Wimbo huu wa Mbaraka Mwinshehe ulikuwa ni jibu la madongo aliyokuwa akirushiwa na Juma Kilaza wa Cuban Marimba. Jambo hili lahitaji maelezo kidogo. Salum Abdalah Yazidu (SAY) alikuwa mwanamuziki maarufu sana pengine kuliko wote nchini katika enzi zake. Mwanzoni hakuwa na lengo la kuanzisha bendi bali kwa mapenzi yake ya muziki wa Cuba alichukua uamuzi wa kutoroka kwenda Cuba iii akafaidi kwa karibu zaidi muziki huu, lakini alichagua wakati mbaya kwenda huko kwani vita vya pili vya dunia vilikuwa bado kwisha hivyo akwakama Mombasa na kurudishwa kwa wazazi wake Morogoro. Ndipo aliporudi na kuanzisha bendi yake mwenyewe mwaka 1948 awali aliita Lapaloma baadae kuibadilisha jina na kuiita Cuban Marimba mwaka huu ulikuwa mwaka 1952, jina hili la Cuban Marimba bila shaka lilitokana na mapenzi yake makubwa kwa muziki wa Cuba. SAY hakuwa mtu pekee aliyependa sana muziki huu kwani tayari ulikuwa umeshapenda na kuteka nyoyo za wapenzi wa muziki eneo hili la Afrika Mashariki na ya kati kama moto na bendi nyingi zilizoanziswa nyakati hizo zilikuwa zikiiga muziki wa Cuba. Hali iliyofanya mitindo ya chacha, rumba, bolero na calypso kuwa maarufu sana. Pamoja na athari hizo SAY alikuwa akitoa tungo zake mwenyewe zilizokuja kuwa maarufu na kupendwa sana kiasi cha kampuni ya kurekodi muziki ya MZURI toka Mombasa kuifuata bendi ya Cuban Marimba Morogoro ili kurekodi nyimbo zao. Kwa bahati mbaya SAY alifariki 18 November 1965 na uongozi wa bendi kuchukuliwa na mwanamuziki mchanga sana wakati huo Juma Kilaza mwaka 1966.Nyimbo hii inanikosha mashairi yake yana kwenda kama hivi
"Tulikuwa na Salum mpaka kaenda Ahera wala hatukutukanana,
Aah, alipoingia yeye aliyoleta si miziki bali ni matusi,
Mji wa Morogoro, ulisifika sana kwa mambo ya miziki na nyimbo zenye maana ooh,
Aah, Amekuja mchafuzi wa jina la Moro Jazz ooh na Morogoro nzima!"
Wahenga nawauliza, je huyo Salum alikuwa ni nani na huyo mchafuzi anayeimbwa hapa na Mbaraka Mwinshehe alikuwa nani, manayekumbuka hii stori mtuhadithie.
Ya kale dhahabu!
Maelezo mazuriWimbo huu wa Mbaraka Mwinshehe ulikuwa ni jibu la madongo aliyokuwa akirushiwa na Juma Kilaza wa Cuban Marimba. Jambo hili lahitaji maelezo kidogo. Salum Abdalah Yazidu (SAY) alikuwa mwanamuziki maarufu sana pengine kuliko wote nchini katika enzi zake. Mwanzoni hakuwa na lengo la kuanzisha bendi bali kwa mapenzi yake ya muziki wa Cuba alichukua uamuzi wa kutoroka kwenda Cuba iii akafaidi kwa karibu zaidi muziki huu, lakini alichagua wakati mbaya kwenda huko kwani vita vya pili vya dunia vilikuwa bado kwisha hivyo akwakama Mombasa na kurudishwa kwa wazazi wake Morogoro. Ndipo aliporudi na kuanzisha bendi yake mwenyewe mwaka 1948 awali aliita Lapaloma baadae kuibadilisha jina na kuiita Cuban Marimba mwaka huu ulikuwa mwaka 1952, jina hili la Cuban Marimba bila shaka lilitokana na mapenzi yake makubwa kwa muziki wa Cuba. SAY hakuwa mtu pekee aliyependa sana muziki huu kwani tayari ulikuwa umeshapenda na kuteka nyoyo za wapenzi wa muziki eneo hili la Afrika Mashariki na ya kati kama moto na bendi nyingi zilizoanziswa nyakati hizo zilikuwa zikiiga muziki wa Cuba. Hali iliyofanya mitindo ya chacha, rumba, bolero na calypso kuwa maarufu sana. Pamoja na athari hizo SAY alikuwa akitoa tungo zake mwenyewe zilizokuja kuwa maarufu na kupendwa sana kiasi cha kampuni ya kurekodi muziki ya MZURI toka Mombasa kuifuata bendi ya Cuban Marimba Morogoro ili kurekodi nyimbo zao. Kwa bahati mbaya SAY alifariki 18 November 1965 na uongozi wa bendi kuchukuliwa na mwanamuziki mchanga sana wakati huo Juma Kilaza mwaka 1966.
