kamdudu
JF-Expert Member
- Jan 20, 2015
- 2,007
- 1,931
Mkuu nimekusoma,naomba niendelee kukudodosa;Kwa hiyo ktk Uislamu wana ndoa wanaruhusiwa kutoa mimba?
Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
Mimba ikishaingia hata ikiwa iko katika kiwango kidogo hata siku moja kinakuwa ni kiumbe mbali na kuwa hakijatiwa roho. Uislamu umekataza kiumbe kuuliwa isipokuwa kukiwa na dharura hiyo.
Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anasema:
“Wala msiwaue wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi Tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa” (al-Israa’ (17): 31).
ila
Mimba inaweza kutolewa ikiwa mwanamke ataambiwa na daktari mzoefu na aliyebobea katika taaluma ya kizazi na awe Muislamu mcha Mngu kuwa kuendelea kubeba mimba hiyo itakuwa ni hatari kwa mama.
La si hivyo basi itakuwa haifai kuitoa kabisa na mwenye kutoa atakuwa na dhambi kubwa mbele ya Allah Aliyetukuka.