Mbadala wa CHADEMA ni CCM wala sio NCCR

Mbadala wa CHADEMA ni CCM wala sio NCCR

Jengeni hoja matusi ayasaidii hapo ndo ccm mnaoneka empty. Kumkosoa sugu most voters Tz nzima 2015 nikukosa hoja za msingi.
 
Kuna watu wanaamini kabisa Magufuli ndie jini aliekuja kuiua CDM, naisubiri kwa hamu sana hiyo siku ya kupiga,kura na kutangaza matokeo, iwepo tume huru au isiwe....nasisitiza tena, ninazisubiri kwa hamu sana hizo siku mbili.

Wengine wanaenda mbali kuamini NCCR itakuwa mbadala wa CDM bungeni, kama CDM nae ataweka wagombea kwenye hayo majimbo wanayoamini NCCR itashinda, basi nafasi ya kushinda CDM ni kubwa zaidi ya NCCR, na hata CCM wenyewe, ni suala la kupiga kura na kuzuia njia za wizi wa kura (CDM wajue namna ya kulinda kura zao).

Hata kama NCCR inategemea kubebwa, lazima wajiulize maswali ya msingi kama wamejiandaaje kubebwa?!, wakibebwa watabebeka?, na hili sio suala la kutoa na kuweka tu, kama wengi wanavyodhani/fikiri.

Kwa nafasi waliyonayo NCCR sasahivi ni vigumu sana NCCR kusimama mbele ya CDM kama chama kikuu cha upinzani nchini, hapa tusidanganyane, CDM watabaki chama kikuu cha upinzani hata kama wakiwa na wabunge watano, na kuna majimbo hata CCM wakiungana na NCCR balaa watalo kutana nalo toka CDM hawataamini.

Simply, CDM needs to go with their cylinders all out blazing, halafu tutaona hiyo Nov kama "mungu" wao atawasaidia, watanzania sio wajinga tena, hata Magufuli mwenyewe analijua hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sera ya kupambana na mafisadi ilikua ngazi kubwa sana iliyoleta hamasa ya mabadiliko,hivi ilishia wapi ?
au mafisadi wamekwisha ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sasa hivi CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO aka chadema ndio hasa watetezi wa rugemalira na seth singh.
Ushahidi ni hotuba za kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa sasa.
Tafuta clip za utube zote utawasikia.
Ogopa this peoples from there

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi watu wanapiga ramli za kuwa NCCR inaweza kuwa mbadala wa Chadema.

Hila ukweli uliopo hapa Tz mbadala wa Chadema ni CCM na mbadala wa CCM ni chadema.


Siasa ni mbinu ...chadema wamewekeza kwa vijana wasomi 70% ccm 25% Act 4.7% Nccr 0.3% chauma 0.00% Tlp 0.00% , Undp 0.00% Namba azidanganyi

Its just matter of time.
Kiongozi umemalizia hoja yako kwa kusema Namba hazidanganyi
sasa tunaomba utapatie formula iliyotumika kupata hizo asilimia zilizo ekezwa kwa vijana kwani nina wasiwasi huna uelewa wa 70% ya population ya vijana tulio nao TZ
 
Sasa hivi watu wanapiga ramli za kuwa NCCR inaweza kuwa mbadala wa Chadema.

Hila ukweli uliopo hapa Tz mbadala wa Chadema ni CCM na mbadala wa CCM ni chadema.


Siasa ni mbinu ...chadema wamewekeza kwa vijana wasomi 70% ccm 25% Act 4.7% Nccr 0.3% chauma 0.00% Tlp 0.00% , Undp 0.00% Namba azidanganyi

Its just matter of time.
Cdm ya new generation ccm ya wazee na kina mama wanaongopewa kirahisi.
 