Morogoro jazz ilianzishwa mapema kidogo mwaka 1944 hata kabla ya Cuban Marimba na ilipofika mwaka 1965 ndipo Mbaraka alipochaguliwa kuiongoza bendi hiyo. Bendi aliyojiunga mwaka 1964 baada ya kukatisha masomo yake shule ya sekondari Mzumbe. Hali hii ilifanya wanamuziki hawa wachanga (Juma Kilaza wa Cuban Marimba na Mbaraka Mwinshehe wa Morogoro jazz) kuanza kuoneana wivu na kuanza kurushiana vijembe, hivyo mchafuzi katika wimbo huu anayeimbwa na Mbaraka ni Juma Kilaza. Hata hivyo Mbaraka hakupata wasaa wa kutosha wa kupiga muziki enzi za SAY kwani alikuwa ndio kwanza kajiunga na Morogoro jazz bila shaka hapa anawazungumzia wanamuziki wenzake waliokuwepo enzi za SAY. Zipo nyimbo nyingine za aina hii wanamuziki wawili hawa walizitunga kuonyeshana ubabe. Kilaza akiwa mtunzi, mpangiliaji wa nyimbo na muimbaji Mbaraka naye akiwa mtunzi, mpangiliaji wa nyimbo, muimbaji pia mpiga gitaa la solo, akiimba huku anapiga gitaa hilo.
Ahsante sana mkuu kwa ufafanuzi huu, swali ni kuwa, huyo mchafuzi aliyeleta matusi ambaye kwa maelezo yako ni Juma Kilaza ni matusi gani aliyaleta, Kuna wimbo wowote unao ukumbuka ambayo ilikuwa wa matusi moja kwa moja. Kwa Moro Jazz?Wimbo huu wa Mbaraka Mwinshehe ulikuwa ni jibu la madongo aliyokuwa akirushiwa na Juma Kilaza wa Cuban Marimba. Jambo hili lahitaji maelezo kidogo. Salum Abdalah Yazidu (SAY) alikuwa mwanamuziki maarufu sana pengine kuliko wote nchini katika enzi zake. Mwanzoni hakuwa na lengo la kuanzisha bendi bali kwa mapenzi yake ya muziki wa Cuba alichukua uamuzi wa kutoroka kwenda Cuba iii akafaidi kwa karibu zaidi muziki huu, lakini alichagua wakati mbaya kwenda huko kwani vita vya pili vya dunia vilikuwa bado kwisha hivyo akwakama Mombasa na kurudishwa kwa wazazi wake Morogoro. Ndipo aliporudi na kuanzisha bendi yake mwenyewe mwaka 1948 awali aliita Lapaloma baadae kuibadilisha jina na kuiita Cuban Marimba mwaka huu ulikuwa mwaka 1952, jina hili la Cuban Marimba bila shaka lilitokana na mapenzi yake makubwa kwa muziki wa Cuba. SAY hakuwa mtu pekee aliyependa sana muziki huu kwani tayari ulikuwa umeshapenda na kuteka nyoyo za wapenzi wa muziki eneo hili la Afrika Mashariki na ya kati kama moto na bendi nyingi zilizoanziswa nyakati hizo zilikuwa zikiiga muziki wa Cuba. Hali iliyofanya mitindo ya chacha, rumba, bolero na calypso kuwa maarufu sana. Pamoja na athari hizo SAY alikuwa akitoa tungo zake mwenyewe zilizokuja kuwa maarufu na kupendwa sana kiasi cha kampuni ya kurekodi muziki ya MZURI toka Mombasa kuifuata bendi ya Cuban Marimba Morogoro ili kurekodi nyimbo zao. Kwa bahati mbaya SAY alifariki 18 November 1965 na uongozi wa bendi kuchukuliwa na mwanamuziki mchanga sana wakati huo Juma Kilaza mwaka 1966.
