Mbarali: Wahujumu uchumi wahukumiwa kulipa Tsh. Milioni 65.5

Mbarali: Wahujumu uchumi wahukumiwa kulipa Tsh. Milioni 65.5

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waliopewa adhabu hiyo ni George Kagomba aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Ferdinand Manyele Mweka Hazina wa wilaya, Athuman Mwasomba aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Ujenzi.

Wengine ni Bakari Nyamu aliyekuwa Mtakwimu Wilaya ya Mbarali, George Mbilla aliyekuwa Diwani, Mikidadi Mwanzembe aliyekuwa Mtendaji Kata na Ponsiano Ngwando aliyekuwa Mtendaji Kata ya Rujewa.

Mahakama ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya iliwatia hatiani kwa kufanya ubadhirifu wa Tsh. Milioni 63.1 ambazo wameagizwa kuzirejesha. Pesa hizo zilipangwa kujenga madarasa ya Shule za Sekondari Rujewa na Ubaruku mwaka 2011.

Pia washtakiwa hao kwa pamoja watatakiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 2.4.
 
Nchi imejaa mchwa kuanzia chini mpaka juu! Hakuna mwenye uchungu. Kila anayepata nafasi ya kusimamia miradi ya wananchi, anawaza kuiba kwanza.
 
Back
Top Bottom