Mkuu sasa hivi CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO aka chadema ndio hasa watetezi wa rugemalira na seth singh.
Ushahidi ni hotuba za kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa sasa.
Tafuta clip za utube zote utawasikia.
Ogopa this peoples from there

Sent using Jamii Forums mobile app
Ishu si utetezi ishu mchakato usio wa haki ,swali alipiga mwenyewe vipi maofisa wa serikali walioshirikiana nae kupiga vipi walionufaika na kupiga wao kwann wako nje.Pili kumshikilia mtu ndani miaka 5 ukisubiri upelelezi ambao hata miaka 60 hautokamilika ni kinyume na haki za binadamu pili ni matumizi mabaya ya Kodi zetu.Hamna kesi pale Kama wahusika wengine wako nje kitakachofanyika ni watakaa ndani then DPP atawaachia kesi za uhujumu uchumi ushahidi wake huwa ni vigumu kuupata na Hadi ukikaa ndani miaka 60 huwezi pata ushahidi labda tu labda tu ukubali kuununua Uhuru wako ukae nao meza moja kisha ukubali kosa hata Kama ukutenda ili uwe huru.Kinachowatesa hao ni kutokubali kuununua Uhuru wao maana yule bwana anachotaka ni kuabudiwa wakishamuabudu tu na kumpa heshima yake kesho tu wako nje.
Pana Jana elf 20 tu alipigwa uhujumu uchumi infact hakutenda Bali hakupewa nafasi ya kusikilizwa ili upate nafasi ya kusikilizwa yaani kupata haki yako ni lzm utakaa ndani miaka alikaa miezi 8 ndani akapima kipi Bora Kati ya familia nje na kukaa ndani miaka huku familia ikiteketea ukisubiria haki yako akaona akiri kosa ili apoteze kazi na kuepusha kukaa miaka akakiri akatozwa millioni moja na nusu na kazi ikaisha yuko huru nje anapambana na biashara kuokoa familia mambo yanakwenda.
Hawa wazee hawana cha kupoteza ni maamuzi yao wausujudie msalaba waubusu au la.Wote waliotoka walikubali kuubusu msalaba msalaba ukitakacho ni kusujudia tu then unakuwa huru.Huwezipewa kesi ya uhujumu uchumi ukiwa na chapa.
 
Kifupi unajua umeandika maoni yako ndio maana umeniambia naruhusiwa kukubaliana au kupingana na mtazamo wako, mimi nakulinga.

Wewe ni miongoni mwa wale mnaoamini wapinzani kazi yao ni kusifia, NO. wapinzani kazi yao ni kuisukuma serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake, na wanapoyapeleka, ndilo jukumu lao, wasisubiri kupongezwa, na kupongezwa ni uamuzi sio lazima, msichezee akili za watu kwenye hili.

Hebu niambie, kama serikali ikitaka kuanza kusifiwa na wapinzani, hiyo kazi ya sasa ya upinzani itafanywa na nani? au jamaa ndio watakuwa wapinzani wao na chama tawala wao at the same time?! muache haya maigizo.

Suala la ukata nalo kama litakuwepo basi litapiga pande zote, kuchangiwa watoke ndani it doesnt mean hawawezi fanya kampeni.

Kama mbunge wa CCM ataweza fanya kampeni jimboni, kwanini wa CDM ashindwe? hiyo issue ya msaada naamini mmeielekeza zaidi kwa NCCR kwasababu wao ndio wenye hali ngumu zaidi, ndio maana wakaahidiwa msaada siku ile walienda ikulu, but mnaitumia jumla kama "mind games" tu ili kujihalalishia wizi mtaoufanya, but it wont be easy for you guyz, believe me.

