Mbarali, Mbeya: Waogelea siku mbili kumsaka aliyeanguka darajani

Mbarali, Mbeya: Waogelea siku mbili kumsaka aliyeanguka darajani

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
CGFM RADIO wameripoti kwamba Wananchi wa Kijiji cha Kapunga Kata ya Itamboleo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamejitokeza siku mbili mfululizo kumtafuta Bwana Mussa Mganwa(35) mkazi wa Kapunga anayehofiwa kusombwa na maji baada ya kuteleza darajani

Mussa alisombwa na maji 28 Februari,2022 majira ya saa sita mchana wakati akijaribu kuvuka mto Chimala akielekea kupandikiza mpunga.

Wazamiaji wamejitokeza kumtafuta Musa bila mafanikio lakini wakiwa na matumaini kumpata licha ya kuogelea zaidi ya kilometa 25 bila mafanikio.

20220303_052436.jpg
20220303_052439.jpg
20220303_052444.jpg
 
Duh! Inatia hasira sana kwakweli! Yaani serikali katika eneo husika imeshindwa kufikiria njia njema ya kujenga daraja kunusuru uhai wa raia wake wa eneo hilo? Ona sasa raia kateleza kapoteza uhai kwa uzembe wao
 
Na hapo kunaonekana kabisa hakuna kikosi maalum cha uokoaji cha polisi chenye K9,yaani bado uokoaji wa miaka ya 47s hadi leo bado upo!kweli safari yetu ni ndefu mno!tunatumia fedha nyingi kuwa na vikosi maalum vya kukimbizana mitaani na wapinzani wa kisiasa,,ndio maana hii wizara ife na tuijenge upya kitaalamu.
 
Daah inasikitisha sana yaani mbarali bado wana madaraja ya aina hiyo licha ya kwamba kuna kilimo kikubwa cha mpunga toka miaka hiyo na mikataba ya uwekezaji tunasikia kila kukicha.
 
Daraja la miti limegharimu maisha ya mwananchi inasikitisha sana.
Poleni sana wafiwa
 
Back
Top Bottom