Mbaroni kwa tuhuma za kuua akijaribu kutoa mimba

Mbaroni kwa tuhuma za kuua akijaribu kutoa mimba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
JESHI la Polisi mkoani Kagera linamshikiria Frodius Protace ‘Gafseki’ (24) mkazi wa Kijiji cha Rushe wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua Saraiya Idd (25) mkazi wa Kijiji cha Mabuye wilayani Misenyi wakati akijaribu kumtoa mimba ya miezi sita kwa malipo ya Sh 600,000.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi alisema mwili wa marehemu uligundulika Oktoba 12 mwaka huu ukiwa umezikwa katika shamba la Anastela Jacob (47).

“Baada ya mwili huo kufukuliwa chini ya usimamizi wa Polisi, tukio hilo liliripotiwa kama kifo chenye mashaka kwa sababu ya kutotambulika lakini pia kukutwa na dalili za kutolewa mimba na kutokwa damu nyingi sehemu za siri na kuwekwa pamba puani.

“Kufuatia uchunguzi uliofanywa, polisi ilifanikiwa kupata taarifa za mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo ndipo alikamatwa na kufanyiwa upekuzi katika makazi yake,” alisema.

Malimi alisema baada ya kufanyiwa upekuzi katika chumba alichokuwa akiishi kulipatikana matandiko kitandani yenye damu na kitambulisho cha mpiga kura cha marehemu.

Aidha Malimi alisema katika mahojiano mtuhumiwa alikiri kushiriki mafunzo ya kozi fupi ya ufamasia lakini hajawahi kuajiriwa serikalini wala kwenye sekta binafsi.

Katika tukio lingine, mahakama ya Wilaya ya Ngara imemhukumu kifungo cha maisha gerezani, Ayubu John (20) kwa kosa la kumbaka mtoto wa dada yake mwenye miaka nane.

Malimi alisema Ayubu ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyakaribi wilayani Ngara alikamatwa na Polisi Oktoba 11, mwaka huu nyumbani kwake kwa kosa la kumbaka mtoto wa dada yake na kumfikisha katika mahakama ya Wilaya hiyo Oktoba 13, mwaka huu.

“Mtuhumiwa akiwa mahakani alikiri kosa la kumbaka mtoto huyo aliyekuwa anaishi naye nyumbani kwake kwa kumlazimisha jambo lililopelekea kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani,” alisema Malimi.
 
Miezi 6 unatoaje kienyeji hivyo? Achilia mbali kutoa mimba tu ni kosa kisheria na kwa Mungu pia.
 
Marehemu alikosea sana kukubali au kupeopose hili zoezi.

Mungu ampe kinachomstahili na huyu bwege aliyetenda kosa hilo sheria imzawadie kujaa na kufurika
 
hata mi hua namuomba Mungu demu akitoa mimba na yeye afe hapo hapo ...
 
Una uhakika Wewe katika historia yakO nzima ya Kimaisha haujawahii Kuua Kilazima ( Kutoa Mimba ) hivyo au unataka 'Kutuzuga' tu Sisi hapa JF?
kawaida mimba hua kiumbe hai baada ya siku 120 ...
kwa hio ukitoa mimba baada ya siku 120 umeua mtu ambaye yuko hai ila ukitoa kabla ya hapo hatuwezi kusema umeua.
 
kawaida mimba hua kiumbe hai baada ya siku 120 ...
kwa hio ukitoa mimba baada ya siku 120 umeua mtu ambaye yuko hai ila ukitoa kabla ya hapo hatuwezi kusema umeua.
Kabla ya siku 120 mimba inakuwa ni kiumbe mfu?
 
Na Ukifatilia hapa aliyefariki ndiye aliyelazimisha kweli kweli hichi kitendo kifanyike.
 
kawaida mimba hua kiumbe hai baada ya siku 120 ...
kwa hio ukitoa mimba baada ya siku 120 umeua mtu ambaye yuko hai ila ukitoa kabla ya hapo hatuwezi kusema umeua.
BIG NO.Ndugu yangu Kamdudu,mimi nimekuwa Mwenyekiti wa Pro life kwa miaka miwili,Watu wengi waliokuwa na mawazo km ya kwako tulikuwa tunawasahihisha;Kwa taarifa yako mtu anahesabika tangu saa ile mimba inatungwa,niulize kwanini; Sababu ni kuwa Mungu anakuwa ameweka pumzi yake ya uhai on the Sport mimba inapotungwa.Thus why Mungu mwenyewe anasema alitujua kabla ya kutungwa mimba,tukiwa tunatungwa mimba ktk matumbo ya mama zetu,yeye alishatujua,rejea Yeremia 1:5.Hivyo Binadamu huanza kuhesabika tangu mimba inapotungwa.
 
mi nimeongea kwa mjibu wa maneno yake mwenyewe Mwenyezi Mungu sijatoa kichwani mwangu !

qur'an 23:14. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji

hayo maneno niliyoongea mimi hapo juu ni ufafanuzi Mtume Muhammad s.a.w akifafanua aya hizo hapo juu.

ulishawahi kujiuliza kwa nini mama mjamzito anaanza clinic baada ya miezi 4 ya ujauzito ????

endelea kufuatilia haya mambo utajua zaidi
 
Kabla ya siku 120 mimba inakuwa ni kiumbe mfu?

ndani ya siku hizo kinachokua ninafanyika ni hiki hapa :

qur'an 23:14. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji

baada ya siku 120 ndio moyo una_star on na mtoto kuanza kupumua baada ta kupuliziwa nafsi ndio huitwa kiumbe hai sasa
 
Miezi 6 unatoaje kienyeji hivyo? Achilia mbali kutoa mimba tu ni kosa kisheria na kwa Mungu pia.
Kwa uzoefu wako[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]upi ni wakati sahihi kutoa mimba sasa kama sio miezi sita tupe uzoefu mnatoa wakati gani?
 
Back
Top Bottom