SoC02 Mbaraka Mwinshehe na maonyesho ya Wajapan mwaka 1970

SoC02 Mbaraka Mwinshehe na maonyesho ya Wajapan mwaka 1970

Stories of Change - 2022 Competition

BARANGA MPINA

New Member
Joined
Aug 28, 2022
Posts
3
Reaction score
1
“TEKINOLOJIA HUWA HAIOMBWI HUIBWA, HUCHUKULIWA KWA HILA”

Mwanamuziki Mbarak Mwinshehe aliacha kumbukumbu ya wimbo wake; “kwanza tunatoa shukrani kwa serikali yetu ya Tanzania. Kwa kutupatia nafasi ya kwenda Osaka Japan, kwenye maonyesho ya Ulimwengu ya mambo yote ya viwanda na biashara. Mwaka wa sabini banda letu limesifika sana Japani.”

1. Wakati fulani TBC kwenye mdahalo uliokuwa umeandaliwa na Dk Ayub Rioba, kijana mmoja alicheka sana liliporejewa tukio la Tanzania kumpeleka Mwanamuziki kwenye maonyesho ya biashara ya bidhaa za viwandani.

2. Huyo kijana ni miongoni mwa wale wanaopenda kukosoa yaliyopita “criticizing the past”

3. Ilibidi kutetea, kwamba ilipotokea Japan kutoa mwaliko na kugharamia kila kitu, haingekuwa halali kwa Tanzania kuacha kushiriki.

4. Hiyo Tanzania ya mwaka 1970, ilikuwa na umri wa miaka mitatu tu tangu ichukue uamuzi mgumu mwaka 1967 ilipotaifisha mali za mabepari na kuziweka njia kuu za uchumi mikononi mwa dola.

5. Tanzania haikuwa na bidhaa za viwanda vyake za kwenda kuwaonyesha walimwengu kule Osaka (Japan). Tanzania isingeweza kupeleka sukari ya kiwanda cha TPC (Arusha chini) au majani ya chai ya kiwanda cha Brooke bond cha Mufindi.

6. Tanzania isingepeleka sabuni za Ommo, sulight wala butter aina ya Blue band, naam isingepeleka bidhaa za “ku- import” zilizokuwa na maandishi “made in England.”

7. Ilikuwa halali kwa Tanzania kunadi kilichokuwa chake tu, yaani ngoma zetu za asili na utamaduni wetu, ili walau kuvutia watalii.

8. Lakini kwanini Japan ilifanya vile kwa walimwengu?

9. JE, Tanzania ilikuwa na umuhimu gani kwa Wajapan hadi ikawa lazima ialikwe?

10. Hapa ndipo ulipo ulazima wa kulijua somo la kujitambua. Maana binaadamu asipojitambua, (asiyejitambua wala kujielewa) lazima wengine watakuja na kujifanya kumvumbua!

11. Wavumbuzi watajifanya kuwa wema wa kumjulisha mhusika alivyo, kisha watamwongoza hadi kwenye uwanja wao ili akifikishwa hapo wamtumie kwa manufaa yao.

12. Mjinga ataishi kwa faida ya wengine, hata akifanikiwa kufika mbinguni bado Mungu hatampa pole kwasababu ya ujinga wake.

13. Mapambano ya Japan yalianzaia mwaka 1945, hapo Ndege za kivita za Marekani zilipodondosha mabomu ya “Atomic” kwenye miji ya Hiroshima na Nagasaki.

14. Inaelezwa kwamba Rais wa Marekani wa wakati huo alisaini matumizi ya “Atomic” huku analia, alilazimishwa na wataalamu wake wa vita.

15. Baada ya Marekani kudondosha mabomu hayo, Rais huyo alitangaza kwamba udondoshaji wa mabomu utaendelea hadi Japan itakaposalimu amri na kukubali kushindwa vita.

16. Makamanda walimshauri kiongozi wa Japan aliyekuwa akipigana bega kwa bega akishirikiana na Adolf Hitler wa Ujerumani na Bennito Musolin wa Italia.

17. Makamanda wa kijapan walisema wanao uwezo wa kupeleka meli yao na kuibomoa New York kulipiza kisasi. Lakini kiongozi wa Japan aliwasihi wakubali matokeo huku akijiapiza “But I will conquer the world economically”

18. Baada ya kumalizika kwa vita (1945) Japan haikuruhusiwa kuwa na Jeshi lake, nayo ilitumia hali hiyo kama fursa ya kuzichepusha gharama za kijeshi na ulinzi, ikazielekeza kwenye elimu, uchumi na ufundi.

19. Japan iliwachukua vijana wake 1,000 wenye akili, wakajiunga na vyuo vya Marekani, lakini vijana wakiwa na maelekezo maalum kwamba wakimaliza kusoma waende kuomba vibarua kwenye viwanda vya magari.

20. Vijana hao walipohitimu wakajichomeka kwenye viwanda mbali mbali vya magari nchini Marekani, wakiwa na lengo maalum. Huyu akichunguza namna inavyotengenezwa, difu, mwingine ringi, mwingine gia boksi, mwingine kabureta, na kila kitu kilichohusu gari.

