Mbappé akabidhiwa jezi ya heshima ya Modrić, aanza enzi mpya Real Madrid

Mbappé akabidhiwa jezi ya heshima ya Modrić, aanza enzi mpya Real Madrid

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Real Madrid wamemkabidhi rasmi Kylian Mbappé jezi namba 10, iliyokuwa ikivaliwa na gwiji Luka Modrić, ambaye amejiunga na AC Milan baada ya kuhudumu Santiago Bernabéu kwa zaidi ya miaka 12.

Hatua hiyo inaashiria enzi mpya ndani ya kikosi cha Los Blancos.

IMG_5674.jpeg


Mbappé amekuwa akivaa jezi namba 10 katika timu ya taifa ya Ufaransa tangu 2018, akiiwakilisha kwa mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa Kombe la Dunia. Hata hivyo, katika klabu alizopita kama Monaco na PSG, alivaa namba 29 na baadaye 7.

Hii ni mara ya kwanza kupewa namba 10 katika klabu, akirithi kutoka kwa Nahodha Luka Modrić mshindi wa Ballon d’Or mwaka 2018.
IMG_5675.jpeg
 
Back
Top Bottom