Issue ni kwamba, wanaweza pewa NCCR msaada wa kifedha, but wakafeli kwa wapiga kura kama hali inavyojionesha sasa, kwa hali ya kawaida, lazima msaada wa kifedha wataopewa uendane na uungwaji mkono wa chama husika kwa wapiga kura, vingibevyo ni kujidanganya tu NCCR itaenda kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni eti kwasababu watakuwa na uwezo wa kusimamisha wagombea kila jimbo, uchaguzi sio bahati nasibu mjomba, kila mtu apate, ni mbinu kama unavyosisitiza mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ccm ni tindo bila nyundo upinzani haiwezi fanya kazi kumbuka ccm inatekeleza sera za upinzani.Apingae upinzani apendi maendeleo
 
Africa Msomi hana nguvu wala hajui kuitumia akili na elimu, wapenda wachawi wakubwa ni walioelimika, mafisadi nj wao, wala Rushwa ni wao, vibaraka wa serekali za njee ni wao, wauza nchi, Imani, Mila na watu wao ni wao.

Zaidi ya hapo ubovu wa Chadema wamewaweka mbele wahuni na vibaka mbele kama viongozi, na wale viongozi wazuei wote wametimuliwa kwa namna moja ama nyengine, hebu chunguza waliojitoa ama kufukuzwa tokea 2010 hadi leo, andika majina yao na sababu ya kuondoka, utapata mshituko.

Chadema ikitegemea kupelekwa popote na akina Sugu,Lema, Mdee nk... basi tutangoja karne mbili

Sent using Jamii Forums mobile app

Haya ni mawazo ya bendera fuata upepo. Yaani kwa maneno marahisi, unatapika propaganda mfu unazozisikia kwa wanaume wenzio, na ww unazirudia humu kama zuzu.
 
Sasa hivi watu wanapiga ramli za kuwa NCCR inaweza kuwa mbadala wa Chadema.

Hila ukweli uliopo hapa Tz mbadala wa Chadema ni CCM na mbadala wa CCM ni chadema.


Siasa ni mbinu ...chadema wamewekeza kwa vijana wasomi 70% ccm 25% Act 4.7% Nccr 0.3% chauma 0.00% Tlp 0.00% , Undp 0.00% Namba azidanganyi

Its just matter of time.
Hakuna mbadala hata ccm inajua ndio maana inahangaika kuwafunga viongozi wa chadema kwa kesi za kitoto mwenye bunduku asishtakiwe eti ashtakiwe asiye hata na fimbo kwa kifo cha risasi Chadema ipo tu nunua wabunge,madiwani siasa za kishamba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni utoto,kwani hao akina mbowe walipitishwa na tume gani ya uchaguzi? Ndio maana mnaambiwa hamna hoja ya msingi kwa sasa. CDM Presidential candidate alipata kura 6000000 dhidi ya 8000000 za CCM na bado mnasema tume haikuwa Huru,au mnafikiria kwa kutumia upande mwingine huko.

Sent using Jamii Forums mobile app

Unachekesha walionunua. Hiyo tume haijawahi kuwa huru, na hicho ni kilio cha toka mfumo wa vyama vingi urudi hapa nchini. Hizo kura 6m japo zilitangazwa lakini bado watu hatukuridhika, kwani kuna vituo vingi tu kilichokuwa kinatangazwa na tume sio kilichokuwa vituoni. Toka ameingia Magufuli madarakani tumeona kwa macho yetu uhayawani na ukatili wa wazi ili mgombea wa ccm atangazwe mshindi. Na yote hayo ni kutokana na tume kutokuwa huru.

Hata huko ulaya wameleta mfumo wa VAR kwenye soka, sio kwamba mshindi alikuwa hapatikani, bali wanataka mshindi apatikane pasipo kuacha shaka. Kama mnashinda kihalali, hofu ya tume kutokuchaguliwa na mwenyekiti wa ccm inatoka wapi?
 
Yaani idadi ndogo ya watu ndio kusema watu wanataka kumwaga damu? Sasa kama MTU anaona vyovyote vile ccm itapita,kwanini aende kupiga kura? Hakuna kumwaga damu ktk kizazi hichi,kama unabusha subiri,Majeshi yapo imara,utaishia kumwaga damu yako tu na mambo yataendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ccm itashinda tu kwa uwezo gani, hayo majeshi huko Egypt au Sudan hayakuwepo?
 
