KERO Mbagala Dar es Salaam: Vyoo vya Stand ya Mabasi na daladala Mbagala rangi tatu ni vichafu sana

KERO Mbagala Dar es Salaam: Vyoo vya Stand ya Mabasi na daladala Mbagala rangi tatu ni vichafu sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

KIXI

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2015
Posts
1,955
Reaction score
2,465
1️⃣ Vyoo vya stand ya mabasi na daladala Mbagala Rangi Tatu viko katika hali mbaya sana! Uchafu umekithiri.

2️⃣ Abiria na wafanyabiashara wanateseka kila siku kwa sababu ya mazingira haya duni. Hili ni eneo linalotumiwa na mamia ya watu kila siku, lakini hali ya vyoo ni ya kusikitisha.

3️⃣ Mbali na harufu mbaya, kuna ukosefu wa maji safi kwa ajili ya kusafisha vyoo na kunawa mikono. Hii ni hatari kwa afya ya watu.

4️⃣ Wananchi wengi wanalipa ada ndogo kutumia vyoo hivi, lakini bado huduma ni mbovu. Swali ni: Je, hizi fedha zinatumika vipi?

5️⃣ Mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua haraka! Tunahitaji usafi wa kudumu, maji safi, na mifumo mizuri ya usimamizi wa vyoo. Hii si anasa—ni haki ya msingi.
20250115_220549.jpg
20250115_220553.jpg
20250115_220617.jpg
20250115_220607.jpg
20250115_220603.jpg
20250115_220619.jpg
 
Hicho ni Choo cha MTU binafsi kumbuka hiyo stand ni kiwanja cha MTU binafsi.serikali hawana chao hapo!!!

Walaumu serikali Kwa kushindwa kujenga stand
 
Kwani ndio vilivyo jengwa kwa msaada wa watu wa Marekani....🙄
 
Watakuambia sababu kubwa ni USAID
 
Watumiaji ndio wachafu hamna ustaarabu lazim viwe vichafu
Samahani kaka, wakati unaandika haya maneno, ulihusisha akili yako japo kidogo?

hapo hakuna hata sehemu ya kunawia mikono baada ya kutoka toilet, angalia hiyo sakafu ilivyo, unataka watumiaji ndio wasafishe hiyo sakafu, watumiaji ndio watafute maji nje, unapochangia jaribu Kufikiri kwanza
 
1️⃣ Vyoo vya stand ya mabasi na daladala Mbagala Rangi Tatu viko katika hali mbaya sana! Uchafu umekithiri.

2️⃣ Abiria na wafanyabiashara wanateseka kila siku kwa sababu ya mazingira haya duni. Hili ni eneo linalotumiwa na mamia ya watu kila siku, lakini hali ya vyoo ni ya kusikitisha.

3️⃣ Mbali na harufu mbaya, kuna ukosefu wa maji safi kwa ajili ya kusafisha vyoo na kunawa mikono. Hii ni hatari kwa afya ya watu.

4️⃣ Wananchi wengi wanalipa ada ndogo kutumia vyoo hivi, lakini bado huduma ni mbovu. Swali ni: Je, hizi fedha zinatumika vipi?

5️⃣ Mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua haraka! Tunahitaji usafi wa kudumu, maji safi, na mifumo mizuri ya usimamizi wa vyoo. Hii si anasa—ni haki ya msingi.
View attachment 3226145View attachment 3226146View attachment 3226147View attachment 3226148View attachment 3226149View attachment 3226150
Vyoo vichafu ni hatari Kwa afya
 
Kwanza uchafu hamuwezi kuushinda hata siku moja
La pili ni lazima kuna kampuni au watu wa kusimamia usafi kila saa
Kama hela zinapigwa hata za kuoshea uchafu wenu basi mna tatizo kichwani
Mwambieni Trump atume watu
 
Hicho ni Choo cha MTU binafsi kumbuka hiyo stand ni kiwanja cha MTU binafsi.serikali hawana chao hapo!!!

Walaumu serikali Kwa kushindwa kujenga stand
Even choo ni cha mtu binafsi haijalishi huyo mmiliki ana wajibu wa kuhakikisha usafi wake unazingatiwa! 🚮🚽 Hakuna kisingizio cha kuwaachia watu watumie choo kichafu, iwe ni mali binafsi au ya umma. Kama anachukua pesa kutoka kwa watumiaji, basi huduma inapaswa kuwa bora.

Pia, eti kwa kuwa serikali haijajenga stand rasmi haiondoi jukumu la wamiliki binafsi kuhakikisha mazingira safi. Afya ya watu ni muhimu zaidi kuliko kusingia eti eneo sio la serikali
 
Hapo naona ndoo ya maji na kopo la kuchotea likiwa limetumbukizwa ndani. Halafu m'bongo utasikia anakuambia ''kutawaza ndiyo usafi, kutumia toilet paper ni uchafu''. Nina.
na hapo nilikuta maji hayatoki , yaani haja inaweza kukata kabisa
 
Back
Top Bottom