrefu, hatimaye nimepata tiba kutoka Hospitali/Clinic ya
Doctor's Plaza iliyopo Kinondoni Morocco, jirani na makao makuu ya Airtel. Ukifika Airtel, elekea upande wa Mashariki sambamba na barabara ya kuelekea Posta, vuka Furaha Medical Centre, kisha vuka hilo ghorofa jipya unaloliona hapo mbele, kwa mbele kidogo utaona ghorofa fupi ina maandishi yameandikwa
LANCET LABORATORIES...ndani ya jengo hili (
Second Floor) ndimo ilimo Clinic ya Doctor's Plaza inayofanya kazi chini ya mwavuli wa LANCET LABORATORIES yenye makao makuu Afrika Kusini.
Siku nilipoenda pale sikumkuta daktari wa ngozi lakini niliomba kuonana na daktari wa kawaida ambaye alini-prescribe dawa ya kupaka inaitwa
BEPROSALIC OINTMENT na vidonge vya kumeza vinaitwa
TERBIFIN. Hizi dawa zimefanikiwa kuponya tatizo langu lililonisumbua kwa zaidi ya miaka 20!
N.B: Beprosalic
ointment ni dawa muhimu sana na haipatikani kwenye maduka ya dawa ya kienyeji. Kwenye maduka ya kienyeji utauziwa Beprosalic
cream ambayo haina uwezo wa kutibu kama ointment. Na wafamasia wengi hawajishughulishi kuzinagtia hilo, kwa hiyo unapaswa kuwa makini wewe mwenyewe mnunuzi.