Tofauti kubwa kati ya Mbaraka Mwinshehe na Juma Kilaza ni kwamba wakati Mbaraka alikuwa anatunga nyimbo zenye ujumbe wa moja kwa moja, Kilaza alikuwa zaidi akitunga nyimbo katika mfumo wa mashairi (guni) yenye mafumbo, kiasi cha kuficha sana ujumbe hivyo si rahisi kugundua matusi yanayotajwa na Mbaraka. Kwa kadri ya kumbukumbu yangu Kilaza hajawahi kutoa wimbo wa matusi ya moja kwa moja yaliyomlenga Mbaraka ama Morogoro jazz. Baadhi ya nyimbo zenye mafumbo ni KWAKO NI KWAKO. Katika wimbo huu bila kuntaja wazi Kilaza anadai kwamba Mbaraka sio mtu wa Morogoro hivyo aache kusifia mji huo kama alivyofanya katika wimbo wa Morogoro yapendeza. Anamkumbusha kwamba anatakiwa kusifia kwao, (Mbaraka ni mzaramo wa kijiji cha Mzenga huko Kisarawe mkoa wa Pwani na ndiko alikozikwa). Alitunga na kurekodi wimbo huu mara tu baada ya Mbaraka Kutoa wimbo Morogoro yapendeza unaosifu uzuri wa mji huo.
unpatikana
View: https://youtu.be/EVfJDMJ8vkQ?si=EthWXdLyKfPbeOC7
Kwako ni kwako ewe mtoto
Hata ikiwa pango ni kwako
Kwako ni kule mwana utokako
Wazee wako kule waliko,
Na huko ndiko maskani kwako,
Nakuhusia mwana, sikia uliko we upo ugenini
mwana wapotea wee, rudi kwa haraka mwana wee sikia weeh
Wengi huwaona duniani humu
Wakiwa mbali na wazazi wao
Huona fahari kudharau kwao
Na kutoa sifa nchi za wenzao
Hawatayari na kujali yao
Huona fahari kudharau kwao
we mdharau kwao mwana nakwambia
eeh sawa na ndege muasi mwituni sikia eeh
Kuna wakati Mbaraka alihama Morogoro jazz na kwenda Kilombero jazz ambako hakukaa kwa kuwa aliona hapamfai na kuamua kujiunga na bendi ya Atomic jazz ya Tanga kwa kurubuniwa (ambako yasemekana kujiunga kwake na bendi hiyo kulisababisha mtafaruku mkubwa uliosababisha ahofie maisha yake na ajutie uamuzi huo) kwa bahati wazee wa Morogoro walimrejesha. Kilaza alipata habari ya Mbaraka kuhama bendi na kumrushia madongo kama kumkebehi na kumsimanga kwa kujifanya anamkanya mtoto aliyepotea kwa fumbo kali. Sehemu ya wimbo inasema
.........Wawapi hao wenzio waliokuwa na payo (hapa anamsuta akidai waliomrubuni wamemwacha peke yake baada ya kumwingiza kwenye matatizo)
kwa kufuata mlio na kumbe kuna kilio, mwanangu wewe (anamsimanga kwamba kwa kuhadaika kiurahisi sasa anajuta)
[wote] Wacha kutangatanga mwanangu wewe
Rejea mwana rejea haraka kuangukia
kama hutapokelewa radhi utajikosea, mwanangu wewe
[wote] Wacha kutangatanga mwanangu wewe
Kwa heri nakwambia, mwanangu wala hauna haya
Mwalimu anafundisha na wewe unachukua, mwanangu wewe
Kwa ufupi Kilaza alikuwa anakera sana na kwa mafumbo yake, ilikuwa ni rahisi kwake kukataa madai ya kumsema Mbaraka ama morogoro jazz
View attachment 3639718