Morogoro jazz ilianzishwa mapema kidogo mwaka 1944 hata kabla ya Cuban Marimba na ilipofika mwaka 1965 ndipo Mbaraka alipochaguliwa kuiongoza bendi hiyo. Bendi aliyojiunga mwaka 1964 baada ya kukatisha masomo yake shule ya sekondari Mzumbe. Hali hii ilifanya wanamuziki hawa wachanga (Juma Kilaza wa Cuban Marimba na Mbaraka Mwinshehe wa Morogoro jazz) kuanza kuoneana wivu na kuanza kurushiana vijembe, hivyo mchafuzi katika wimbo huu anayeimbwa na Mbaraka ni Juma Kilaza. Hata hivyo Mbaraka hakupata wasaa wa kutosha wa kupiga muziki enzi za SAY kwani alikuwa ndio kwanza kajiunga na Morogoro jazz bila shaka hapa anawazungumzia wanamuziki wenzake waliokuwepo enzi za SAY. Zipo nyimbo nyingine za aina hii wanamuziki wawili hawa walizitunga kuonyeshana ubabe. Kilaza akiwa mtunzi, mpangiliaji wa nyimbo na muimbaji Mbaraka naye akiwa mtunzi, mpangiliaji wa nyimbo, muimbaji pia mpiga gitaa la solo, akiimba huku anapiga gitaa hilo.
Tofauti kubwa kati ya Mbaraka Mwinshehe na Juma Kilaza ni kwamba wakati Mbaraka alikuwa anatunga nyimbo zenye ujumbe wa moja kwa moja, Kilaza alikuwa zaidi akitunga nyimbo katika mfumo wa mashairi (guni) yenye mafumbo, kiasi cha kuficha sana ujumbe hivyo si rahisi kugundua matusi yanayotajwa na Mbaraka. Kwa kadri ya kumbukumbu yangu Kilaza hajawahi kutoa wimbo wa matusi ya moja kwa moja yaliyomlenga Mbaraka ama Morogoro jazz. Baadhi ya nyimbo zenye mafumbo ni KWAKO NI KWAKO. Katika wimbo huu bila kuntaja wazi Kilaza anadai kwamba Mbaraka sio mtu wa Morogoro hivyo aache kusifia mji huo kama alivyofanya katika wimbo wa Morogoro yapendeza. Anamkumbusha kwamba anatakiwa kusifia kwao, (Mbaraka ni mzaramo wa kijiji cha Mzenga huko Kisarawe mkoa wa Pwani na ndiko alikozikwa). Alitunga na kurekodi wimbo huu mara tu baada ya Mbaraka Kutoa wimbo Morogoro yapendeza unaosifu uzuri wa mji huo.Ahsante sana mkuu kwa ufafanuzi huu, swali ni kuwa, huyo mchafuzi aliyeleta matusi ambaye kwa maelezo yako ni Juma Kilaza ni matusi gani aliyaleta, Kuna wimbo wowote unao ukumbuka ambayo ilikuwa wa matusi moja kwa moja. Kwa Moro Jazz?