Mkakati unataka uwe upi, cdm sio chama cha kigaidi, bali kinatumia njia za kisiasa kwani kina ushawishi mkubwa kwa watu. Kwasasa njia ya box la kura ndio ya amani, ndio maana tunadai tume huru ya uchaguzi. Iwapo njia hiyo ya box la kura haitafanikiwa, basi kuna njia nyingine nyingi zitatumika japo zina gharama zake.
Kwahiyo mpaka sasa hivi hii tume huru ya uchaguzi mkishaandika hapa mashabiki kadhaa kwamba "tunataka tume huru"
Basi ndio mmeshadai hivyo, na mnaanza kusubiri utekelezaji wa uundwaji wa tume huru?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha nicheke kwanza, nadhani unafikiri tume huru ni lazima idaiwe na cdm. Kwa taarifa yako tume huru ya uchaguzi tunaidai sisi wananchi tuliochoka kura zetu kuchezewa, na kuwekewa viongozi wasio chaguo letu. Nitakupa mfano mrahisi na halisi. Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi tuligoma kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura, na sababu ya kugoma ni ule uhayawani tuliouona kwenye chaguzi zote za marudio baada ya Magufuli kuingia madarakani. Mbowe na Halima Mdee hawakujua kuwa wananchi tunajitambua, wakaenda kujiandikisha na kuitisha watu kujitokeza kujiandikisha, hakuna mtu mwenye akili timamu alijitokeza kwenye uhuni ule. Baada ya kuona uhalisia wa wananchi kususia kujiandikisha, vyama vyote vya upinzani vilijitoa kwenye uchaguzi ule.

Hata sasa nadhani umeona mwenyewe jinsi watu wamepuuza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura. Hapa tulipo hatujali hata ikibaki wiki moja tunataka tume huru ya uchaguzi, vinginevyo hatuwezi kushiriki huo uhuni uitwao uchaguzi. Cdm au chama chochote cha siasa kinaweza kushiriki huo uchaguzi, lakini sisi wapiga kura tunaojitambua hatuko tayari kushiriki uhuni wowote bila tume huru ya uchaguzi. Kwa taarifa yako njia ya box la kura ni moja kati ya njia ya kuweza kupata kiongozi, lakini sio njia pekee ya kupata kiongozi. Umma unapoamua hakuna jinsi. Cdm au chama chochote kinachojali matakwa ya umma, ni juu yao kujua kuwa wapiga kura wengi hatuna tena imani na tume hii iliyopo ya uchaguzi, na hata wakipatikana viongozi chini ya tume hii, watukuwa viongozi kwa mujibu wa sheria, lakini hawatakuwa na uhalali wa umma.

Madhara ya kuwa na viongozi walio kisheria bila uhalali wa umma, sio rahisi kiongozi asiye na uhalali wa umma kushawishi jamii kushiriki shuguli za maendeleo. Ni nadra kiongizi asiye na uhalali kutoa tamko/amri na watu wakatii. Kiongozi huyo ataoongoza jamii yenye mpasuko na isiyomuheshimu. Kiongozi aliyepatikana bila ridhaa umma atajikuta akitawala kwa mabavu zaidi kuliko ushawishi na maelewano. Mifano ya kuongoza watu bila ridhaa yao, nadhani uliona watu wakivyofurahia timu ya taifa kufungwa huko Afcon baada ya Makonda kujihusisha na timu. Nadhani unaona watu wanavyofurahia majanga kwa taifa lao na kukosekana mshikamano. Kwa sasa kuna janga la corona, lakini mwitikio wa kuchangia hauna hamasa iliyokuwa huko nyuma, bali mwitikio ni wa hofu ya kimamlaka kuliko ridhaa ya watu. Tutafika mahali hata kuzikana tutaangaliana ww ni nani, sherehe nk. Hizi ni baadhi tu athari za kuongoza bila ridhaa ya wananchi. Huko tutakwenda,na serikali itakayotawala katika mazingira hayo haitapata uungwaji mkono wa kweli,labda ule wa kinafiki kama sasa, hali hiyo haitamuacha yoyote na furaha, kuanzia kiongozi wala mwananchi wa kawaida zaidi ya watu kutumia huduma zilizopo, bila kuappreciate chochote zaidi ya kubeza.
Hivi chadema na vyama vya upinzani hoja ya kujitoa kwenye ule uchaguzi ilikuwa ni kwa sababu ya wananchi kugoma kwenda kujiandikisha?

