Mbao wadai mwamuzi aliwanyonga

Mbao wadai mwamuzi aliwanyonga

Ni sawa na ule msemo wa ukiwa mbunge wa upinzani basi we kila kitu kinachofanywa na Serikali ni kukosoa tu...! Ndo kinachotokea hapa wana yanga wanasema ile sio penalty ilhali mpira tumeangalia wote, tukio tumeona wote ila wanabisha tu kwakuwa wao ni wapinzani wa simba
 
Refa alikuwa upande Wa simba waziwazi. Angalia alipomaliza kipindi cha pili, mbao fc walikuwa kwenye move kuelekea lango LA simba lakini mwamuzi akapuliza kipenga cha kumaliza mpira. Huu si umalizaji mzuri.
Kawaida Mpira huisha si kwenye shambulizi kama hili. Binsfsi si shabiki Wa Mbao ila iliniboa sana
 
Referee walikuwa making kwenye hiyo fainari kwani mda wore walikuwa anaangalia SAA yake lakini umakini wake Wa kuangalia SAA kila wakati Kwa lengo asije akajiasahau kutoa penati ndani ya mda Wa uwanjani kwani zikiingia penati Hazina mwenyewe lolote laweza kutokea!
 
Refa alikuwa upande Wa simba waziwazi. Angalia alipomaliza kipindi cha pili, mbao fc walikuwa kwenye move kuelekea lango LA simba lakini mwamuzi akapuliza kipenga cha kumaliza mpira. Huu si umalizaji mzuri.
Kawaida Mpira huisha si kwenye shambulizi kama hili. Binsfsi si shabiki Wa Mbao ila iliniboa sana
Mkuu uko serious kweli! Kinachomaliza mpira sio uko eneo lipi la mpira bali muda ukifika wa kumaliza mpira! Hizi fikra ndo zinaleta fujo, watu hawaangalii tena mpira kama professionalism yenye sheria bali kuangalia hisia na matamanio yao
 
Refa alikuwa upande Wa simba waziwazi. Angalia alipomaliza kipindi cha pili, mbao fc walikuwa kwenye move kuelekea lango LA simba lakini mwamuzi akapuliza kipenga cha kumaliza mpira. Huu si umalizaji mzuri.
Kawaida Mpira huisha si kwenye shambulizi kama hili. Binsfsi si shabiki Wa Mbao ila iliniboa sana
Sio kweli mkuu, refa anamaliza mpira muda wa mchezo unapoisha na sio kusubiria tukio Fulani litokee
 
Mbona Azam Tv walionesha tukio mubashara na wote tulishuhudia mpira ukigonga mkono wa beki wa Mbao bila ubishi kabisa, wanataka kutuambia nini sasa! Ahsante Azam Tv maana kama sio wao hakika ubishi huu usingeisha kamwe kwa jinsi sisi wabongo tulivyo!
Was it hand to ball or ball to hand?
 
BAADA ya kupoteza mchezo wa fainali ya Kombe la FA mbele ya Simba kwa mabao 2-1, wachezaji wa Mbao FC wamemtupia lawama za waziwazi mwamuzi aliyechezesha mechi hiyo, Ahmed Kikumbo kutoka Tanga.

Juzi Jumamosi, Mbao FC ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Simba katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Kilio cha Mbao kwa mwamuzi huyo wa kati ni namna alivyowazawadia penalti Simba dakika ya 118 ambayo Shiza Kichuya alifunga na kufanya matokeo kuwa 2-1 mpaka mwisho, wakidai kwamba hakukuwa na madhambi yaliyofanyika kwenye eneo la hatari.

Beki wa kulia wa timu hiyo, Boniface Maganga, amesema mwamuzi hakuwa makini kwenye uamuzi wake, kwani hakuna mchezaji aliyefanya madhambi kwa kushika mpira kwenye eneo lao la hatari kama alivyodai mwamuzi, jambo ambalo liliwatoa mchezoni.

“Ukiangalia vizuri utagundua kwamba hakuna mchezaji wetu aliyeshika, bali ulimgonga sehemu nyingine katika harakati za kuokoa hatari, lakini tukashangaa mwamuzi anaweka penalti,” alisema Maganga.

Naye kocha wa kikosi hicho, Etienne Ndayiragije, raia wa Burundi, amesema wamekubali matokeo hayo na amewapongeza wachezaji wake kwa kazi kubwa waliyoifanya tangu mwanzo hadi mwisho wa michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa, wakati mwamuzi huyo anaamuru iwe penalti, wachezaji wa Mbao walimvaa na kutaka kumpiga mpaka askari walipoingia uwanjani na kumuokoa hali ambayo ilimfanya hadi Ndayiragije na benchi lake la ufundi kufanya kazi ya ziada ya kuwatuliza ambapo mchezo ulisimama kwa takriban dakika tatu.

KUweni wakweli. Kwani hakushika mpira?
Cheki hapa chini?
 
Ukiangalia vizuri hata Yule mchezaji aliyeshika Mpira hakuwa akilalamika
Mkuu tuko pamoja yule mchezaji alieunawa mpira alikua mpole mno nafikiri moyoni aliwashangaa sana wenzake wakihemuka.wabongo tuache ushabiki tuwe wahalisia.
 
Was it hand to ball or ball to hand?
Swali zuri hilo, angalia natural position ya mkono, Je mpira uliufata mkono kwenye natural position, mbili kulikua na ulazma wa kutoa mkono vile? Tatu mpira ulikua spd Kali kiasi cha mtu kushindwa kutoa mkono?
 
546fcb9bf226d3348bcd8fc68dad5f94.jpg
mwenye macho haambiwi Tazama.
 
Was it hand to ball or ball to hand?
Kwa mujibu wa mkufunzi wa waamuzi, Leslie Liunda, hiyo si hoja pekee ya kubatilisha au kuhalalisha adhabu. Kuna natural position ya mikono na speed ya mpira pamoja na busara za mwamuzi. Mwisho wa yote, kinachoangaliwa ni maamuzi ya mwamuzi
 
Mbona Azam Tv walionesha tukio mubashara na wote tulishuhudia mpira ukigonga mkono wa beki wa Mbao bila ubishi kabisa, wanataka kutuambia nini sasa! Ahsante Azam Tv maana kama sio wao hakika ubishi huu usingeisha kamwe kwa jinsi sisi wabongo tulivyo!
Kama. Mpira uligonga mkono basi haikuwa penalty mkuu.
 
Mbona Azam Tv walionesha tukio mubashara na wote tulishuhudia mpira ukigonga mkono wa beki wa Mbao bila ubishi kabisa, wanataka kutuambia nini sasa! Ahsante Azam Tv maana kama sio wao hakika ubishi huu usingeisha kamwe kwa jinsi sisi wabongo tulivyo!
Katazame tena uache uongo
 
Back
Top Bottom