LGE2024 Mbarali: CHADEMA yashinda vitongoji 4 kati ya 7 na CCM vitongoji 2

LGE2024 Mbarali: CHADEMA yashinda vitongoji 4 kati ya 7 na CCM vitongoji 2

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata ushindi katika kijiji cha Itamba, wilayani Mbarali, kwa kushinda vitongoji vinne kati ya saba. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika vitongoji viwili, huku kitongoji kimoja cha Mapangala kikikataa wagombea wote kwa kura nyingi za "HAPANA".

Matokeo ya kitongoji cha Mapangala yalikuwa kama ifuatavyo:

  • CCM: Kura 61
  • HAPANA: Kura 220

Kutokana na matokeo haya, CHADEMA inatarajiwa kuongoza halmashauri ya kijiji cha Itamba.

Ukiona hivyo ujue CCM wahakuwa na namna kabisa. Yaani mpaka kura za hapana zimeshinda ...OMG!!
 
Hivi kura za hapana zikiwa nyingi dhidi ya mgombea pekee, utaratibu unakuwa vip hapo?
 
Back
Top Bottom