Mbao zenye dawa ni bora kuliko chuma

Mbao zenye dawa ni bora kuliko chuma

Mbao Tanzania

Senior Member
Joined
May 31, 2021
Posts
170
Reaction score
215
Inatamanisha kutumia chuma katika kuezeka au kukamilisha ujenzi wa majengo na utengezaji wa samani kama vitanda, meza, makochi n.k.

Lakini malighafi ya chuma ni gharama sana na inaweza kukupatia hasara. Chuma kinapata kutu, kinaoza, kinasumbua kwenye uandaaji na matumizi yake.

Ni bora kutumia mbao zilizotiwa dawa ya kuzitunza na kuua wadudu, hizi unaweza kudumu nazo katika ujenzi na utengenezaji wa thamani kwa hata zaidi ya miaka 50.

Tumetimiza wajibu wetu wa kutoa ushauri.
 
Asante kwa ushauri mzuri..tumekusikia
 
Ni ulize kidogo ndugu, mbao ngumu mfano mninga mkongo na wanziwe izinapaswa kuwekwa dawa kama ilivyosema
 
Hapana, mbao za aina hiyo hazina ulazima wa kuziweka dawa kwani zenyewe asili yake ni ngumu na imara sana.
 
Mkuu, naomba kuuliza, Je Mkangazi ni moja ya mbao ngumu isiyoliwa na wadudu?. Nataka kutumia kwa fremu za madirisha
 
Inatamanisha kutumia chuma katika kuezeka au kukamilisha ujenzi wa majengo na utengezaji wa samani kama vitanda, meza, makochi n.k.

Lakini malighafi ya chuma ni gharama sana na inaweza kukupatia hasara. Chuma kinapata kutu, kinaoza, kinasumbua kwenye uandaaji na matumizi yake.

Ni bora kutumia mbao zilizotiwa dawa ya kuzitunza na kuua wadudu, hizi unaweza kudumu nazo katika ujenzi na utengenezaji wa thamani kwa hata zaidi ya miaka 50.

Tumetimiza wajibu wetu wa kutoa ushauri.
Hizi dawa zenu feki zinavutia sana wadudu, tena wanazipenda na kuzihusudu.
Kwa ambao tuko mbali na bahari, chuma ni bora zaidi
 
Wasalaam,
Wakuu naomba ushuhuda wa mdau ambaye amewahi kutumia hizi mbao treated ambazo zimezagaa sana hapa mjini kwa mwonekano wa rangi ya kijani atupe ushuhuda wake juu ya ubora wa mbao hizo dhidi ya wadudu wanaokula mbao.
Mbao ninazozizungumzia ni hizi ambazo unakuta mmiliki wa hardware ananunua mbao ambazo hazina dawa, kisha anazichovya kwenye mapipa yenye dawa na kuziuza kama treated.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
kwa uhakika zaidi nunua dawa yako mwenyewe uzitibu
hizo nyingine ni rangi tu hamna dawa mle
 
Wakuu naomba ushuhuda wa mdau ambaye amewahi kutumia hizi mbao treated ambazo zimezagaa sana hapa mjini kwa mwonekano wa rangi ya kijani atupe ushuhuda wake juu ya ubora wa mbao hizo dhidi ya wadudu wanaokula mbao.
wengi wanaweka dawa za ukili
hata ile dawa yenyewe haimzuii yule 'mdudu msumeno' kuicharanga
 
Sina utaalam wa kujenga lakin kuna dawa tulikua tunatumia kwenye ujenzi wa greenhouse Ku treat ile mirunda/poles inaitwa Tanaleth , nzito lakin inachoma sana kwenye ngozi. Hiyo ilikua nzuri sana. Sijui kama bado inapatikana.
 
Wasalaam,
Wakuu naomba ushuhuda wa mdau ambaye amewahi kutumia hizi mbao treated ambazo zimezagaa sana hapa mjini kwa mwonekano wa rangi ya kijani atupe ushuhuda wake juu ya ubora wa mbao hizo dhidi ya wadudu wanaokula mbao.
Mbao ninazozizungumzia ni hizi ambazo unakuta mmiliki wa hardware ananunua mbao ambazo hazina dawa, kisha anazichovya kwenye mapipa yenye dawa na kuziuza kama treated.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Usikubali mbao ambayo imekuwa treated tayari na wauzaji na pia usikubali dawa ambayo inawekwa na wauzaji, nunua dawa mwenyewe, weka mwenyewe kwenye pipa lao halafu waachie wao wahangaike kuzi treat, wakiweka dawa wenyewe jua tu unawekewa rangi ya kijani ya keki, mchwa wakija baadae imekula kwako.
 
Wasalaam,
Wakuu naomba ushuhuda wa mdau ambaye amewahi kutumia hizi mbao treated ambazo zimezagaa sana hapa mjini kwa mwonekano wa rangi ya kijani atupe ushuhuda wake juu ya ubora wa mbao hizo dhidi ya wadudu wanaokula mbao.
Mbao ninazozizungumzia ni hizi ambazo unakuta mmiliki wa hardware ananunua mbao ambazo hazina dawa, kisha anazichovya kwenye mapipa yenye dawa na kuziuza kama treated.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Tatizo uhuni mwingi, wengine wanazipaka rangi za ukili ule wa kushona mikeka.
 
Wasalaam,
Wakuu naomba ushuhuda wa mdau ambaye amewahi kutumia hizi mbao treated ambazo zimezagaa sana hapa mjini kwa mwonekano wa rangi ya kijani atupe ushuhuda wake juu ya ubora wa mbao hizo dhidi ya wadudu wanaokula mbao.
Mbao ninazozizungumzia ni hizi ambazo unakuta mmiliki wa hardware ananunua mbao ambazo hazina dawa, kisha anazichovya kwenye mapipa yenye dawa na kuziuza kama treated.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Hakuna dawa hapo mkuu, imewekwa rangi tupu.
 
kama mfuko wako uko vizuri nenda sao hill pale unapata mbao treated kweli na kwa vipimo sahihi na kamwe hutojutia hela yako.
 
Hii nchi inataka kuzidi sasa, asilimia kubwa ya watu wanakoment kuwa ile sio dawa/sumu bali ni rangi.

Tutakuwa tumejitengenezea mazingira mabovu ambayo yanamnyima kufaidi kila awaye yote. Trust issues kwa wataalamu, mafundi na viongozi haimuachi mhusika yeyote salama.
 
Chuma ni nzuri kuliko mbao hilo halipingiki sio kutu ukiwa unataka kitu chenye uhakika huwezi kwepa gharama mbao ni bahati nasibu wauzaji wengi ni matapeli wanashawishi ili ununue dawa wanazoweka kwenye mbao ni feki haswaa na sio zile wanazotumia kwenye majengo ya serikali nk dawa ya mbao ya kuchemsha ndio kiboko ya wadudu ila sio huo utapeli wa kuroweka kwenye pipa mnaongeza na pesa
 
Vyotebni bora kama vikiandaliwa kwa ubora, vikawekwa kinga na vikatumika kwenye ujenzi kwa kufuata kanunui madhubuti....

Vyote ni vibovu kama niliyotaja hapo juu havito fuatwa.
 
Back
Top Bottom