21. Baada ya kujiridhisha kwamba wamechota maarifa ya kutosha, vijana wa kijapan walirudi kwao mmoja mmoja kwa wakati wake. Waliporudi nchini mwao ndipo Japan ikaanza mradi wa kuunda gari yao.

22. CIA iliiarifu “Pentagon” (utawala wa Marekani) wakati huo ikiongozwa na Rais J. F. Kennedy, kwamba Wajapan wanaunda gari lao kutokana na tekinolojia waliyoiiba Marekani!

23. Lakini utawala wa Kennedy haukuona tishio lolote kwenye habari hiyo, maana kwa wakati huo kilichokuwa kinawatikisa wao kama watawala wa Marekani ni kitendo cha USSR kuiuzia CUBA makombora na Ndege za kijeshi.

24. Watawala wa Marekani walisema “that is a toy” wakimaanisha gari la kijapani litakuwa kama toi tu la kitoto.

25. Miaka hiyo ambayo watu wa Afrika walitoka kutawaliwa, yaani maziwa waliyonyonya kwenye ukoloni yakiwa hayajaisha kwenye mifupa yao, yeye aliyeonekana amenunua ama anatumia bidhaa ya kijapani ilikuwa aibu labda awe “illiterate” asiyejua kusoma wala kuandika.

26. Lakini waliosoma wa wakati huo walifurahia kutumia vitu “made in England.” Gari zilizotumika kwenye ofisi zote za serikali nchini mwetu zilikuwa aina ya Landrover 109.

27. Wakubwa waliokuwa na mshahara uliofikia shs 1,000/= au zaidi, walimiliki Pegeot 404 maana kulikuwa na utaratibu wa kukopeshwa gari na kukatwa shs 500/= kila mwezi kwa miaka minne.

28. Wajapan hawakukata tamaa waliendelea kuboresha magari yao hadi walipojiridhisha kwamba wanaweza kuingia kwenye ushindani wa soko kimataifa, ndipo wakaandaa maonyesho ya mwaka 1970 ya bidhaa za viwandani. Lengo likiwa kuyatambulisha magari yao.

29. Tanzania ilikuwa nchi mlengwa ama “strategic country” kutokana kwanza na siasa yake iliyojitangazia kwa wakati huo, maana Wajapani walijua Tanzania imejitangazia uadui na makampuni ya Ulaya mangaribi ambayo mali zao zilitaifishwa.

30. Wajapani pia walijua kwamba uhusiano wa Tanzania na nchi za Ulaya mangaribi umeingia ubaridi haifanani na Kenya.

31. Lakini pia Wajapani waliisoma hali ya Tanzania kijiografia, wakakuta kuna mazingira ya upendeleo, inapakana na nchi nyingi ambazo zingeweza kununua bidhaa za kijapan, Zambia, Burundi, Rwanda Zaire na Uganda ambazo hazina bahari (hazina bandari) na kwa maana hiyo zingeitegemea Tanzania.

32. Wajapani walikuwa na uhakika wa kuzipiku nchi za Ulaya mangaribi Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwenye soko la magari, kwasababu za kijiografia.

33. Tanzania imeunganishwa na Japani kwa bahari ya Hindi, meli iliyobeba mzigo wa magari ilitumia kati ya siku 21 hadi 28 (kwa wakati huo) na wala mzigo haukuliwa bandari nyingine yoyote, gharama za usafirishaji zilikuwa nafuu.

34. Baada ya maonyesho yao ndipo tulipoanza kuona gari za kijapani zikifurika nchini Tanzania, nakumbuka tukiwa wanafunzi tilivyokuwa tukichekana mtu anapokosea na kuita Dustan badala ya Dutsan.

35. Haikuchukua muda mrefu malori aina ya Bedford yaliyokuwa yakitengenezw Marekani, yalianza kutoweka na nafasi yake kuchukuliwa na ISUZU iliyopewa sifa za bandia ikiitwa Isuzu chuma mtupu!

36. Baadaye Wajapan wakaliingia Bunge letu, wakalishawishi, wabunge wakaanza kukopeshwa “mashangingi” taratibu Wajapani wakaziondoa serikalini gari za Kiingereza na Kifaransa.

37. Maendeleo ni kujiamini, Tanzania ikiongozwa na wanaojitambua, wanaojikubali na wanaojiamini, uwezekano wa kuufuta umaskini ni kazi ndogo kuliko wengi wanavyofikiri.

38. Tatizo ni imani. Hapa sijui kama dini za kigeni (Uislam na Ukristo) zina mchango wake katika kukandamiza fahamu za wasomi!

39. Maana Wajapani na Wachina wenye dini zao, hawana wasomi “hopeless.”

40. Katika Tanzania msomi mwenye shahada yake bado anawaza kuiibia wizara, kisha fedha alizoiba kuzificha kwenye Benki za Uswisi! Hapo kisomo + dini = 0 (sikitu)

41. Lakini hao “wasomi majanga” ndio waliotamalaki kwenye nafasi za uongozi kwenye maeneo yote na sekta zote. Wanaamini kwamba wanajua, wala hawajui kwamba hawajui.
“Can we pursue without elites?”
 
Upvote 0
Back
Top Bottom