Kwa wapenzi wa muziki wa Mbaraka Mwinshehe Mwaruka Soloist National, hivi karibuni binti wa nguli huyo aitwae Muhtaji Mbaraka Mwinshehe anayeendeleza kazi ya baba yake, kwa support ya KC Media (kampuni yangu), amerekodi wimbo mwingine wa baba yake aliourudia upya katika studio za KC Records Wimbo unaitwa MTAA WA SABA nakufanya nyimbo alizokwisha rekodi katika studio hii kwa support ya KC Media kuwa tano: SHIDA, SONIASA, ESTER, MOROGORO YAPENDEZA na sasa MTAA WA SABA wimbo uliokatika mfumo wa video. Tafadhali kwa heshima ya nguli Mbaraka Mswinshehe tumuunge mkono binti huyu kwa juhudi zake, wimbo unapatikana youtubeTofauti kubwa kati ya Mbaraka Mwinshehe na Juma Kilaza ni kwamba wakati Mbaraka alikuwa anatunga nyimbo zenye ujumbe wa moja kwa moja, Kilaza alikuwa zaidi akitunga nyimbo katika mfumo wa mashairi (guni) yenye mafumbo, kiasi cha kuficha sana ujumbe hivyo si rahisi kugundua matusi yanayotajwa na Mbaraka. Kwa kadri ya kumbukumbu yangu Kilaza hajawahi kutoa wimbo wa matusi ya moja kwa moja yaliyomlenga Mbaraka ama Morogoro jazz. Baadhi ya nyimbo zenye mafumbo ni KWAKO NI KWAKO. Katika wimbo huu bila kuntaja wazi Kilaza anadai kwamba Mbaraka sio mtu wa Morogoro hivyo aache kusifia mji huo kama alivyofanya katika wimbo wa Morogoro yapendeza. Anamkumbusha kwamba anatakiwa kusifia kwao, (Mbaraka ni mzaramo wa kijiji cha Mzenga huko Kisarawe mkoa wa Pwani na ndiko alikozikwa). Alitunga na kurekodi wimbo huu mara tu baada ya Mbaraka Kutoa wimbo Morogoro yapendeza unaosifu uzuri wa mji huo.
unpatikana
View: https://youtu.be/EVfJDMJ8vkQ?si=EthWXdLyKfPbeOC7
Kwako ni kwako ewe mtoto
Hata ikiwa pango ni kwako
Kwako ni kule mwana utokako
Wazee wako kule waliko,
Na huko ndiko maskani kwako,
Nakuhusia mwana, sikia uliko we upo ugenini
mwana wapotea wee, rudi kwa haraka mwana wee sikia weeh
Wengi huwaona duniani humu
Wakiwa mbali na wazazi wao
Huona fahari kudharau kwao
Na kutoa sifa nchi za wenzao
Hawatayari na kujali yao
Huona fahari kudharau kwao
we mdharau kwao mwana nakwambia
eeh sawa na ndege muasi mwituni sikia eeh
Kuna wakati Mbaraka alihama Morogoro jazz na kwenda Kilombero jazz ambako hakukaa kwa kuwa aliona hapamfai na kuamua kujiunga na bendi ya Atomic jazz ya Tanga kwa kurubuniwa (ambako yasemekana kujiunga kwake na bendi hiyo kulisababisha mtafaruku mkubwa uliosababisha ahofie maisha yake na ajutie uamuzi huo) kwa bahati wazee wa Morogoro walimrejesha. Kilaza alipata habari ya Mbaraka kuhama bendi na kumrushia madongo kama kumkebehi na kumsimanga kwa kujifanya anamkanya mtoto aliyepotea kwa fumbo kali. Sehemu ya wimbo inasema
.........Wawapi hao wenzio waliokuwa na payo (hapa anamsuta akidai waliomrubuni wamemwacha peke yake baada ya kumwingiza kwenye matatizo)
kwa kufuata mlio na kumbe kuna kilio, mwanangu wewe (anamsimanga kwamba kwa kuhadaika kiurahisi sasa anajuta)
[wote] Wacha kutangatanga mwanangu wewe
Rejea mwana rejea haraka kuangukia
kama hutapokelewa radhi utajikosea, mwanangu wewe
[wote] Wacha kutangatanga mwanangu wewe
Kwa heri nakwambia, mwanangu wala hauna haya
Mwalimu anafundisha na wewe unachukua, mwanangu wewe
Kwa ufupi Kilaza alikuwa anakera sana na kwa mafumbo yake, ilikuwa ni rahisi kwake kukataa madai ya kumsema Mbaraka ama morogoro jazz
View attachment 3639718