Kwa kumbukumbu zangu hoja yao ilikuwa ni wagombea wao kuenguliwa kimizengwe na kama ccm isingewaengua wale wagombea chadema na vyama vyote wangeshiriki na wala hiyo hoja ya kwamba mligoma kujiandikisha haina mashiko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachekesha walionunua. Hiyo tume haijawahi kuwa huru, na hicho ni kilio cha toka mfumo wa vyama vingi urudi hapa nchini. Hizo kura 6m japo zilitangazwa lakini bado watu hatukuridhika, kwani kuna vituo vingi tu kilichokuwa kinatangazwa na tume sio kilichokuwa vituoni. Toka ameingia Magufuli madarakani tumeona kwa macho yetu uhayawani na ukatili wa wazi ili mgombea wa ccm atangazwe mshindi. Na yote hayo ni kutokana na tume kutokuwa huru.

Hata huko ulaya wameleta mfumo wa VAR kwenye soka, sio kwamba mshindi alikuwa hapatikani, bali wanataka mshindi apatikane pasipo kuacha shaka. Kama mnashinda kihalali, hofu ya tume kutokuchaguliwa na mwenyekiti wa ccm inatoka wapi?
Tume ipo kwa mujibu wa katiba sasa kama mnataka mabadiriko ya tume anzeni na katiba itakayobeba hayo yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi chadema na vyama vya upinzani hoja ya kujitoa kwenye ule uchaguzi ilikuwa ni kwa sababu ya wananchi kugoma kwenda kujiandikisha?

Kwa kumbukumbu zangu hoja yao ilikuwa ni wagombea wao kuenguliwa kimizengwe na kama ccm isingewaengua wale wagombea chadema na vyama vyote wangeshiriki na wala hiyo hoja ya kwamba mligoma kujiandikisha haina mashiko.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli mizengwe ya wazi ilichangia vyama kutangaza kujitoa, lakini sababu hasa hata hivyo vyama vilijua fika ukiachia mizengwe iliyokuwepo, watu wengi hawakuwa wamejiandikisha, na wengi ni wapiga kura wa upinzani. Hivyo hivyo vyama vikaona havina haja ya kushiriki mchakato haramu, ambao hata wapiga kura wake wasingeshiriki.
 
NCCR ilishakufaga zamani za kale enzi za Mabere Marando, Masumbuko Lamwai na King Lyatonga Mrema kule timwili la Tanga......nashangaa kuniambia ati leo kuna NCCR chama cha siasa laah
 
Tume ipo kwa mujibu wa katiba sasa kama mnataka mabadiriko ya tume anzeni na katiba itakayobeba hayo yote

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuwepo kwa mujibu wa katiba hiyo haimaanishi kuwa ni tume huru. Magufuli sio mtu anayetii katiba, hasa katiba hii ambayo inamuweka juu ya sheria na katiba. Katiba iko pending na sababu hasa ni yeye haitaki kwa sababu zake binafsi, hata kama ccm waliichakachua. Hatuna tatizo na kusubiri hiyo katiba mpya, kuliko kushiriki huu uhuni uitwao uchaguzi. Cdm wao kama chama wanaweza kushiriki hilo watajua wao, ila sisi wapiga kura tunaojitambua hatuwezi kushiriki huo ushenzi.
 
Back
Top Bottom